Tanzania huenda ikatuchukua karne nzima kumpata Rais Samia mwingine

Ni lini baada ya huyu tutampata samia mwingine, Rais aliyeshindwa kukusanya kodi halali na kukimbilia kutengeneza tozo za ajabu ajabu?

Ni lini baada ya huyu tutampata samia mwingine, Rais mpiga dili na mabeberu ambaye ameamua kuua mradi wa bwawa la nyerere?

Ni lini baada ya huyu tutampata samia mwingine, Rais ambaye ndani ya miezi mitatu ya uongozi wake kumekuwa na mgao wa maji na umeme nchi nzima?

Ni lini baada ya huyu tutampata samia mwingine, Rais asiyeweza kuongoza serikali zaidi ya kudemka na kujilegeza (macho kurembua).
Uongo mtupu huu,ulioandika.Andika ukweli.Wananchi tunafurahi kuwa na Rais Samia,Raha sana.
 
Namkubali huyu rais lakini hizi pambio zenu zitamharibu.
Nyie waimba pambio tafadharini sana msije mkamharibu rais. Pambio zenu ziwe na kias.

Unasema karne utadhani wewe ni Mungu!
 
Umesahau,

Uhuru wa mahakama,
Demokrasia,
Uhuru wa kujieleza
Uhusiano kimataifa,
Ujenzi wa LNG
Ujenzi wa bandari ya Bagamoyo
Ujenzi wa SGR
ujenzi wa SG
Ataongeza ndege zingine 4,bila kuweka hili team ile bila kuona ndege huwa hawaridhiki.
 
Huo utaratibu wa kuongoza kwa vipindi viwili vya miaka mitano mitano usitiswe tu, anayeshinda uchaguzi atawale kwa miaka mitano tu, tuchague Rais mwingine.
Miaka kumi inatengeneza miungu watu wanaojiona kuwa watanzania zaidi kuliko Tanzania yenyewe.
 
Kama Taifa hebu tutafakari haya:

1. Ni lini tena baada ya huyu tutampata Samia mwingine atakayeongeza kwa mkupuo wanafunzi wapya elfu 29 kwenye HESLB simnakumbuka mtangulizi wake yeye ilimchukua miaka mitano kufikisha wanafunzi wapya 32.

2. Ni lini tena baada ya huyu tutampata Samia mwingine atakayekusanya kodi kwa wastani wa TZS 17.2 Trilioni kwa mwezi bila ya kukimbiza wafanyabiashara wala kuwadhulumu chochote.

3. Ni lini tena baada ya huyu tutampata Samia mwingine anayewahurumia na kuwarejesha shuleni watoto wa masikini waliopata mimba wakiwa shuleni kwa kurubuniwa kwa chips na bodaboda.

4. Ni lini tena baada ya huyu tutampata Samia mwingine atakayekuza uwekezaji wa nje FDIs mara sita zaidi kwa miezi sita tu yaani kutoka $510M hadi $3BL.

5. Ni lini tena baada ya huyu tutampata Samia mwingine kwa miezi saba tu ataongeza hifadhi yetu ya fedha za kigeni kwa TZS 4.4Trilion yaani kutoka $4.8BL mwezi March hadi $6.7BL mwezi September 2021.

6. Ni lini tena baada ya huyu tutampata Samia mwingine atakayenunua ambulance 395 na magari 214 kwaajili ya chanjo wakati mtangulizi wake kwa miaka mitano alinunua ambulance 117 tu bila magari ya chanjo.

7. Ni lini tena baada ya huyu tutampata Samia mwingine atakayenunua CT SCAN kila mkoa mtakumbuka tangu uhuru zilikuwepo CT SCAN mbili tu bara na visiwani.

8. Ni lini tena baada ya huyu tutampata Samia mwingine atakayetununulia MRI kwenye kila hospitali ya kanda nchi nzima sina historia kama tulikuwa na MRI yeyote kabla ya hizi mpya za mama Samia.

9. Ni lini tena baada ya huyu tutampata Samia mwingine atakaye nunua "Water drilling holes machines " 25 toka mashine moja ya Halmashauri ya Tarime tuliyokuwa nayo,Rais anakwenda kumaliza shida ya maji kwa vitendo.

10. Ni lini tena baada ya huyu tutampata Samia mwingine atakayetujengea madarasa elfu 15 ya sekondari na mengine elfu 3 ya shule shikizi, Sawa na wastani wa kila shule moja ya sekondari ya serikali madarasa mapya manne (4).

11. Ni lini tena baada ya huyu tutampata Samia mwingine atakayewapanga wamachinga wetu kwenye Permanent Premises ili watambulike na kupewa mikopo na huduma zingine za kibiashara kama Semina na mafunzo kirahisi badala ya kuwatumia kama mtaji wa kisiasa na kuwaacha wakiogelea kwenye umasikini mwaka wa Uchaguzi hata mwaka wa Uchaguzi.

12. Ni lini tena baada ya huyu tutampata Samia mwingine atakayefuta wasiojulikana na walevi wa madaraka na kuwafanya watu waishi kwa Uhuru na kujiamini ndani ya nchi yao na kulifungua Taifa kimataifa.

