Inasikitisha. Kama wanalipwa bila kazi nayo inazidi kusikitisha. Ila inabidi wakae mkao wa kula na wao maana huwa wakifukuzwa kazi, kazi pekee ni kufungua biashara zake au kufungua Mpelelezi wa kujitegemea ambayo kwa Tz bado ngumu. Hiyo kazi huwa inaisha vibaya kama hukujiandaa mapema. Na kwa hali ilivyo, kama akija kichaa basi hao jama wote watapanguliwa na kuanza upya maana huwezi anza na watu ambao wameshanogewa na visenti vya CCM. Ila ubaya mmoja ni kuwa, wale wenye moyo na ari ya kuifanyia kazi nchi yao, ndiyo wanakuwa frustrated. Unakusanya habari nzuri kuliokoa taifa, ukiipeleka kwa boss unapigwa warning USIRUDIE kuipeleleza hiyo scandal maana ni ya Kigogo fulani.....