Helium Tanzania: Chanzo, Utafiti, Faida, na Mwelekeo wa baadaye

GodfreyTara

New Member
Sep 12, 2023
3
5
.Mradi wa Helium Tanzania:
Chanzo, Utafiti, Faida, na Mwelekeo wa Baadaye.

Utangulizi:

Helium, gesi adimu isiyoweza kuchoma, isiyo na harufu, isiyoonekana, na isiyo na ladha, imekuwa ikipata umaarufu katika sayansi na viwanda kwa zaidi ya karne moja. Lakini, je, wewe unajua kwanini gesi hii inapata umaarufu mkubwa nchini Tanzania?
Fuatilia katika makala yangu Hii ambayo imechambua kwa kina kuhusu ugunduzi, uchimbaji, na umuhimu wa helium kwa Tanzania na dunia kwa ujumla.

Chanzo na Ugunduzi wa Helium Tanzania:

Tanzania, ikiwa na bonde la ufa linalofahamika kijiolojia kama Bonde la Ufa la Afrika Mashariki, imeanza kujitokeza kama mmojawapo wa wazalishaji wakubwa wa helium duniani. Kulingana na takwimu, inakadiriwa kuwa Tanzania ina akiba ya futi bilioni 138 za ujazo wa helium, hii ni baada ya kugundulika kwa akiba ya futi bilioni 54 za ujazo wa gesi hiyo mnamo 2016 katika Ziwa Rukwa.

IMG_0518.jpeg

Kampuni Zinazohusika na Helium:

Kampuni mbili kubwa zimejitokeza kufanya utafiti wa kina na uchimbaji wa helium nchini Tanzania.
Kampuni ya Helium One na Noble Helium zimeonesha nia ya dhati katika kutambua na kuchimba gesi hii. Zaidi ya hayo, kampuni hizi mbili zilishirikiana kutafuta rig ya kuchimbia gesi hiyo katika Bonde la Rukwa. Kwa sasa, zote zinafanya kazi ya uchimbaji katika eneo hilo.
Heliumone1 ana eneo la 2,965 km² pia NobleHelium ana Eneo lenye 5,464 km².
Yanayonesha kiwango kikubwa cha helium
Kuifanya Tanzania kuongoza katika uchimbaji,uzalishaji na usafirishaji wa gesi Hii Ya Helium Duniani.

IMG_0521.jpeg

Tanzania inatarajia kuanza uzalishaji wa helium mnamo 2025 ikiwa mipango itaenda kama ilivyopangwa,huku utafiti ukiendelea katika Bonde la ufa la Rukwa,Balangda na Ziwa Eyasi.

IMG_0457.jpeg

IMG_0520.jpeg

Jinsi Helium Inavyopatikana:

Kijiolojia, mchakato wa uzalishaji wa helium unatokana na kuoza kwa elementi za Uranium na Thorium zilizomo katika ganda la bara la kale. Gesi hii inaachiliwa wakati ganda linapovunjika kutokana na nguvu za tektoniki. Ganda hilo la kale linapovunjika, inaachilia gesi ya helium ambayo kisha inakusanywa.

Utafiti kutoka Chuo Kikuu cha Oxford unakadiria kuwa futi bilioni 700,000 za ujazo wa helium zimezalishwa katika Craton ya Tanzania katika kipindi cha miaka bilioni 2.5.
Helium inaachiliwa na majimaji moto wakati mwamba wa msingi (Basement) unapopasuka

Umuhimu wa Helium Duniani:

Kama gesi adimu, helium ina matumizi mengi katika sekta mbalimbali.

Sekta ya Matibabu: Helium hutumika katika MRI scanners na mifumo ya kupumulia, kwa sababu ya tabia zake zisizoweza kureact na molekuli nyingine.

IMG_0449.jpeg

-Teknolojia: Inahitajika katika utengenezaji wa semi-conductors, fiber-optics na katika data centres

IMG_0448.jpeg
IMG_0445.jpeg

Kutokana na uzito wake mdogo na uwezo wa kufikia joto la chini sana.

Utafiti wa Anga (Space Exploration) : Hutumika katika shughuli za anga kama vile uchunguzi wa roketi na kutambua uvujaji.
IMG_0444.jpeg

Nishati: Helium ina jukumu kubwa katika sekta ya nishati, haswa katika nyuklia.

