Rais mwenye maono ya kuthubutu kama Obama tulishampata, Nyerere, whats more daring and visionary than "Azimio la Arusha"
Mbishi na mbwatukaji kama Ahmedinajad, tushampata, Benjamin William Mkapa ambaye aliwapiga vijembe kina Tony Blair kwenye CHOGM Australia 2001 na kumsifia Mugabe mpaka Blair akampoza kwa kumpa position katika team yake ya Afrika.
Asiyetishiwa na wawekezaji kama Hugo Chavez, Huyu Nyerere, aliyepiga beat kwamba kama wawekezaji hawawezi kufikisha offer ya royalties tunayoitaka tutakaa na madini yetu.
Mwenye kuzungukwa na watu wenye uwezo kama Lula - Yaani wewe hawa corrupt bunch wa Brazil ndio umewaona watu wenye uwezo?
Na mwenye mvuto kwa watu wa kawaida kama Zuma -Huyo babako JK tunaye lakini charisma yake haisaidii chochote, sanasana inatulostisha tu maana watu wanashindwa ku focus kwenye issues wanamuonea haya rais akitabasamu, Nyerere anakwambia kama unamchagua rais kwa haiba nenda kanywe naye chai.
Rais ambaye amefyatuka kidogo (au sana kutegemea na kipimo) ambaye hakupiga magoti kwa kila mtu anayejiita "mwekezaji" na tulikuwa naye, Nyerere alikuwa chizi, literary, na alisema nchi inahitaji "mwehu" ili iendelee.Lakini hata baada ya kuwa na mwehu huyu kama rais kwa miaka ishirini na kitu bado tunasota.
Kufyatuka si tija, tushakuwa na rais fyatu na hakusaidia that much kiuchumi.