Titho Philemon
Member
- Nov 15, 2019
- 35
- 113
Tanzania kama taifa licha ya ukongwe wake toka tupate uhuru ni dhahiri kwamba mifumo ya utawala imekuwa ikibidi kuwa mibovu kila kukicha. Hii hali imekuwa ikichangiwa sana sana na uchu wa viongozi waliowahi kushika nyadhifa kubwa serikalini kutaka uzao wao urithi nafasi na kufuata nyayo zao katika madaraka.
CHADEMA kama chama kikuu cha upinzani hapa nchini, kimekuwa kikipata uungwaji mkono kutoka kwa wanyonge wengi na wazalendo wa taifa kutokana na hoja pamoja na dhamira yao ya kuhakikisha na kuhimiza umoja wa kitaifa, utawala wa sheria, udumishaji wa demokrasia pamoja na uwazi na uwajibikaji kwa viongozi wa umma.
Serikali kupitia CCM imetengeneza taswira mpya, mbaya tena ya kijima kwakuamini kwamba kila wazo linalokinzana na matakwa ya kiongozi wa CCM kwamba ni la kipinzani. Wanaenda mbali zaidi na kuzidi kutumia kamati za maadili kuwanyamanzisha wale wana CCM wanaoonekana vichomi katika kuibua madhaifu yaliyomo ndani ya chama chao.
Vifuatavyo ni vitu ambavyo serikali ya CCM imevifanya na hatimaye kuondoa radha yake masikioni mwa wananchi:-
1. Utelekezwaji wa washtakiwa Ripoti ya CAG.
Kupitia hili wananchi wanasikia hela zimepotelea kwenye sekta fulani lakini walengwa hawachukuliwi hatua. Hii hali siyo tu inawaumiza wananchi, lakini pia inawapa nguvu wapinzani na kuondoa matumaini ya Chama tawala kwenye maskio ya watanzania.
2. Matumizi ya anasa ya fedha za umma.
Chini ya utawala wa CCM kumekuwa na kunashuhudiwa upotevu mkubwa wa pesa ya umma kwa matumizi yasiyo na umuhimu wowote (anasa) kwa wananchi. Unakuta ziara zinakuwa nyingi tena za viongozi wa vyama ndani ya nchi majukumu ambayo wangetekeleza MA DC, DED, RC na mawaziri unakuta hela ya serikali na magari vinatumiwa unnecessary kutimiza ziara za kichama.
Pamoja na mengine mengi, CHADEMA ikishika dola chini ya mfumo wao pendwa wa majimbo, serikali itabadirika na tena maswala ya kufitiniana sisi kwa sisi wakati wote ni watanzania hayatokuwepo.
TANZANIA BILA CCM INAWEZEKANA!!!