IMG_0447.jpeg

Mwelekeo wa Baadaye:

Kwa kuangalia mbele, Tanzania ina nafasi kubwa katika soko la dunia la helium. Bei ya helium imeongezeka kwa zaidi ya 135% katika miaka minne iliyopita, na soko lake linakadiriwa kuwa na thamani ya zaidi ya dola bilioni 2.7. Kwa Tanzania, hii inamaanisha kuwa nchi inaweza kujipatia mapato makubwa kutokana na uzalishaji na uuzaji wa gesi hii.

Kama bidhaa yenye thamani kubwa, helium katika hali yake ya kimiminika inaweza kusafirishwa kwa kutumia kontena za ISO zilizowekwa kwenye malori bila haja ya kutumia mabomba.

Utegemezi wa Teknolojia kwenye Helium katika karne Moja Hii :

Helium, gesi adimu ya kipekee na yenye uhaba mkubwa duniani, imekuwa chachu kuu katika mageuzi ya kiteknolojia kwa kipindi cha karne moja iliyopita. Uwepo wake haukujulikana kwa muda mrefu hadi takribani miaka mia moja iliyopita, ambapo matumizi yake yalizidi kugunduliwa kutokana na sifa zake za kipekee.

Katika enzi za Vita Baridi, ambayo inajulikana kama "Cold War" kwa Kiingereza, matumizi ya Helium yalishamiri. Upelelezi wa kijeshi mnamo miaka ya 1920 ulitegemea gesi hii, na hata zaidi wakati wa kilele cha Vita Baridi, ambapo Helium ilikuwa muhimu katika uendeshaji wa makombora ya masafa marefu na mifumo mingine ya ulinzi.

Zaidi ya matumizi hayo ya kijeshi, helium ikaja kutumika kwa kiasi kikubwa katika utafiti wa anga za juu, uzalishaji wa vifaa vya nusu-kendara (semiconductors) na nyaya za fiber optic, utabibu wa nyuklia, uunganishaji wa metali (welding) maalum, na hata katika upimaji wa uvujaji wa hewa.

Teknolojia za kijeshi na ulinzi wa mataifa makubwa zinategemea kwa kiasi kikubwa vifaa ambavyo katika uzalishaji au utendaji kazi wake vinahitaji Helium. Gesi hii imechukua nafasi kubwa hasa kutokana na sifa zake ambazo hazipatikani kwa gesi nyingine.

Miaka ya 1990 ilishuhudia ongezeko la matumizi ya Helium katika sekta ya cryogenics, hususan kwa matumizi ya mashine za MRI ambazo zilitegemea sumaku zinazofanya kazi katika hali ya baridi sana (superconducting magnets). Hii ilipelekea mahitaji ya Helium duniani kuongezeka kwa asilimia 30.

Katika miongo miwili iliyopita, umuhimu wa Helium umezidi kujitokeza. Ni gesi isiyoweza kubadilishwa na nyingine katika utengenezaji wa vifaa vya nusu-kendara vinavyotumika katika kompyuta, simu janja, magari yanayojiendesha apa unamkumbuka Elon musk na magari ya Tesla ,televisheni za kisasa, na hata katika vifaa vya kijeshi.
Sekta ya anga pia imeanza kutumia Helium kwa kiwango kikubwa, hasa kutokana na kuongezeka kwa kampuni binafsi zinazojihusisha na utafiti wa anga.

Tathmini ya Benki ya America pamoja na JP Morgan mnamo 2017 inabashiri kuwa sekta ya anga itakuwa na thamani ya dola za Kimarekani trilioni 3 (TSH 7.5 quadrillion au TSH trilioni 7,500) ifikapo mwaka 2050.
Hii inaonyesha jinsi gani Helium itakuwa na umuhimu wa kipekee katika miaka ijayo.

Ni wazi kuwa ugavi thabiti wa Helium ni jambo la msingi na linapaswa kutazamwa kama suala la kipaumbele kwa mustakabali wa sayari yetu. Ni wajibu wa jamii ya kimataifa kuhakikisha kuwa Helium inapatikana kwa wingi na kwa uhakika ili kutekeleza miradi mikubwa ya kiteknolojia inayosubiri siku za usoni na ndipo sisi kama Tanzania tutakapo nufaika na rasimali hii adhimu sana.

