Tetesi: Tanzania inalipwa mabilioni ya fedha toka nje ambazo zimefanywa siri na serikali hazina rekodi, tumenunulia ndege, na kujenga SGR na Stiegler nk

Umeandika pumba tupu na katika hilo swala la helium hujui chochote
Kwa taarifa yako tu ipo kiasi cha futi cubic 54 billion ambazo kwenye soko la dunia huo mzigo ni kama trillion 10 hivi hapo hajaingia mkataba na wamiliki wa kitalu kutoa gharama za utafutaji na uchimbaji unakuja potosha umma hapo hizi akili za nyumbu wa DJ

Sent using Jamii Forums mobile app
Hapa hujanyoosha popote juu ya "upotoshaji" unaodai mleta mada anaufanya. Badala yake unabwabwaja mambo tofauti kabisa!
Hukuweka chochote kinachoonyesha upotoshaji ni upi, na ukweli ni upi. Mmesoma shule za wapi kiasi hata kuelewa mada mnashindwa?

Hivi nyinyi walevi mnatokea wapi?
 
Hili ni sawa kabisa.
Kuna tofauti kubwa sana kulisema na kulitekeleza.

Ndio, tutafaidika kidogo na mikataba hii mipya kuliko ilivyokuwa hapo zamani, lakini mwelekeo bado ni ule ule wa kuchimba na kusafirisha nje.
Tunayo madini ya graphite sehemu mbalimbali nchini, yanachimbwa na kusombwa, wala hatutaki kujua yanatumika kutengeneza mali zipi, ili nasi tujaribu kutengeneza mali hizo tuwauzie wengine.

Hiyo helium, hivyo hivyo. Utajiri wetu ni wa kuchimba na kusafirisha. Huko ndiko kufaidika na utajiri huo?

Hawa vijana wanaomaliza vyuo na kukaa vijiweni, hatuuoni huo utajiri tunaoupoteza bure? Kwa nini kusiwe na mikakati ya kuwaunganisha vijana hawa na hizi mali zetu ili tufaidike zaidi nazo kikamilifu!

Sasa najua sitaeleweka, lakini ukweli ni kwamba bado hatuna mipango endelevu ya kuutumia huu utajiri tulio nao kikamilifu.
Kweli kabisa..point..
 
Najaribu kujiuliza lakini sipati jibu! hizo fedha nyingi zinazotolewa kwa siri na bila mfumo rasmi wowote was serikali zitalipwa vipi na serikali (tz) zijazo kwa hao wanao zitowa ?

Ina maana watoaji wanatapeliwa!

Kama wanajenga na kufanya miradi mikubwa ya maendeleo ni vizuri na huo ni uzalendo, labda ulitaka iweje ?

Wazifiche hizo fedha ughaibuni !!!

Nchi masikini kama tZ. cha kupambana hapo(helium) ni kupata tuu kodi yetu ya haki kwa hao watao wekeza na kufanya nao mikataba sahihi yenye tija siyo ya akina Mangungu!

Suala nyeti kiasi hicho lataka utulivu , tujifunze toka kwa majirani zetu eg . DRC

Tufanye kazi kwanza biashara kubwa kama hiyo unazoshindana na nchi zilizokwisha endelea kama USA ni .......... wakati sisi hatuna technolog,wataalamu wala wazoefu ni ngumu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tetesi zlizopo ni kwamba serikali ya Tanzania imekuwa ikilipwa mabilioni ya fedha na kampuni za nje lakini fedha hizi zimefanywa siri bila kuingizwa katika kasri za serikali, na hivyo kuwa nje ya wigo wa ukaguzi wa serikali kutia na CAG. Hili ndilo simulizi lililopo.

Nitawawapa dondoo za mazungumzo yaliyofanyika.

