Tanzania haitopata rais kama Kikwete

Tanzania haitopata rais kama Kikwete

Ni kweli hatutapata kama JK na mie naomba tusimpate kama yeye kwa kuwa ndiyo uongozi pekee ambao wameongoza kwa kutorosha pesa kupeleka nje ya nchi na kuficha. Na ndiye rais aliye ahidi kurekebisha mikataba yote ya madini na hatujaona chochote. Na mengine mengi tu " kumbukeni wenyewe sina haja ya kuwakumbusha.
 
Ni kweli tena sana, kwani Tanzania ikimpata Rais mdhaifu, (m.w.i.z.i akiwashirikisha familia nzima), na msanii kama tulikuwa naye hadi sasa, ni maumivu hadi lini, ebu tema mate chini ili Mungu atuepushe na balaa hilo.


ni bora ateme mate chini japoa hata akitema juu lazima yarudi chini
 
Na uhakika hatatokea tena kwa sababu watanzania wameanza kupata elimu na hawatafanya kosa la kuangalia sura kumchagua rais!
 
Alhamdulillah nimeishi awamu zote,, Kikwete alochofanya ni kusahihisha ya awamu zote na kukubali kubebla lawama. Kama kikwete asingefungua democrasia ya kweli mengi tusingeyajua, Kikwete kwa dhati yake ameruhus watu kusema hata kama katika kusema huko kutamgharimu, haya maovu yanayosemwa leo kuhusu Rushwa ni kwa vile JK karuhusu watu kujadili na kusema waziwazi kinachomponza JK ni kutoa kwa uhuru wa kujieleza. Watu sasa wanaweza sema chochote, labda wanetu hawajui hili, Enzi za mwalimu kwa style hii ya kumtusi JK wengi wangekua Lupango wazee wenzangu watakubaliana nami tu ( sisemi kwa ubaya ) Mwinyi nae alipata dhila kama hii, Enzi za Mzee mkapa wasingeweza sema wayasemayo leo, CUF wanakumbuka kule Pemba nini kilitokea, na hapa Dar !!! Enzi za mwalimu hali kwa wananchi ilikua mbaya sana , kulikua hakuna barabara kabisa wa sumbawanga, kigoma, mtwara mashahidi, barabara zilikua Arusha na Kiliumajaro ,, leo waweza toka mtwara mpka kigali bila kukanyaga vumbi.. ni mengi sana siwezi orodhosha sema tu akuchukuiae hata ukimfanyia vipi bado atakuchukukia ,, ila tujiulize wanaomchukia JK hawayaoni haya ?au kuna agenda iliyojificha?

Tofautisha enzi zile marais wa awamu ya kwanza walikuwa ni zaidi wa wafalme maana watu walikuwa gizani na marais wa awamu zile walijigawia mali maana hazikuwa accountable sababu rais ndo alikuwa mahakama na ni bunge utakuta marais wa awamu zile kama Kenyatta, Banda, Mobutu, Habyarimana, Nguema, nk walijirundikia mali na kuua wapinzani wao lakini bado Nyerere hakuwahi kujilimbikizia mali wala kuua mwanasiasa ulipopingana naye alifungua mipaka uondoke kama Kambona na wafusi wake alipondoka akaachia madaraka akiwa hana kitu na hakuna hata mtoto akiwa anamiliki gari na katawala kwa miaka 24 jangili Kikwete kaingia madarakani Ridhwani bilionea ana miliki malori, vituo vya mafuta, mpiga madeal na mashamba mahekta kule Kilombero wakati baba yake katawala miaka 9 tu familia yake imetajirika ghafla na yeye mwenyewe bilionea mali zimeibiwa za wananchi hadharani mfano 2005 kulikuwa na tembo Tanzania 165,000 kwa sasa ni 55,000 tu JK akishirikiana na majangili.wenzake akina Kinana kafyeka mali za nchi

Jimmy Carter rais wa Marekani alipohojiwa baada ya kifo cha Nyerere mwaka 1999 alisema "For us in the west we didn't see Julius Nyerere only as a leader but also as a saint compared to his African counterparts"

Nyerere usilinganishe na huyo aliyefaa kuwa mkuu wa wilaya ya Misungwi akatumia matajiri kununua urais na sasa nchi imeyumba wala haheshimiki kama presidaa anaonelana ze comedy
 
Kwa upande wa elimu akuna kitu namatokeo ya elimu hii inayotolewa tanzania mtaiona baadaye watoto wetu watakapokataliwa kwenye nchi za jirani na wawekezaji hizo divion five za kawambwa,ukienda tu kwenye mabenk hapa kwetu wanaangalia hesabu o level na a level una c or d,bado awajapima gpa,sawa amefanya ya.kwake,lakini Mungu atatupa kiongozi bora,ajapungukiwa na watu mpaka jk aonekane yeye ni bora kuliko wengine.
 
Nchi yetu Tanzania timeshuhudia vipindi vya marais wengi.Ila kwa uelewa na ufuatiliaji wangu,tunaweza kukaa muda mrefu sana tusipoangalia katika kupata rais kama huyu JK wa pili hapa nchini.

Japo anabezwa,anakashifiwa na kuitwa dhaifu lakini ukweli utabaki palepale Kikwete ni rais bora kuliko wote tuliopata kuwashuhudia.

Siku atakayokaa pembeni tutamkumbuka.

Nadhani inafaa tumtambue kama rais wa karne ktk nch yetu.
Miaka mitatu baadae, utabiri wako umetimia. Shikamoo mkuu
 
Ni kwa sababu Jakaya Kikwete ni mmoja tu, kwa hiyo huwezi kabisa kumpata kama yeye. Lakini kwa suala la kuongoza vizuri nchi, huwezi sema nchi haiwezi kupata Rais bora kumzidi au wa kiwango chake wakati viongozi bora wanazaliwa kila siku.
Ni aibu kwako muanzisha hii thread kwa kutoa maelezo haya hadharani kwa nchi yenye raia zaidi ya milioni 45 kwa kutopata kiongozi kama yeye. Umechemka sana mkuu.
Ova
Maisha yanaendaje huko?
 
Ni kweli hatutapata kama JK na mie naomba tusimpate kama yeye kwa kuwa ndiyo uongozi pekee ambao wameongoza kwa kutorosha pesa kupeleka nje ya nchi na kuficha. Na ndiye rais aliye ahidi kurekebisha mikataba yote ya madini na hatujaona chochote. Na mengine mengi tu " kumbukeni wenyewe sina haja ya kuwakumbusha.
Upo?
 
Nchi yetu Tanzania timeshuhudia vipindi vya marais wengi.Ila kwa uelewa na ufuatiliaji wangu,tunaweza kukaa muda mrefu sana tusipoangalia katika kupata rais kama huyu JK wa pili hapa nchini.

Japo anabezwa,anakashifiwa na kuitwa dhaifu lakini ukweli utabaki palepale Kikwete ni rais bora kuliko wote tuliopata kuwashuhudia.

Siku atakayokaa pembeni tutamkumbuka.

Nadhani inafaa tumtambue kama rais wa karne ktk nch yetu.

nitajie ile mikataba 17 aliyosaini na wachina ilikuwa ya nini, mbona haijulikani?
raisi anaangalia watu wanagawana pesa kwenye rambo?
una habari gesi ya mtwara sio yetu?
hata wanyama walikuwa na wasiwasi na maisha yao, tembo walikuwa wanapungua kwa kasi nk.
 

Tanzania haitapata tena raisi kama Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Kikwete, Magufuli. Sasa la ajabu kitu gani?
 
Back
Top Bottom