IMG_0516.jpeg

IMG_0514.jpeg

Kwa muhtasari,ugavi thabiti wa helium ni muhimu mno kwa mustakabali wa sayari yetu.

Kuna mabadiliko makubwa ya kiteknolojia yanayokuja ambayo yanaweza kutufanya tutumie helium nyingi zaidi hivi karibuni.

Ifikapo 2025,mradi mkubwa huko Ufaransa uitwao "ITER"(International Thermonuclear Experimental Reactor) unalenga kuonesha tunaweza kutengeneza umeme kwa kutumia Nyuklia ya fusion(Nuclear Fussion).
Njia yenye nguvu na safi ya kuzalisha nishati.
IMG_0515.jpeg

Nchi kadhaa na makampuni makubwa yanatumia mabilioni kwenye hili,kwa sababu ikiwa itafanya kazi,inaweza kutusaidia kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kwa kutupa umeme mwingi wa kijani kwa kutumia gesi hii ya Helium.
Hii ni muhimu sana kwa mustakabali wa sayari 🌍 yetu.
Majina makubwa kama Amazon, Google na Bill Gates pia wanawekeza kwenye miradi hii.

Kila mtu anashindania kuwa wa kwanza kupata suluhisho sahihi la Nishati kwa kutumia gesi hii ya Helium.

Kwa Tanzania,kuwa na akiba kubwa ya helium adimu inatoa fursa kubwa Mno.
Helium inaweza kutumika katika mchakato wa fusion pale majaribio ya ITER yatakapoisha na kuonesha Majibu Chanya na sisi kui-adapt na nchi kuzalisha umeme wa kijani na zaidi kwa kutumia teknolojia hii ya kisasa sana.
Hapa sasa nadhani Ile migao na kukatika kwa umeme itakuwa Historia kama ya Vita vya majimaji😊.

Hii itaweza kuchangia maendeleo ya kiuchumi na kiteknolojia nchini na kutoa nafasi ya Tanzania kuwa kiongozi na kinara katika uzalishaji wa nishati endelevu barani Afrika na Dunia kwa Ujumla wake.

Wakati dunia ikitoka kwenye Mageuzi na mapinduzi ya viwanda,sasa tukielekea kwenye mageuzi ya ki-digitali na Uku tukishuhudia mageuzi ya teknolojia za akili bandia, roboti, na mifumo mingine ya kiteknolojia inayobadilisha jinsi tunavyofanya kazi, kuwasiliana na kuishi.

Hitimisho:

Tanzania, chini ya uongozi thabiti wa Rais Dr. Suluhu Samia, ina fursa adimu na kubwa ya kuleta mabadiliko ya kiuchumi na kiteknolojia kupitia uzalishaji wa helium. Uzalishaji wa helium utatoa fursa nyingi kwa Watanzania, kuanzia ajira, mafunzo ya kiteknolojia, na hata fursa za biashara.

Ni muda wa muafaka kwa Tanzania 🇹🇿 kushiriki kikamilifu na kutumia fursa katika kipindi ambacho Tanzania imepata Rais Dr.SuluhuSamia na viongozi aliowachagua ambao wana nia ya dhati katika kuwaletea mabadiliko na kuwainua Watanzania.

Chini ya uongozi thabiti wa awamu ya 6,Rais Dr. SuluhuSamia amejitolea kuleta mageuzi ambayo yatawawezesha Watanzania kufikia maendeleo ya kiuchumi,kiteknolojia na kijamii
Mradi kama huu wa helium utatoa fursa nyingi kwa Watanzania, ikiwemo ajira zenye tija, mafunzo ya kiteknolojia
na fursa za biashara.
Zaidi ya hapo, wananchi wanaweza kufaidika na upatikanaji wa umeme wa bei nafuu, kuboreshwa kwa huduma za afya kupitia teknolojia mpya, na kuzalisha bidhaa zenye thamani kubwa kwa matumizi ya ndani na nje ya nchi.

Kwa kushirikiana na sekta binafsi na jamii
serikali inaweza kuunda mazingira ambayo yatawawezesha wajasiriamali na wakulima kufikia masoko mapya,kuongeza uzalishaji, na kuboresha maisha yao.
Pia, kuwepo kwa teknolojia mpya kutoka miradi kama hii kunaweza kusaidia katika kuboresha elimu,kutoa mafunzo ya ujuzi mpya kwa vijana, na kuwawezesha Watanzania kushiriki kikamilifu katika uchumi wa kisasa.

Chini ya uongozi wa Rais Suluhu, Tanzania ina kila kitu inachohitaji kufikia mafanikio hayo.
IMG_0285.jpeg

Ni jukumu letu sote kama Watanzania kushirikiana na serikali yetu, kuunga mkono juhudi hizi na kuhakikisha tunatumia kikamilifu fursa zinazotolewa ili kuinua maisha ya kila Mtanzania.
Baada ya 2025, Tanzania itakuwa imejikita kama tegemeo kuu katika soko la helium duniani.

IMG_0523.jpeg

Hakika, Tanzania ina nafasi kubwa ya kuwa kiongozi wa uzalishaji wa helium duniani. Hii si tu itachangia maendeleo ya kiuchumi na kiteknolojia nchini, bali pia itatoa nafasi kwa Tanzania kuchukua jukumu kubwa katika soko la dunia la gesi hii adimu.

Hii ni hatua ya kihistoria na inaashiria kipindi kipya cha mageuzi na maendeleo kwa Tanzania 🇹🇿

IMG_0529.jpeg

Helium One and Noble Helium to pool Tanzania rig sourcing | African EnergyLondon AIM-listed Helium One Global has entered an agreement with Australian Securities Exchange (ASX)-listed Noble Helium “to co-operate in sourcing and securing a suitable drilling rig” for drilling operations in the Rukwa Basin. Helium One said its Rukwa project is the “largest known primary helium resource in the world”.

In June, the University of Oxford and Norwegian exploration company Helium One announced the discovery of a significantly large deposit of helium gas in Tanzania. The deposit, only one of what the researchers believe to be many, contains a probable resource of about 1.5 billion cubic meters. By comparison, the U.S. Federal Helium Reserve currently holds 685 million cubic meters, and total known U.S. reserves are 4.3 billion cubic meters. Global helium consumption is running about 227 million cubic meters a year.
 
.Mradi wa Helium Tanzania:
Chanzo, Utafiti, Faida, na Mwelekeo wa Baadaye.

Utangulizi:

Helium, gesi adimu isiyoweza kuchoma, isiyo na harufu, isiyoonekana, na isiyo na ladha, imekuwa ikipata umaarufu katika sayansi na viwanda kwa zaidi ya karne moja. Lakini, je, wewe unajua kwanini gesi hii inapata umaarufu mkubwa nchini Tanzania?
Fuatilia katika makala yangu Hii ambayo imechambua kwa kina kuhusu ugunduzi, uchimbaji, na umuhimu wa helium kwa Tanzania na dunia kwa ujumla.

Chanzo na Ugunduzi wa Helium Tanzania:

Tanzania, ikiwa na bonde la ufa linalofahamika kijiolojia kama Bonde la Ufa la Afrika Mashariki, imeanza kujitokeza kama mmojawapo wa wazalishaji wakubwa wa helium duniani. Kulingana na takwimu, inakadiriwa kuwa Tanzania ina akiba ya futi bilioni 138 za ujazo wa helium, hii ni baada ya kugundulika kwa akiba ya futi bilioni 54 za ujazo wa gesi hiyo mnamo 2016 katika Ziwa Rukwa.

View attachment 2763238

Kampuni Zinazohusika na Helium:

Kampuni mbili kubwa zimejitokeza kufanya utafiti wa kina na uchimbaji wa helium nchini Tanzania.
Kampuni ya Helium One na Noble Helium zimeonesha nia ya dhati katika kutambua na kuchimba gesi hii. Zaidi ya hayo, kampuni hizi mbili zilishirikiana kutafuta rig ya kuchimbia gesi hiyo katika Bonde la Rukwa. Kwa sasa, zote zinafanya kazi ya uchimbaji katika eneo hilo.
Heliumone1 ana eneo la 2,965 km² pia NobleHelium ana Eneo lenye 5,464 km².
Yanayonesha kiwango kikubwa cha helium
Kuifanya Tanzania kuongoza katika uchimbaji,uzalishaji na usafirishaji wa gesi Hii Ya Helium Duniani.

