Tanzania huenda ikatuchukua karne nzima kumpata Rais Samia mwingine

UPUMBAVU MTUPU
UPUMBAVU MTUPU
UPUMBAVU MTUPU
UPUMBAVU MTUPU
UPUMBAVU MTUPU.
Kwa taarifa yako, hata watoto wadogo wanajua kuwa, Rais wa pekee kabisa Tanzania na Afrika alikuwa ni MAGUFULI tu.Huyu ndo Rais anayeishi mioyoni mwa Watanzania.
Alisacrifice maisha yake kwa ajili ya sisi Watanzania Wanyonge.
Nyekundu itakuwa Nyekundu tu na Nyeupe itakuwa Nyeupe tu.
Hakuna mtu anayeweza kubadili hilo.
CHAPA ya kitu ikishapigwa mioyoni mwa watu ni nani anayeweza kuifuta. Hakuna kabisa.
Ni kweli kabisa ni wa kipekee maana alisimama na misimamo take kuhusu korona weee hatimaye.....!( This is a scientific issue) lazima kama msomi ukubaliane na scie activities)
 
Naona wapambe wa chief Hangaya mnapiga propaganda mfu. Ni hivi, mama wa kambo si mama.
Umesahau,

Uhuru wa mahakama,
Demokrasia,
Uhuru wa kujieleza
Uhusiano kimataifa,
Ujenzi wa LNG
Ujenzi wa bandari ya Bagamoyo
Ujenzi wa SGR
ujenzi wa SG
 
Hawa chawa wasiokuwa na staha yoyote sijui wanaokotwa wapi.

Huyo Rais Samia aliyekuwepo kachukuliwa na nani; au na yeye kamfuata mtangulizi wake?

Hivi kweli watu kama huyu mleta mada hapa nao wanahesabika huko wanakotoka kwamba wapo mapambanoni kumpamba anayewalisha?

Unaleta mada kama hii hapa, unataka watu wajadili nini?

Niseme tu, ninakujibu hivi hapa kufuatana na kichwa cha mada yako. Kama kuna mambo umeyaandika huko chini siyajui mimi. Kwa kawaida huwa sisomi mada za kipuuzi kama ijionyeshavyo kwenye kichwa cha habari.
 
Ni lini baada ya huyu tutampata samia mwingine, Rais aliyeshindwa kukusanya kodi halali na kukimbilia kutengeneza tozo za ajabu ajabu?

Ni lini baada ya huyu tutampata samia mwingine, Rais mpiga dili na mabeberu ambaye ameamua kuua mradi wa bwawa la nyerere?

Ni lini baada ya huyu tutampata samia mwingine, Rais ambaye ndani ya miezi mitatu ya uongozi wake kumekuwa na mgao wa maji na umeme nchi nzima?

Ni lini baada ya huyu tutampata samia mwingine, Rais asiyeweza kuongoza serikali zaidi ya kudemka na kujilegeza (macho kurembua).
Ni lini tutampata Samia mwingine anayezurura kila kukicha na ndege juu mawinguni akituacha wananchi wake ardhini?

Ni lini tutampata Samia mwingine ambaye amejitahidi kuongeza mfumuko wa Bei hata kwa vitu visivyo luxury Kama Rim Paper,Mafuta ya kupika na Petrol


Huyu mama alianza vizuri sana hata siye tulomchukia Mwendazake na kikosi chake tulimpenda Mama lakini mama kama anaanza kugonga miti
 
Heshima ni kitu cha BURE jifunze kuandika Kwa staha
Kwani harembui? We huoni mijicho yake ile ilivyolegezwa?

Amiri jeshi gani anarembua? Anaaibisha nchi.

Amiri jeshi gani hawezi hata kufoka japo kidogo atie mikwara ya kutisha wazembe?

Au ndo mambo ya kizenji? Ulegevu na kurendemka?
 
Ni lini tutampata Samia mwingine anayezurura kila kukicha na ndege juu mawinguni akituacha wananchi wake ardhini?

Ni lini tutampata Samia mwingine ambaye amejitahidi kuongeza mfumuko wa Bei hata kwa vitu visivyo luxury Kama Rim Paper,Mafuta ya kupika na Petrol


Huyu mama alianza vizuri sana hata siye tulomchukia Mwendazake na kikosi chake tulimpenda Mama lakini mama kama anaanza kugonga miti
HAKUNA KAMA #SSH,INCHI ILIHARIBIKA HII NDG,KWA MAMBO 75%FICTIONS, AND ILLUSIONS,KWA SASA INAKAA KWENYE MSTARI TARATIBU UNDER HIGH SUPERVISION MDA SIO MREFU WATANZANIA TUTAFURAHI SANA.
 
Kama Taifa hebu tutafakari haya:

1. Ni lini tena baada ya huyu tutampata Samia mwingine atakayeongeza kwa mkupuo wanafunzi wapya elfu 29 kwenye HESLB simnakumbuka mtangulizi wake yeye ilimchukua miaka mitano kufikisha wanafunzi wapya 32.

2. Ni lini tena baada ya huyu tutampata Samia mwingine atakayekusanya kodi kwa wastani wa TZS 17.2 Trilioni kwa mwezi bila ya kukimbiza wafanyabiashara wala kuwadhulumu chochote.

3. Ni lini tena baada ya huyu tutampata Samia mwingine anayewahurumia na kuwarejesha shuleni watoto wa masikini waliopata mimba wakiwa shuleni kwa kurubuniwa kwa chips na bodaboda.

4. Ni lini tena baada ya huyu tutampata Samia mwingine atakayekuza uwekezaji wa nje FDIs mara sita zaidi kwa miezi sita tu yaani kutoka $510M hadi $3BL.

5. Ni lini tena baada ya huyu tutampata Samia mwingine kwa miezi saba tu ataongeza hifadhi yetu ya fedha za kigeni kwa TZS 4.4Trilion yaani kutoka $4.8BL mwezi March hadi $6.7BL mwezi September 2021.

6. Ni lini tena baada ya huyu tutampata Samia mwingine atakayenunua ambulance 395 na magari 214 kwaajili ya chanjo wakati mtangulizi wake kwa miaka mitano alinunua ambulance 117 tu bila magari ya chanjo.

7. Ni lini tena baada ya huyu tutampata Samia mwingine atakayenunua CT SCAN kila mkoa mtakumbuka tangu uhuru zilikuwepo CT SCAN mbili tu bara na visiwani.

8. Ni lini tena baada ya huyu tutampata Samia mwingine atakayetununulia MRI kwenye kila hospitali ya kanda nchi nzima sina historia kama tulikuwa na MRI yeyote kabla ya hizi mpya za mama Samia.

9. Ni lini tena baada ya huyu tutampata Samia mwingine atakaye nunua "Water drilling holes machines " 25 toka mashine moja ya Halmashauri ya Tarime tuliyokuwa nayo,Rais anakwenda kumaliza shida ya maji kwa vitendo.

10. Ni lini tena baada ya huyu tutampata Samia mwingine atakayetujengea madarasa elfu 15 ya sekondari na mengine elfu 3 ya shule shikizi, Sawa na wastani wa kila shule moja ya sekondari ya serikali madarasa mapya manne (4).

11. Ni lini tena baada ya huyu tutampata Samia mwingine atakayewapanga wamachinga wetu kwenye Permanent Premises ili watambulike na kupewa mikopo na huduma zingine za kibiashara kama Semina na mafunzo kirahisi badala ya kuwatumia kama mtaji wa kisiasa na kuwaacha wakiogelea kwenye umasikini mwaka wa Uchaguzi hata mwaka wa Uchaguzi.

12. Ni lini tena baada ya huyu tutampata Samia mwingine atakayefuta wasiojulikana na walevi wa madaraka na kuwafanya watu waishi kwa Uhuru na kujiamini ndani ya nchi yao na kulifungua Taifa kimataifa.

Nitaendelea na tafakuri yangu

Mungu wewe upo uliko unajuwa siri nzito sana.
 
Kiukweli Tanzania iko salama mikononi mwa Rais SSH hasahasa;
1. Hakuna kikundi cha wasiojulikana kilichokuwa kinateka na kuua

2. Hakuna matusi kwenye majukwaa kama yule dikteta alivyokuwa anasema "Baki na mavi yako"

3. Hakuna task force ya TRA iliyokuwa inanyang'anya wafanyabiashara fedha zao

4. Hakuna TAKUKURU iliyokuwa inabambikiza watu makesi ya uwongo

5. Hakuna matumizi mabaya ya fedha za Serikali kama kujenga Airport Kijijini Chato

6. Hakuna matakwimu ya uwongo kama vile kukua kwa uchumi by 7.8% wakati ukweli ni 4.2%

7. Hakuna uwongo wa kusema tunajenga kwa fedha zetu wakati tunakopa kwenye mabenki ya kimataifa
CHADEMA wanalia sana aise
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom