Tanzania inahitaji Rais Fyatu?

hapa kijeshi jeshi tu, nashangaa hadi sasa hili jeshi letu bado halijachukua hatua wakati nchi inateketea na mafisadi
 
Tunahitaji Rais ambaye amefyatuka kidogo (au sana kutegemea na kipimo) ambaye hatopiga magoti kwa kila mtu anayejiita "mwekezaji" na ambaye hatozungukwa na wenye kuimba sifa zake.

Tunahitaji Rais ambaye amefyatuka kama Mrema!!!!!!

MKJJ,

Naomba ninukuu maneno ya Thomas Sankara (Burkina Faso 1983):

"You can not carry out fundamental change without a certain amount of madness...It comes from nonconfirmity, the courage to to turn your back to the old formulas, the courage to invent the future..."
 
Nasikia Davis Mwamunyange ni mchapa kazi saaana. Sijui kama ana sifa za UFISADI.

land+forces.JPG

Inabidi miaka yote 5 awe anavaa hayo Magwanda ya kazi na si kuvaa ki-ofisa. Kweli cha moto tutakiona ila walau nchi inaweza kwenda kama nchi. Halafu hapo tusikie eti owner wa Dowans hajulikani. Eti Mafisadi wana akili sana.......
 
We are lacking institutions in the sense the recognized modes with which communities and associations regulate their activities. Mind you, the institution does not refer directly to [person at all but to the form of order along which their activites are related and directed!
 
mkjj,

naomba ninukuu maneno ya thomas sinkara (burkina faso 1983):

"you can not carry out fundamental change without a certain amount of madness...it comes from nonconfirmity, the courage to to turn your back to the old formulas, the courage to invent the future..."

ameeeeeeeeeeeeeeeeeennnnnnnnnnnnnnn!!
 
nadhani iendeshwe kijeshi kwanza ili tuiipate habari yake

.....ANGALIA FAILI ZA VIONGOZI WA JUU JESHINI AMBAO WAMEDUMU KAZINI KWA ZAIDI YA MIAKA 20,kama sio wote wengi wana kadi za ccm ambazo watazichukua baada ya kustaafu.Hivyo usitegemee tofauti labda iweje sijui maana system ni ile ile.
 
Hata Obama alipokuwa Ghana hivi karibuni alisema kinachohitajika kwenye UONGOZI wa NCHI zetu hizi ni TAASISI zenye nguvu KIKATIBA na KISHERIA sio mtu/watu wenye nguvu. Tuimarishe Taasisi hizi kama BUNGE, MAHAKAMA, URAIS( sio RAIS), NGOs, vyama vya siasa,.....
 
hapa kijeshi jeshi tu, nashangaa hadi sasa hili jeshi letu bado halijachukua hatua wakati nchi inateketea na mafisadi

Mkuu nchi ipo chini ya wanjeshi so far...
Rais na mw/kiti wa chama tawala Luteni Kanali KIkwete
waziri habari... Kaptain Mkuchika
waziri ardhi.... Kaptain Chiligati
Katibu mkuu chama... Luteni Makamba
Mburudishaji Taifa... Kaptain Komba
Fisadi mkubwa Taifa ... Luteni Lowasa

hapo bado hujaanza wakuu wa mikoa na wilaya ndio utachoka kabisa kina Kanali Machibya, Simbakalia, Balele kibao
 
Wote hawa "watoro" jeshini siku nyingi! Lowasa hajawahi kuwa mwanajeshi. Ongeza Mzee Pinda kama watu wa UwT nao ni wajeshi.
 
Hata Obama alipokuwa Ghana hivi karibuni alisema kinachohitajika kwenye UONGOZI wa NCHI zetu hizi ni TAASISI zenye nguvu KIKATIBA na KISHERIA sio mtu/watu wenye nguvu. Tuimarishe Taasisi hizi kama BUNGE, MAHAKAMA, URAIS( sio RAIS), NGOs, vyama vya siasa,.....

Hata zikiwepo, bado watakuja na kuziscrew up. Wameiba BoT. Wameiba hadi JWATZ. Usalama wa Taifa uko hoi, hasa kitengo cha UCHUMI. Nchi inafisidiwa wao wamelala. Sanasana wako busy kuangalia nani anataka kuiondoa CCM. Azimio la Arusha walilivunjilia mbali....itakuwa hizo Taasisi?

Ghana walimwaga damu. Jerry Rawlings alipoingia madarakani (sina uhakika kabla au baada) kuna meli tatu kubwa zilikuwa zimeshehena kokoa kupeleka Ulaya. Zile Meli zilipotea kiajabu (kama Tanzania na Dowans, watu wanapokea pesa ila hawajulikani). Basi Mawaziri wahusika walikamatwa na bila mazungumzo mengi, WALIUAWA. Nafikiri kutoka hapo, Jerry na vijana wake (nilibahatika kukutana na mmoja) waliweka jiwe la msingi imara wa sheria. Kama akina Mkorofi na kuwateketeza wahusika wa Richmond na EPA tu ili kuweka msingi, basi watu kama TICT watakuwa wanarudisha wenyewe bandari zetu na kujisalimisha.......

Huu ndiyo UZURI na UBAYA wa Wanajeshi. Mkibahatika mtakuwa kama Ghana. Mkiwa na Nuksi, mtakuwa kama Guinea Conacry

Huyu ndiyo FFU kweli yaani Fanya Ufisadi Uone.
1671160760_873aac7d75.jpg
 
nadhani iendeshwe kijeshi kwanza ili tuiipate habari yake

Usiseme hivyo FL1,tafadhali futa kauli yako ya kusema iendeshwe kijeshi ili tuipate habari yake,hivi unafikiri nchi zinazoendeshwa kwa style hiyo watu wako wako kwenye hali gani? Unafikiri utapata hata muda wa kutoa maoni kama sasa unavyotoa? hebu fikri tu utakua na muda wa kufanya kazi maana wakati mwingine itatolewa amri ya kutotembea ovyo eitha nyakati fulani je utakuwa katika hali gani?try to think twice.
 
Sikonge,
Tukiimarisha Bunge angalau kwa kuanzia tu tunaweza kuleta mabadiliko. Angalia Bunge la Kenya lilivyo na nguvu sasa. Hata TEUZI za Kibaki zinagonga mwamba. Shida kubwa ya Wanajeshi wakisha jikita kwenye vyeo hivi vya kisiasa hawatatoka.
Sema tu Mzee wetu Sitta keshajeruhiwa na NEC ya CCM na bado anahesabu chenchi iliyobaki kwenye mkutano wa CPA Arusha.
 
Sikonge,
Tukiimarisha Bunge angalau kwa kuanzia tu tunaweza kuleta mabadiliko. Angalia Bunge la Kenya lilivyo na nguvu sasa. Hata TEUZI za Kibaki zinagonga mwamba. Shida kubwa ya Wanajeshi wakisha jikita kwenye vyeo hivi vya kisiasa hawatatoka.

WildCard,
Nalifahamu hilo. Ila nchi yetu naona ukuta haufai tena. Inakuwa bora kuuvunja na kuujenga upya. Hapo sasa lolote laweza kutokea. Ila ukweli ni mmoja kuwa nchi inahitaji sana Displine. I wish Mgeruman angelitawala hadi tunapata uhuru. Waingereza na hiki kitabia chao cha mashati meupe na tai, ni kama ka-Uarabu. Wao akili mukichwa, na sisi tunawaiga tu....
 
Hata zikiwepo, bado watakuja na kuziscrew up. Wameiba BoT. Wameiba hadi JWATZ. Usalama wa Taifa uko hoi, hasa kitengo cha UCHUMI. Nchi inafisidiwa wao wamelala. Sanasana wako busy kuangalia nani anataka kuiondoa CCM. Azimio la Arusha walilivunjilia mbali....itakuwa hizo Taasisi?

Sikonge,

Hao wako hoi baada ya kuvimbiwa vibaya! Hakuna tofauti kati ya UWT na Government hapa. Hao UWT wakiona issue unafikiri wanatakiwa kuiripoti wapi?Serikalini kwa JK or kwa MKPP or wapi? unafikir wanapenda kutwanga maji kwenye kinu? nao ni binadamu kama sisi, they got needs vile vile....so nao wanajoin the battle kuwakandamiza wanyonge na kutii kiu ya mabwana na yao pia!

Tena FYI, hivi vijamaa ukikutana navyo huku uswaz vinasumbua sana, vikinywa bia eti vinatoa EUROs au Pound.....! wapi na wapi?
 
Wakuu tuache kufikiria tawala za kijeshi.Mimi nadhani tupate raia mmoja tu mzalendo mwenye vision na uchungu wa kweli na maendeleo ya nchi hii.Hawa watu wapo isipokuwa bado hawajapewa nafasi au wanabaniwa au wanavurugwa na system isiyoitakia mema nchi.
Embu tuchukulie mfano tumpe urais Pombe Magufuli leo hii,hivi hatutaweza kusonga kweli?
 
Usiseme hivyo FL1,tafadhali futa kauli yako ya kusema iendeshwe kijeshi ili tuipate habari yake,hivi unafikiri nchi zinazoendeshwa kwa style hiyo watu wako wako kwenye hali gani? Unafikiri utapata hata muda wa kutoa maoni kama sasa unavyotoa? hebu fikri tu utakua na muda wa kufanya kazi maana wakati mwingine itatolewa amri ya kutotembea ovyo eitha nyakati fulani je utakuwa katika hali gani?try to think twice.

Acha woga na wewe bana! Rights are never given, they are fought for!
 
Back
Top Bottom