Tanzania inahitaji Rais Fyatu?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,474
39,987
Tunahitaji Rais mwenye maono ya kuthubutu kama Obama, mbishi na mbwatukaji kama Ahmedinajad, asiyetishiwa na wawekezaji kama Hugo Chavez, mwenye kuzungukwa na watu wenye uwezo kama Lula na mwenye mvuto kwa watu wa kawaida kama Zuma. Tunahitaji Rais ambaye amefyatuka kidogo (au sana kutegemea na kipimo) ambaye hatopiga magoti kwa kila mtu anayejiita "mwekezaji" na ambaye hatozungukwa na wenye kuimba sifa zake.

Tunahitaji Rais ambaye amefyatuka kama Mrema!
 
Mimi napendekeza Mtikila awe rais. Waziri mkuu awe Lyatonga Mrema, Makamu wa Rais awe Magufuli. Halafu tumwombe Mungu amfufue Sokoine awe waziri wa mambo ya ndani. Serikali hiyo iwe ya miezi sita tu. Labda nchi yetu takatifu itapata habari yake.
 
Mi napendekeza Mtikila awe rais,. Waziri mkuu awe Lyatonga Mrema, Makamu wa Rais awe Magufuli. Afu tumwombe Mungu amfufue Sokoine awe waziri wa mambo ya ndani. Serikali hiyo iwe ya miezi sita tu. Labda nchi yetu takatifu itapata habari yake.

homeboy,
ai mini SHEMEJI,unatafuta nin kwenye jukwaa la wazee?
 
Tunahitaji Rais mwenye maono ya kuthubutu kama Obama, mbishi na mbwatukaji kama Ahmedinajad, asiyetishiwa na wawekezaji kama Hugo Chavez, mwenye kuzungukwa na watu wenye uwezo kama Lula na mwenye mvuto kwa watu wa kawaida kama Zuma. Tunahitaji Rais ambaye amefyatuka kidogo (au sana kutegemea na kipimo) ambaye hatopiga magoti kwa kila mtu anayejiita "mwekezaji" na ambaye hatozungukwa na wenye kuimba sifa zake.

Tunahitaji Rais ambaye amefyatuka kama Mrema!!!!!!

Halelujah, finally someone is showing love to Mrema!
Hapa kijeshijeshi ndio tutafika!
 
Kwa matatizo tuliyonayo sasa hivi, kama kweli tunataka kufika salama tunakokwenda, kiongozi ni lazima awe na kichwa cha mwendawazimu. Hata China,USSR na leo hii Russia chini ya Putin, zilijengwa na watu ambao vichwa vyao vilikuwa vimefyatuka. Na mfano mwingine hauko mbali...ni hapa jirani Rwanda. Kagame hataki kujipendekeza kwa mtu
 
mi napendekeza mtikila awe rais,. Waziri mkuu awe lyatonga mrema, makamu wa rais awe magufuli. Afu tumwombe mungu amfufue sokoine awe waziri wa mambo ya ndani. Serikali hiyo iwe ya miezi sita tu. Labda nchi yetu takatifu itapata habari
chrispin naona unaota ndoto za alinacha
 
Ni kweli tunahitaji Raisi imara anayejiamini na kufuatilia kwa makini mipango ya maendeleo. KWELI tunahitaji mbwatukaji, wakuthubutu, asiyemwoga, na zaidi anayezungukwa na watu wanaojiamini na sio kujipendekezaaaaaa....

Tuna safari ndefuuu lakini njia ya mabadilikoo ipo
Tujengee uthubutuu katika jamii yetu, nasikitika wasomii ndio wanaongoza kundi la wasiojiamini na wanafikii katika masulaa muhimu ya maendeleoo ya Taifa
 
Wanajeshi jamani waogopeni, sina imani nao hata kidogo. Ndio maana jeshini nidhamu ni kitu cha kwanza!
Na tunachokosa kwenye UONGOZI wa NCHI yetu kwa sasa ni NIDHAMU katika kila kitu.

Hatuna nidhamu kwenye MAADILI na MIIKO ya UONGOZI; hatuna nidhamu katika matumizi ya MALIASILI na RASILMALI za NCHI hii; hatuna nidhamu katika kuheshimu KATIBA na SHERIA za NCHI......
 
rais fyatu huyu awe na ujasiri wa kutimua na kupitia upya mikataba ya wawekezaji wanaoneemesha makwao kwa kutumia rasilimali zetu na kutuacha hohe hahe! asile meza moja na mafisadi, ambaye yuko tayari na uwezo wa kujiuliza ni kwa nini pamoja na utajiri wote tuliobarikiwa na mungu bado tumeendelea kuwa masikini, mwenye utayari wa kutoa upofu huu uliotugubika...................nani sasa?! ..........labda mm
 
tunahitaji rais mwenye maono ya kuthubutu kama obama, mbishi na mbwatukaji kama ahmedinajad, asiyetishiwa na wawekezaji kama hugo chavez, mwenye kuzungukwa na watu wenye uwezo kama lula na mwenye mvuto kwa watu wa kawaida kama zuma. Tunahitaji rais ambaye amefyatuka kidogo (au sana kutegemea na kipimo) ambaye hatopiga magoti kwa kila mtu anayejiita "mwekezaji" na ambaye hatozungukwa na wenye kuimba sifa zake.

Tunahitaji rais ambaye amefyatuka kama mrema!!!!!!

jeshi lishike nchi kwa miaka 5! Ule wa kwanza tu nchi imeshanyooka!
 
Back
Top Bottom