Kama kumbukumbu zangu ziko sawa. Wakati wa Magufuli ulikuwa supporter wake. Nashangaa now ni kama umemgeuka
Itakuwa kumbukumbu zako haziko sawa.
Hayati rais Magufuli alifanya baadhi ya mambo ambayo najivunia mpaka kesho kwayo. Nimehojiwa na baadhi ya Taasisi za kimataifa kuhusu Tanzania's approach on COVID-19 na mahojiano hayo yamerikodiwa (reference zipo), katika mahojiano hayo nimejivunia kuwa naongozwa na rais Magufuli. Namna serikali yake ilivyoliendea suala la COVID basi kwangu alistahili na anastahili pongezi za hali ya juu. Sitokutajia hayo mahojiano kwa sababu za privacy.
Ila pia hayati rais Magufuli alifanya mambo ya ajabu sana ambayo hakuna mtu au Mtanzania mwenye akili timamu, mpambanuzi na mwenye uelewa wa mambo atayakubali. Bahati mbaya mambo hayo mabaya yalikuwa mengi kuliko mema aliyoyafanya. Na hata hayo mema ukiyaangalia kwa undani basi kuna ukakasi wa hali ya juu.
Mfano, ununuzi wa ndege za Atcl kwa cash na bila kupitia bungeni lilikuwa ni suala linamlomtia doa sana.
Ujenzi wa airport ya chato lilikuwa ni suala baya sana ambalo kiongozi mwenye busara hakutakiwa hata kulifikiria.
Namna ya suala la korosho mwaka 2018 liligubikwa na ghiliba na sintofahamu nyingi sana.
Jaribio la mauaji ya Tundu Lissu akiwa kama kiongozi bungeni, na namna ambavyo serikali ililiendea suala lile ilikuwa haikubaliki.
Kupotea/kutekwa kwa baadhi ya watu prominent ambapo hali hiyo ilikuwa ina public interests na serikali yake kutofanikiwa kutoa majibu mazuri kwa wananchi ilionyesha udhaifu mkubwa sana. Mfano Mohamed Dewji.
Suala la wateule wake kufanya mambo kinyume na muongozo wa viongozi wa Umma halafu yeye kuamua kunyamaza iliichafua picha yake.
All in all, mimi sikuwa supporter wake kama unavyosema lakini alikuwa rais wangu niliyemheshimu. Nilimpongeza alipopatia na alipostahili pongezi na kumkosoa na kumshauri alipokosea.
Usinichukie mkuu!