"Asikudanganye mtu, suala la Tanzania kununua ndege kwa fedha za kodi na pia kujenga Stiegler na SGR, daraja la Salenda na hizo flyover na mabarabara na miradi mikubwa inayofanyika, sio kwamba ni fedha za kodi. Tanzania haina ubavu huo wa fedha za kodi kufanya miradi mikubwa kama hiyo. Mnadanganywa. Tanzania imekuwa ikilipwa mabilioni ya fedha ambayo zimefanywa siri, na uongozi wa nchi kutumia fedha hizo kama mtaji wa kisiasa".

Lakini je, fedha hizo zinatoka wapi, na kwa nini Tanzania ilipwe? Simulizi linaendelea.

"Fedha hizo ni fedha za Helium ya Tanzania. Katika nchi ambazo zimebarikiwa rasilimali asili Tanzania labda inaongoza. Kuanzia miaka ya 2010 dunia ilionekana kwamba inaishiwa gesi ya Helium ambayo imekuwa ikitengenezwa viwandani na kuuzwa kwa bei kubwa"

"Kuna nchi sita tu duniani zinazozalisha Helium kwa sasa, na viwanda 14 duniani. Karibu nusu ya hii gesi inatoka USA. na theruthi moja inatoka Qatar. Sasa viwanda vyote hivi 14 vilivyopo duniani, vinazalisha Helium kutokana na natural gas. Tanzania ni nchi pekee duniani ambayo Helium imepetikana ardhini kwa wingi sana na ndio maana sasa iko katika nafasi ya kuongoza soko la Helium duniani".

"Hii gesi inapopatikana ardhini inakuwa na concentration ya wastani wa 2% na hivyo kufanya bei yake kuwa juu sana kwa kuchimba, na ndio maana inazalishwa viwandani. Sasa jambo moja la ajabu lilitokea. Mwaka 2015 wataalamu waligundua hii gesi Tanzania ikiwa inapatikana kwa kiwango cha juu sana, kati ya 5-15%. Hii ilifanya Tanzania kuwa nchi pekee ambayo ina Helium ardhini ambayo inaweza kuchimbwa na kuzalishwa kwa gharama ya chini kuliko inavyozalishwa na viwanda hivi 14 katika nchi 6 duniani. Na matokeo ni kwamba Tanzania ikajikuta katika nafasi ya kuongeongoza soko la Helium duniani, kama ambavyo Saudi Arabia inaongoza soko la mafuta duniani."

"Kwa sasa kuna upungufu mkubwa wa Helium. Kufuatia upungufu wa hii gesi, Marekani hata walianza kuweka hifadhi kubwa ya gesi hii kwa ajili ya matumizi ya baadae. Upungufu wa hii gesi umefanya bei yake uongezeka kwa zaidi ya asilimia 135% kwa mwaka mmoja tu!"

"Hii gesi ya Helium ni muhimu sana na itaipaisha Tanzania kiuchumi kuliko hata kama ingekuwa na mafuta. Matumizi ya hii gesi ni pamoja na kwenye mambo kama welding na hata utaalamu wa space (kwa kiingereza uses of Helium gas: are arc welding, chromatography, medical lasers, optical fiber, intercontinental ballistic missiles, space travel, etc)"

"Lakini sasa kukawa na tatizo. Ikiwa Tanzania ingeruhusiwa kuchimba hii Helium na kuuza, basi ingeuza kwa bei poa kiasi kwamba ingeua kabisa uzalishaji wa hivi viwanda 14, USA akiwa mzalishaji mkubwa. Basi inaonekana kulikuwa na makubaliano kwamba Tanzania icheleweshe uzalishaji wa Helium hadi wakati unaokubalika. Lakini kwa kufanya hivyo, lazima kulikuwa na makubaliano kwamba Tanzaia ilipwe fedha nyingi kama "compensation" ya kuzuia uzalishaji wa Helium ili kunusuru kampuni zinazouza Helium kwa sasa. Hiyo ndiyo fedha inayofanya miradi yenu ambayo wanasiasa wenu wanawaambia eti ni kodi za wananchi ili kuji-promote kisiasa. Habari ya ugunduzi wa Heluim Tanzania na umuhimu wa hii gesi katika soko la dunia, ilipaswa kuwa kubwa kuliko kama Tanzania ingegundua mafuta. Sasa jiulize, kwa nini wanasiasa wenu wamekaa kimya kuhusu huu ugunduzi mkubwa uliofanyika Tanzania? Tanzania ni nchi pekee duniani unapata Helium ardhini na utatawala soko la dunia kama ilivyo kwa Tanzanite, na mnakaa kimya, kwa nini?"

NB: Kwa wale mnaochangia mada hii bila kufikirisha sana ubongo wenu, jiulizeni jambo hili: Je implications za Tanzania kuwa nchi pekee duniani yenye Helium inayopatikana ardhini kwa wingi, ambayo inaweza kuua soko la nchi 6 pekee duniani zinazozalisha Helium kwa sasa, huku Marekani ikiwa imeshikilia zaidi ya asilimia 50% ya soko hilo, ni nini? Jiulizeni pia kwa nini serikali yetu imekaa kimya sana kuhusu huu ugunduzi wa Helium nchini ambayo itatatuweka karibu sawa kimapato na nchi zinazozalisha mafuta?

Pia tafakarini sana kile Bloomberg wamesema kuhusu ugunduzi wa Helium Tanzania, "With such extreme sensitivity in this market, a big new helium source could, just maybe, transform a whole country’s economy. A country such as, say, Tanzania".

Mwisho tafakarini sana matumizi ya Helium, kutia ndani matumizi yake katika makombora ya masafa marefu (intercontinental ballistic missiles), space travel, chromatography, medical lasers, optical fiber nk

Reference: In Photos: Massive Underground Helium Reserve Found in Tanzania
Reference: That huge helium deposit under Tanzania is even bigger than we thought
Reference: Tanzania could become top helium producer - African Business Magazine

Taarifa ya Bloomberg Businessweek juu ya Helium ya Tanzania
2019-08-28

Among the key uses for helium today are arc welding, chromatography, medical lasers, optical fiber, intercontinental ballistic missiles, and space travel. The Large Hadron Collider, the particle accelerator outside Geneva wrestling with the biggest questions of physics, needs 120 metric tons of helium a week to keep running. Helium can make things superconductive, meaning they can transmit electricity basically forever without generating any heat, and other helium properties make the element essential for semiconductor manufacturing. Every MRI machine in the world bathes its magnetic coils in liquid helium to prevent overheating.

Like the price of lithium, the price of helium is one of the more opaque among commodities, but reports said it jumped 135% from the previous year. With such extreme sensitivity in this market, a big new helium source could, just maybe, transform a whole country’s economy. A country such as, say, Tanzania.

Helium prices

Current price: $37.50 per 1000 cubic feet
View attachment 1331611
Mwanzo mlidai JPM alikuwa anakusanya malimbikizo ya kodi za awamu ya tatu, hamkuishia hapo mkaenda kuchongea kwenye taasisi kubwa za fedha ili tunyimwe mikopo nalo halikusaidia miradi inaendelea kuota kama uyoga na hakuna kuishiwa.Mmegundua serikali inaendelea kuanzisha miradi mikubwa kwa pesa zake sasa unaanza ngonjera za Herium. Bavicha mnakaazi by the way mmepata mgombea urais ??? Kisulisuli kinawaangukia kuanzia june
 
Ni napata ukakasi......bring mkeka kuonesha malipo......Mimi ni opposition, some good things I note with great honor and applaud...... What troubles me though ni uhai wa watu wetu na hali zetu!
 