Nitaendelea na tafakuri yangu

Hata mwenda kuzimu mulimpa sifa hadi mka fika mahali mkamfananisha na Mungu.
Leo mnaona madudu aliyo fanya. Hata shetani haya fanyi kwa wanadamu. Samia nae naona mnaelekea huko huko. Maisha yamekuwa magumu bado mna mpa sifa za kijinga. Ifike mahali muamke. Acheni usifia ujinga
 
Hata mwenda kuzimu mulimpa sifa hadi mka fika mahali mkamfananisha na Mungu.
Leo mnaona madudu aliyo fanya. Hata shetani haya fanyi kwa wanadamu. Samia nae naona mnaelekea huko huko. Maisha yamekuwa magumu bado mna mpa sifa za kijinga. Ifike mahali muamke. Acheni usifia ujinga
Chadema mnapenda mjazwe pesa mifukoni,ndilo tatizo lenu.
 
Si Bora ya magufuli, tulikuwa na umeme, maji, vifaa vya ujenzi kwa Bei Chee, mfumuko wa Bei ulikuwa hakuna, sasa HUYU SSH dah tunalia sisi wafanyabiashara mzunguko wa pesa hakuna, mauzo hakuna, umeme wa mgao, maji ya mgao, vifaa vya ujenzi Bei juuuuu.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Mfuate Kuzimu huyo Dikteta ambaye unaamini umeme ulikuwa haukatiki na bei hazikupanda
 
Ilitoka takwimu kwenye kila watanzania 5 mmoja ni kichaa..

Na pia nimeamini illiteracy rate bado ni ya kiwango cha juu Tanzania
 
UPUMBAVU MTUPU
UPUMBAVU MTUPU
UPUMBAVU MTUPU
UPUMBAVU MTUPU
UPUMBAVU MTUPU.
Kwa taarifa yako, hata watoto wadogo wanajua kuwa, Rais wa pekee kabisa Tanzania na Afrika alikuwa ni MAGUFULI tu.Huyu ndo Rais anayeishi mioyoni mwa Watanzania.
Alisacrifice maisha yake kwa ajili ya sisi Watanzania Wanyonge.
Nyekundu itakuwa Nyekundu tu na Nyeupe itakuwa Nyeupe tu.
Hakuna mtu anayeweza kubadili hilo.
CHAPA ya kitu ikishapigwa mioyoni mwa watu ni nani anayeweza kuifuta. Hakuna kabisa.
 
UPUMBAVU MTUPU
UPUMBAVU MTUPU
UPUMBAVU MTUPU
UPUMBAVU MTUPU
UPUMBAVU MTUPU.
Kwa taarifa yako, hata watoto wadogo wanajua kuwa, Rais wa pekee kabisa Tanzania na Afrika alikuwa ni MAGUFULI tu.Huyu ndo Rais anayeishi mioyoni mwa Watanzania.
Alisacrifice maisha yake kwa ajili ya sisi Watanzania Wanyonge.
Nyekundu itakuwa Nyekundu tu na Nyeupe itakuwa Nyeupe tu.
Hakuna mtu anayeweza kubadili hilo.
CHAPA ya kitu ikishapigwa mioyoni mwa watu ni nani anayeweza kuifuta. Hakuna kabisa.
Kwa Watanzania wasukuma sawa anaishi kwenye mioyo yenu. Kweli kuna Watanzania wapumbavu. Dubwasha tumelizika Chato tarehe 27/ 03/ 21 na sasa hivi ni chakula cha minyoo tu bado unadai anaishi kwenye mioyo yenu. Misukule wahaedi
 
UPUMBAVU MTUPU
UPUMBAVU MTUPU
UPUMBAVU MTUPU
UPUMBAVU MTUPU
UPUMBAVU MTUPU.
Kwa taarifa yako, hata watoto wadogo wanajua kuwa, Rais wa pekee kabisa Tanzania na Afrika alikuwa ni MAGUFULI tu.Huyu ndo Rais anayeishi mioyoni mwa Watanzania.
Alisacrifice maisha yake kwa ajili ya sisi Watanzania Wanyonge.
Nyekundu itakuwa Nyekundu tu na Nyeupe itakuwa Nyeupe tu.
Hakuna mtu anayeweza kubadili hilo.
CHAPA ya kitu ikishapigwa mioyoni mwa watu ni nani anayeweza kuifuta. Hakuna kabisa.
Wacha kupotosha watu. Magufuli alikuwa anaharibu Nchi kwa vitendo vyake VIOVU. Laiti angekuwa mtetezi wa wanyonge asingeiba kura za Serikali za Mitaa zote za 2019 na za uchaguzi Mkuu wa 2020.

Mungu alijuwa na ALIKASIRISHWA na UFEDHULI wake ndiyo akaamua kuikomboa Tanzania kutoka kwa Shetani Dikteta na kuipeleka roho yake jehanam baada ya siku 114 toka aibe uchaguzi wote wa Oktoba 2020.
 
Kuna maswali najiuliza mbona kama wanasiasa wa tanzania baraz Wana uwezo mkubwa sana katka comedy kuliko hata politics Kuna haja yakua halalisha kua politics in tz is directly proportional to comedy

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom