Mwande na Mndewa

JF-Expert Member
Feb 26, 2021
949
2,865
TANZANIA BILA TOZO INAWEZEKANA.

Leo 12:15hrs 10/09/2022

Tozo ni makato yanayofanywa katika kila hatua ya mtu kutaka kuitumia fedha yake, jambo ambalo halishauriwi kwenye kodi,chukulia kwa mfanyakazi aliyelipwa mshahara wake benki,akitoa anakatwa tozo wakati tayari ameshakatwa kodi ya mfanyakazi (PAYE) Akiitoa aiingize kwenye akaunti yake ya M-pesa au Tigopesa, atakatwa na atakapotaka kuitoa ili aitumie atakatwa tena,Hiki ni kipato kimoja ambacho kimekatwa (kodi ya mshahara) PAYE…kwa sheria za kodi huwezi kukata kodi tatu kwenye chanzo kimoja,

Tozo sio tu kutoza kodi mara mbili kwa kipato kimoja (double taxation) bali ni utitiri wa tozo (multiplicity of levies)uliowekwa kila muamala baada ya Serikali kuona kuna miamala mingi inafanyika kidijitali,kati ya hasara nyingi za tozo,mojawapo ni,kupunguza hamasa ya kutumia huduma za fedha,Inatakiwa iondolewe,Nukuu waziri mkuu wa zamani wa Uingereza, Margareth Thatcher aliyewahi kusema: “Hakuna nchi iliyowahi kuendelea kwa kuwatoza wananchi wake kodi kuliko kiwango chao cha kuweza kulipa.”

Wakuu wa mabenki nchini walisema tozo ni pato la Serikali, hivyo wenye mamlaka ya kuiondoa ni Serikali na siyo benki.Wakuu wa mabenki wanatamani wananchi wengi watumie huduma za kifedha kwa njia ya kielektroniki na kidijitali, hivyo tozo ikiondolewa italeta unafuu wa huduma za kibenki na kuleta fedha zaidi kwenye mfumo rasmi,tozo imeua utunzaji wa fedha kwenye mfumo rasmi.Tukiondoa tozo kwenye huduma za kibenki, itaongeza uhuru wa wananchi kufanya malipo kupitia benki na miamala ya fedha kielektroniki ambayo ni njia ya haraka na salama,

Tozo hii si kodi ya biashara wala si kodi inayotokana na faida ya biashara, bali chimbuko lake ni ushirikiano wa pamoja kuunganisha nguvu ili tuweze kupata rasilimali tutekeleze majukumu hayo ambayo ni ya lazima,lakini kwa tathmini tozo ina athari za kwenye uchumi kuanzia kwa watu wa chini, hivyo inakwenda kinyume na misingi inayokubalika duniani na haipaswi kutumika.tozo katika miamala ya simu, benki, visimbuzi, kwenye mita za umeme-Lipa Umeme Kadiri Unavyotumia (LUKU), tozo kwenye mafuta ya diseli, taa na petroli na pia kadi za simu.Tozo hizi zinagusa mapato binafsi ya mtu, ambayo pengine yashakatwa kodi zingine (personal income tax),baadhi ya wananchi wamelalamika kukatwa tozo ama kodi mara tatu kwa mapato yale yale na kwa viwango vinavyoonekana kama mzigo kwa mwananchi.

-Rasilimali za Watanzania zinazoweza kuondoa tozo na kodi za kwenye mafuta na kupunguza mfumuko wa bei za bidhaa.

Bandari ya Dar es Salaam ambayo inahudumia nchi tano,Zambia,Malawi,Rwanda,Burundi,na Congo,Kabla ya Rais Magufuli mapato ya bandarini yalikuwa kati ya Sh200 bilioni hadi Sh300 bilioni kwa mwezi, lakini baada ya kuingia Rais Magufuli na kudhibiti mianya ya uingizaji mizigo, Aprili 2016 walikusanya Sh458 bilioni na Juni 2016 walikusanya Sh517 bilioni,mapato ya bandarini yaliongezeka kwa sababu waliziba mianya ya uingizaji mizigo kwa njia zisizo rasmi na walijipanga vema kuhakikisha mizigo yote inapita bandarini na kulipiwa kodi stahiki,hivi sasa Serikali inaweza kuongeza ufanisi na kukusanya zaidi ya Bilioni 600 hadi 700.Mlima Kilimanjaro ambae ni mrefu barani Africa,ambapo Watalii wanafika kileleni wakitembea na fimbo urefu wa 5,895 mita,Ziwa Manyara lenye aina ya ndege 600 wanaotua kunywa maji,moja kati ya ziwa zuri kuliona kwa macho hapa duniani,Serengeti National Park,

Rasilimali ya dhahabu,Almasi,Tanzanite ,Ruby,rhodolite,sapphire,emerald,amethyst,chrysoprase,peridot, tormaline,chrysoberyl,spunels,garnets,zircons,Coal,Uranium,soda,kaolin,tin, gypsum,phosphate, rasilimali hizi zote zinazomilikiwa na Serikali kwa asilimia 100 zinaweza kutupa pesa itayoondoa tozo,pesa itayoondoa kodi ya kwenye mafuta petrol na dizeli na kuyashuka toka 3,300 hadi 1,800 kwa lita moja,nashauri uwazi kwenye upatikanaji wa madini ili Serikali iweze kupata kodi na kuendesha mambo yake bila tozo.

Serikali itaweza kupata kodi endapo itasimamia vyema ukusanyaji kodi husika kwa kiwango kinachoridhisha na kwa kila kinachostahili sasa hili linakuwa gumu ukizingatia kasi ya ufisadi ambayo sasa imekuwa ndio style ya maisha ya viongozi mbalimbali,kama kuna anayedai yeye si fisadi basi ni suala la muda tu kabla mambo yake hayajagunduliwa au yuko smart tu mambo yake hayajulikani,

-Rasilimali Maji iliyopo Tanzania,kwa ajili ya kilimo.

1.Ziwa Victoria ambalo linakwenda kumwaga maji katika mto Nile na kuhudumia nchi ya Kenya,Uganda na Misri huku Tanzania ikiwa hakuna inachofaidika nalo hususani kwenye kilimo.
2.Mto Ruvu

3.Mto Wami

4.Mto Pangani

5.Mto Rufiji

6.Ziwa Tanganyika

7.Ziwa Nyasa.

8.Ziwa Manyara.

9.Ziwa Eyasi

10.Ziwa Rukwa

-Rasilimali Samaki

Eneo la uvuvi la bahari ya Hindi,kilomita 223,000 ,Nile perch,Sardines,prawns ambao wanapatikana kwa wingi na wamekuwa wakisafirishwa,ikiweza kuchangia 1.6% GDP kama juhudi ikifanyika tunaweza kufanya rasilimali samaki wakachangia 30% GDP na kutengeneza ajira kwa asilimia 30%

-Aina ya Samaki wa kuuza nje ya nchi.

1.Nile perch(Lates niloticus)

2.Tilapia(Oreochromis niloticus)

3.Dagaa (Lake Sardine) Rastrineobola argentea wanaopatikana Ziwa Victoria.

-Samaki wa Ziwa Tanganyika.

1.Dagaa (Stolothrissa tanganicae and limnothrissa miodon)

2.L.Stappersii,L.Marie na L.Microlepis.

-Samaki wa Ziwa Nyasa

1.Tilapia

2.Haplochromis spp

3.Lake Sardines Engraulicypris sardella.

Kwa makisio Serikali inaweza kuvuna tani 730,000 za samaki kutoka Ziwa Victoria,Ziwa Tanganyika,Ziwa Nyasa,makisio yakiitoa EEZ ambayo haijafikiwa kiuvuvi.

-Kodi tulizonazo hivi sasa kabla ya kujumlisha tozo.

Kodi kwenye mapato kwa wafanyabiashara binafsi (income tax), kodi ya mapato kwa makampuni (corporate tax), kodi ya mapato kwa wafanyakazi (mfano PAYEE), michango ya mifuko ya hifadhi ya jamii (Social security), Kodi ya majengo (property tax), kodi ya ardhi, kodi na ushuru wa kusafirisha na kuingiza bidhaa nchini, kodi ya ongezeko la thamani (VAT) , kodi ya faida ya mtaji (capital gains tax) na kodi nyinginezo nyingi.

-Tufute kodi hizo,tutumie vizuri rasilimali zetu tuzizobarikiwa na Mungu,kupata yafuatayo.

1.Mtu binafsi hatolipa kodi ya mapato,Serikali itakusanya Payroll Tax yaani Paye ama kodi ya malipo ya mshahara,kupitia kodi hii Serikali inaweza kufanya kila mfanyakazi akakatwa asilimi 6% ya mshahara wake unaokwenda serikalini,kodi hiyo ya payee 6% itakuwa kama kuongeza tu uwajibikaji wa wananchi wa Tanzania kwenye kuchangia shughuli na huduma za maendeleo.Rasilimali zitasaidia sana kujenga uchumi wa taifa hili la Tanzania,Ni jukumu letu kufanya sekta binafsi katika taifa hili kuwa imara zaidi ili kuvutia wawekezaji wengi wa ndani na nje.Yote yatawezekana kama mfumo wetu wa masuala a kodi utakuwa rafiki kwa wazawa na wageni.

Nimalizie kwa hoja inayoulizwa sana na Wananchi, ni tozo ama kodi ngapi zinawekwa, unaziweka maeneo gani na viwango gani vya gharama za hizo kodi ama tozo unakata? Pengine maswali haya ndiyo yanaleta mjadala mkubwa hapa nchini Tanzania,maoni yangu nimeyatoa,nashaauri tena Tanzania inaweza kuandika historia kuwa nchi pekee ambayo Wananchi wake wanaishi bila kulipa kodi ya Mapato yaani income tax,Mapato ya kuendesha Serikali yanaweza kutokana na gawio kutoka kampuni za Serikali na sales tax kwenye bidhaa na huduma,Pumzika kwa amani Hayati Rais John Pombe Magufuli ulikuwa unatupeleka uko ila ukaondoka ghafla,Formula yangu itabaki pale pale (Nchi kubwa= watu wengi na makusanyo makubwa.) rasilimali tunaweka ziliwe na mchwa (Nchi ndogo = watu wachache na makusanyo kidogo) rasilimali zinajenga nchi case study ya Rwanda.

Nikiishia hapa,Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854

-Bachelor of Business Administration in International Business.

-Master of Leadership and Management.

Recent Publications;-
-Assessment on the Effects of Micro-Financing on Poverty Reduction.
 
Back
Top Bottom