50thebe
JF-Expert Member
- Mar 10, 2011
- 4,139
- 4,119
Nchi yetu Tanzania timeshuhudia vipindi vya marais wengi.Ila kwa uelewa na ufuatiliaji wangu,tunaweza kukaa muda mrefu sana tusipoangalia katika kupata rais kama huyu JK wa pili hapa nchini.
Japo anabezwa,anakashifiwa na kuitwa dhaifu lakini ukweli utabaki palepale Kikwete ni rais bora kuliko wote tuliopata kuwashuhudia.
Siku atakayokaa pembeni tutamkumbuka.
Nadhani inafaa tumtambue kama rais wa karne ktk nch yetu.
Of course amekuwa ni raisi aliyesafiri kwenda ng'ambo mara nyingi kuliko maraisi wote waliomtangulia. Kuvunja hii record itakuwa ngumu kwa raisi ajaye.
Bila ubishi, tumeona ari mpya, nguvu mpya na kasi mpya zilivyobadilika kuwa ari zaid, nguvu zaidi na kasi zaidi. Hizi mbiu ziliekezwa kwenye nini? Hiki ndicho kinakazia kwa nini hatutapa Raisi Makini kama Mh Dr Prof Kikwete.