Recall:

Tutaongea kila kitu na kukitilia shaka lakini sio suala la uwepo wa gesi ya Helium Tanzania. Hadi sasa waliosimamisha uchimbaji sio Helium One, ni serikali. Na kumbuka taarifa kuhusu uwepo wa hiigesi sio za Helium One
 
Tetesi zlizopo ni kwamba serikali ya Tanzania imekuwa ikilipwa mabilioni ya fedha na kampuni za nje lakini fedha hizi zimefanywa siri bila kuingizwa katika kasri za serikali, na hivyo kuwa nje ya wigo wa ukaguzi wa serikali kutia na CAG. Hili ndilo simulizi lililopo.

Nitawawapa dondoo za mazungumzo yaliyofanyika.

"Asikudanganye mtu, suala la Tanzania kununua ndege kwa fedha za kodi na pia kujenga Stiegler na SGR, daraja la Salenda na hizo flyover na mabarabara na miradi mikubwa inayofanyika, sio kwamba ni fedha za kodi. Tanzania haina ubavu huo wa fedha za kodi kufanya miradi mikubwa kama hiyo. Mnadanganywa. Tanzania imekuwa ikilipwa mabilioni ya fedha ambayo zimefanywa siri, na uongozi wa nchi kutumia fedha hizo kama mtaji wa kisiasa".

Lakini je, fedha hizo zinatoka wapi, na kwa nini Tanzania ilipwe? Simulizi linaendelea.

"Fedha hizo ni fedha za Helium ya Tanzania. Katika nchi ambazo zimebarikiwa rasilimali asili Tanzania labda inaongoza. Kuanzia miaka ya 2010 dunia ilionekana kwamba inaishiwa gesi ya Helium ambayo imekuwa ikitengenezwa viwandani na kuuzwa kwa bei kubwa"

"Kuna nchi sita tu duniani zinazozalisha Helium kwa sasa, na viwanda 14 duniani. Karibu nusu ya hii gesi inatoka USA. na theruthi moja inatoka Qatar. Sasa viwanda vyote hivi 14 vilivyopo duniani, vinazalisha Helium kutokana na natural gas. Tanzania ni nchi pekee duniani ambayo Helium imepetikana ardhini kwa wingi sana na ndio maana sasa iko katika nafasi ya kuongoza soko la Helium duniani".

"Hii gesi inapopatikana ardhini inakuwa na concentration ya wastani wa 2% na hivyo kufanya bei yake kuwa juu sana kwa kuchimba, na ndio maana inazalishwa viwandani. Sasa jambo moja la ajabu lilitokea. Mwaka 2015 wataalamu waligundua hii gesi Tanzania ikiwa inapatikana kwa kiwango cha juu sana, kati ya 5-15%. Hii ilifanya Tanzania kuwa nchi pekee ambayo ina Helium ardhini ambayo inaweza kuchimbwa na kuzalishwa kwa gharama ya chini kuliko inavyozalishwa na viwanda hivi 14 katika nchi 6 duniani. Na matokeo ni kwamba Tanzania ikajikuta katika nafasi ya kuongeongoza soko la Helium duniani, kama ambavyo Saudi Arabia inaongoza soko la mafuta duniani."

"Kwa sasa kuna upungufu mkubwa wa Helium. Kufuatia upungufu wa hii gesi, Marekani hata walianza kuweka hifadhi kubwa ya gesi hii kwa ajili ya matumizi ya baadae. Upungufu wa hii gesi umefanya bei yake uongezeka kwa zaidi ya asilimia 135% kwa mwaka mmoja tu!"

"Hii gesi ya Helium ni muhimu sana na itaipaisha Tanzania kiuchumi kuliko hata kama ingekuwa na mafuta. Matumizi ya hii gesi ni pamoja na kwenye mambo kama welding na hata utaalamu wa space (kwa kiingereza uses of Helium gas: are arc welding, chromatography, medical lasers, optical fiber, intercontinental ballistic missiles, space travel, etc)"

"Lakini sasa kukawa na tatizo. Ikiwa Tanzania ingeruhusiwa kuchimba hii Helium na kuuza, basi ingeuza kwa bei poa kiasi kwamba ingeua kabisa uzalishaji wa hivi viwanda 14, USA akiwa mzalishaji mkubwa. Basi inaonekana kulikuwa na makubaliano kwamba Tanzania icheleweshe uzalishaji wa Helium hadi wakati unaokubalika. Lakini kwa kufanya hivyo, lazima kulikuwa na makubaliano kwamba Tanzaia ilipwe fedha nyingi kama "compensation" ya kuzuia uzalishaji wa Helium ili kunusuru kampuni zinazouza Helium kwa sasa. Hiyo ndiyo fedha inayofanya miradi yenu ambayo wanasiasa wenu wanawaambia eti ni kodi za wananchi ili kuji-promote kisiasa. Habari ya ugunduzi wa Heluim Tanzania na umuhimu wa hii gesi katika soko la dunia, ilipaswa kuwa kubwa kuliko kama Tanzania ingegundua mafuta. Sasa jiulize, kwa nini wanasiasa wenu wamekaa kimya kuhusu huu ugunduzi mkubwa uliofanyika Tanzania? Tanzania ni nchi pekee duniani unapata Helium ardhini na utatawala soko la dunia kama ilivyo kwa Tanzanite, na mnakaa kimya, kwa nini?"

NB: Kwa wale mnaochangia mada hii bila kufikirisha sana ubongo wenu, jiulizeni jambo hili: Je implications za Tanzania kuwa nchi pekee duniani yenye Helium inayopatikana ardhini kwa wingi, ambayo inaweza kuua soko la nchi 6 pekee duniani zinazozalisha Helium kwa sasa, huku Marekani ikiwa imeshikilia zaidi ya asilimia 50% ya soko hilo, ni nini? Jiulizeni pia kwa nini serikali yetu imekaa kimya sana kuhusu huu ugunduzi wa Helium nchini ambayo itatatuweka karibu sawa kimapato na nchi zinazozalisha mafuta?

Pia tafakarini sana kile Bloomberg wamesema kuhusu ugunduzi wa Helium Tanzania, "With such extreme sensitivity in this market, a big new helium source could, just maybe, transform a whole country’s economy. A country such as, say, Tanzania".

Mwisho tafakarini sana matumizi ya Helium, kutia ndani matumizi yake katika makombora ya masafa marefu (intercontinental ballistic missiles), space travel, chromatography, medical lasers, optical fiber nk

Reference: In Photos: Massive Underground Helium Reserve Found in Tanzania
Reference: That huge helium deposit under Tanzania is even bigger than we thought
Reference: Tanzania could become top helium producer - African Business Magazine

Taarifa ya Bloomberg Businessweek juu ya Helium ya Tanzania
2019-08-28

Among the key uses for helium today are arc welding, chromatography, medical lasers, optical fiber, intercontinental ballistic missiles, and space travel. The Large Hadron Collider, the particle accelerator outside Geneva wrestling with the biggest questions of physics, needs 120 metric tons of helium a week to keep running. Helium can make things superconductive, meaning they can transmit electricity basically forever without generating any heat, and other helium properties make the element essential for semiconductor manufacturing. Every MRI machine in the world bathes its magnetic coils in liquid helium to prevent overheating.

Like the price of lithium, the price of helium is one of the more opaque among commodities, but reports said it jumped 135% from the previous year. With such extreme sensitivity in this market, a big new helium source could, just maybe, transform a whole country’s economy. A country such as, say, Tanzania.

Helium prices

Current price: $37.50 per 1000 cubic feet
View attachment 1331611
Sasa kwa Nini iwe hivyo?
 
Baadhi ya Watanzania shida

Pesa ikiingia kwa siri akauti ya serikali shida ikitumiwa kwa siri shida

Sioni tatizo hela ikiingia akaunti za serikali kwa siri sababu kutoka lazima kuwe.na official signatories na official procedures

Kuingia ziingie tu is not a big deal
 
Hizi ziliingia akaunti ipi ?

FB_IMG_1665831491154.jpg
 
Back
Top Bottom