View attachment 2763239

Tanzania inatarajia kuanza uzalishaji wa helium mnamo 2025 ikiwa mipango itaenda kama ilivyopangwa,huku utafiti ukiendelea katika Bonde la ufa la Rukwa,Balangda na Ziwa Eyasi.

View attachment 2763244
View attachment 2763243

Jinsi Helium Inavyopatikana:

Kijiolojia, mchakato wa uzalishaji wa helium unatokana na kuoza kwa elementi za Uranium na Thorium zilizomo katika ganda la bara la kale. Gesi hii inaachiliwa wakati ganda linapovunjika kutokana na nguvu za tektoniki. Ganda hilo la kale linapovunjika, inaachilia gesi ya helium ambayo kisha inakusanywa.

Utafiti kutoka Chuo Kikuu cha Oxford unakadiria kuwa futi bilioni 700,000 za ujazo wa helium zimezalishwa katika Craton ya Tanzania katika kipindi cha miaka bilioni 2.5.
Helium inaachiliwa na majimaji moto wakati mwamba wa msingi (Basement) unapopasuka

Umuhimu wa Helium Duniani:

Kama gesi adimu, helium ina matumizi mengi katika sekta mbalimbali.

Sekta ya Matibabu: Helium hutumika katika MRI scanners na mifumo ya kupumulia, kwa sababu ya tabia zake zisizoweza kureact na molekuli nyingine.

View attachment 2763225

-Teknolojia: Inahitajika katika utengenezaji wa semi-conductors, fiber-optics na katika data centres

View attachment 2763226View attachment 2763227

Kutokana na uzito wake mdogo na uwezo wa kufikia joto la chini sana.

Utafiti wa Anga (Space Exploration) : Hutumika katika shughuli za anga kama vile uchunguzi wa roketi na kutambua uvujaji.
View attachment 2763228

Nishati: Helium ina jukumu kubwa katika sekta ya nishati, haswa katika nyuklia.

View attachment 2763229

Mwelekeo wa Baadaye:

Kwa kuangalia mbele, Tanzania ina nafasi kubwa katika soko la dunia la helium. Bei ya helium imeongezeka kwa zaidi ya 135% katika miaka minne iliyopita, na soko lake linakadiriwa kuwa na thamani ya zaidi ya dola bilioni 2.7. Kwa Tanzania, hii inamaanisha kuwa nchi inaweza kujipatia mapato makubwa kutokana na uzalishaji na uuzaji wa gesi hii.

Kama bidhaa yenye thamani kubwa, helium katika hali yake ya kimiminika inaweza kusafirishwa kwa kutumia kontena za ISO zilizowekwa kwenye malori bila haja ya kutumia mabomba.

Utegemezi wa Teknolojia kwenye Helium katika karne Moja Hii :

Helium, gesi adimu ya kipekee na yenye uhaba mkubwa duniani, imekuwa chachu kuu katika mageuzi ya kiteknolojia kwa kipindi cha karne moja iliyopita. Uwepo wake haukujulikana kwa muda mrefu hadi takribani miaka mia moja iliyopita, ambapo matumizi yake yalizidi kugunduliwa kutokana na sifa zake za kipekee.

Katika enzi za Vita Baridi, ambayo inajulikana kama "Cold War" kwa Kiingereza, matumizi ya Helium yalishamiri. Upelelezi wa kijeshi mnamo miaka ya 1920 ulitegemea gesi hii, na hata zaidi wakati wa kilele cha Vita Baridi, ambapo Helium ilikuwa muhimu katika uendeshaji wa makombora ya masafa marefu na mifumo mingine ya ulinzi.

Zaidi ya matumizi hayo ya kijeshi, helium ikaja kutumika kwa kiasi kikubwa katika utafiti wa anga za juu, uzalishaji wa vifaa vya nusu-kendara (semiconductors) na nyaya za fiber optic, utabibu wa nyuklia, uunganishaji wa metali (welding) maalum, na hata katika upimaji wa uvujaji wa hewa.

Teknolojia za kijeshi na ulinzi wa mataifa makubwa zinategemea kwa kiasi kikubwa vifaa ambavyo katika uzalishaji au utendaji kazi wake vinahitaji Helium. Gesi hii imechukua nafasi kubwa hasa kutokana na sifa zake ambazo hazipatikani kwa gesi nyingine.

Miaka ya 1990 ilishuhudia ongezeko la matumizi ya Helium katika sekta ya cryogenics, hususan kwa matumizi ya mashine za MRI ambazo zilitegemea sumaku zinazofanya kazi katika hali ya baridi sana (superconducting magnets). Hii ilipelekea mahitaji ya Helium duniani kuongezeka kwa asilimia 30.

Katika miongo miwili iliyopita, umuhimu wa Helium umezidi kujitokeza. Ni gesi isiyoweza kubadilishwa na nyingine katika utengenezaji wa vifaa vya nusu-kendara vinavyotumika katika kompyuta, simu janja, magari yanayojiendesha apa unamkumbuka Elon musk na magari ya Tesla ,televisheni za kisasa, na hata katika vifaa vya kijeshi.
Sekta ya anga pia imeanza kutumia Helium kwa kiwango kikubwa, hasa kutokana na kuongezeka kwa kampuni binafsi zinazojihusisha na utafiti wa anga.

Tathmini ya Benki ya America pamoja na JP Morgan mnamo 2017 inabashiri kuwa sekta ya anga itakuwa na thamani ya dola za Kimarekani trilioni 3 (TSH 7.5 quadrillion au TSH trilioni 7,500) ifikapo mwaka 2050.
Hii inaonyesha jinsi gani Helium itakuwa na umuhimu wa kipekee katika miaka ijayo.

Ni wazi kuwa ugavi thabiti wa Helium ni jambo la msingi na linapaswa kutazamwa kama suala la kipaumbele kwa mustakabali wa sayari yetu. Ni wajibu wa jamii ya kimataifa kuhakikisha kuwa Helium inapatikana kwa wingi na kwa uhakika ili kutekeleza miradi mikubwa ya kiteknolojia inayosubiri siku za usoni na ndipo sisi kama Tanzania tutakapo nufaika na rasimali hii adhimu sana.

View attachment 2763232
View attachment 2763231

Kwa muhtasari,ugavi thabiti wa helium ni muhimu mno kwa mustakabali wa sayari yetu.

Kuna mabadiliko makubwa ya kiteknolojia yanayokuja ambayo yanaweza kutufanya tutumie helium nyingi zaidi hivi karibuni.

Ifikapo 2025,mradi mkubwa huko Ufaransa uitwao "ITER"(International Thermonuclear Experimental Reactor) unalenga kuonesha tunaweza kutengeneza umeme kwa kutumia Nyuklia ya fusion(Nuclear Fussion).
Njia yenye nguvu na safi ya kuzalisha nishati.
View attachment 2763214

Nchi kadhaa na makampuni makubwa yanatumia mabilioni kwenye hili,kwa sababu ikiwa itafanya kazi,inaweza kutusaidia kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kwa kutupa umeme mwingi wa kijani kwa kutumia gesi hii ya Helium.
Hii ni muhimu sana kwa mustakabali wa sayari 🌍 yetu.
Majina makubwa kama Amazon, Google na Bill Gates pia wanawekeza kwenye miradi hii.

Kila mtu anashindania kuwa wa kwanza kupata suluhisho sahihi la Nishati kwa kutumia gesi hii ya Helium.

Kwa Tanzania,kuwa na akiba kubwa ya helium adimu inatoa fursa kubwa Mno.
Helium inaweza kutumika katika mchakato wa fusion pale majaribio ya ITER yatakapoisha na kuonesha Majibu Chanya na sisi kui-adapt na nchi kuzalisha umeme wa kijani na zaidi kwa kutumia teknolojia hii ya kisasa sana.
Hapa sasa nadhani Ile migao na kukatika kwa umeme itakuwa Historia kama ya Vita vya majimaji😊.

Hii itaweza kuchangia maendeleo ya kiuchumi na kiteknolojia nchini na kutoa nafasi ya Tanzania kuwa kiongozi na kinara katika uzalishaji wa nishati endelevu barani Afrika na Dunia kwa Ujumla wake.

Wakati dunia ikitoka kwenye Mageuzi na mapinduzi ya viwanda,sasa tukielekea kwenye mageuzi ya ki-digitali na Uku tukishuhudia mageuzi ya teknolojia za akili bandia, roboti, na mifumo mingine ya kiteknolojia inayobadilisha jinsi tunavyofanya kazi, kuwasiliana na kuishi.

Hitimisho:

Tanzania, chini ya uongozi thabiti wa Rais Dr. Suluhu Samia, ina fursa adimu na kubwa ya kuleta mabadiliko ya kiuchumi na kiteknolojia kupitia uzalishaji wa helium. Uzalishaji wa helium utatoa fursa nyingi kwa Watanzania, kuanzia ajira, mafunzo ya kiteknolojia, na hata fursa za biashara.

Ni muda wa muafaka kwa Tanzania 🇹🇿 kushiriki kikamilifu na kutumia fursa katika kipindi ambacho Tanzania imepata Rais Dr.SuluhuSamia na viongozi aliowachagua ambao wana nia ya dhati katika kuwaletea mabadiliko na kuwainua Watanzania.

Chini ya uongozi thabiti wa awamu ya 6,Rais Dr. SuluhuSamia amejitolea kuleta mageuzi ambayo yatawawezesha Watanzania kufikia maendeleo ya kiuchumi,kiteknolojia na kijamii
Mradi kama huu wa helium utatoa fursa nyingi kwa Watanzania, ikiwemo ajira zenye tija, mafunzo ya kiteknolojia
na fursa za biashara.
Zaidi ya hapo, wananchi wanaweza kufaidika na upatikanaji wa umeme wa bei nafuu, kuboreshwa kwa huduma za afya kupitia teknolojia mpya, na kuzalisha bidhaa zenye thamani kubwa kwa matumizi ya ndani na nje ya nchi.

Kwa kushirikiana na sekta binafsi na jamii
serikali inaweza kuunda mazingira ambayo yatawawezesha wajasiriamali na wakulima kufikia masoko mapya,kuongeza uzalishaji, na kuboresha maisha yao.
Pia, kuwepo kwa teknolojia mpya kutoka miradi kama hii kunaweza kusaidia katika kuboresha elimu,kutoa mafunzo ya ujuzi mpya kwa vijana, na kuwawezesha Watanzania kushiriki kikamilifu katika uchumi wa kisasa.

Chini ya uongozi wa Rais Suluhu, Tanzania ina kila kitu inachohitaji kufikia mafanikio hayo.
View attachment 2763235

Ni jukumu letu sote kama Watanzania kushirikiana na serikali yetu, kuunga mkono juhudi hizi na kuhakikisha tunatumia kikamilifu fursa zinazotolewa ili kuinua maisha ya kila Mtanzania.
Baada ya 2025, Tanzania itakuwa imejikita kama tegemeo kuu katika soko la helium duniani.

View attachment 2763250

Hakika, Tanzania ina nafasi kubwa ya kuwa kiongozi wa uzalishaji wa helium duniani. Hii si tu itachangia maendeleo ya kiuchumi na kiteknolojia nchini, bali pia itatoa nafasi kwa Tanzania kuchukua jukumu kubwa katika soko la dunia la gesi hii adimu.

Hii ni hatua ya kihistoria na inaashiria kipindi kipya cha mageuzi na maendeleo kwa Tanzania 🇹🇿

View attachment 2763252
Helium One and Noble Helium to pool Tanzania rig sourcing | African EnergyLondon AIM-listed Helium One Global has entered an agreement with Australian Securities Exchange (ASX)-listed Noble Helium “to co-operate in sourcing and securing a suitable drilling rig” for drilling operations in the Rukwa Basin. Helium One said its Rukwa project is the “largest known primary helium resource in the world”.

In June, the University of Oxford and Norwegian exploration company Helium One announced the discovery of a significantly large deposit of helium gas in Tanzania. The deposit, only one of what the researchers believe to be many, contains a probable resource of about 1.5 billion cubic meters. By comparison, the U.S. Federal Helium Reserve currently holds 685 million cubic meters, and total known U.S. reserves are 4.3 billion cubic meters. Global helium consumption is running about 227 million cubic meters a year.
Hivi Tanzanite imeisha??
 
Back
Top Bottom