Tanzania: Big banks' profits fall amid continuing industry woes

Tanzania: Big banks' profits fall amid continuing industry woes

Mimi nikienda bank nachukuwa forms 2.
1. Deposit slip
2. TT transfer form.
Baada ya experience ya FBME, hela yangu hailali kwenye account. Tena nafanya haya kabla ya saa sita mchana ili kuhakikisha hela isilale kwao.
Hahaaaa
 
Jamani, sasa mnatakaje? mnataka achukue hela awawekee mfukoni? kuwa wabunifu! No longer bussness as usual!
 
Miamala siku hizi ni kupitia mitandao ya simu,hizo bank baadae sana
 
Benki ndio msema ukweli
Tukumbuke 2008
 
Kwa mlinganisho na uchumi wetu bado hizo ni faida kubwa sana. Bilioni 35 ni zaidi ya fedha zilizojenga mabweni mapya UDSM na fedha walizopewa Magereza kwa ajili ya kujenga makazi Ukonga, combined!

Hayo mabenki yametangaza faida za makumi ya mabilioni baada ya kuondoa gharama za uendeshaji na kujilipa marupurupu yao kebekebe. Ni faida kubwa.

Ukilinganisha na faida walizokuwa wakipata wakati wa uchumi wa madili na ukwapuaji wa fedha za uma (yaani wakati wa kula na wezi) unaweza kusema faida sio kubwa. Ila sasa inawezekana ni faida halali.
Sidhani kama umeelewa. Rudia kusoma tena

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ahueni iliyoanza kujitokeza kwenye sekta ya fedha nchini, imepigwa dafrao baada ya faida ya benki kubwa kupungua kwenye robo ya pili ya mwaka huu.

Itakumbukwa, benki hizo ziliyumba kuanzia robo ya tatu mwaka jana kutokana na mabadiliko kadhaa yaliyofanywa na Serikali ikiwamo kuhamisha akaunti zote za taasisi za umma kutoka benki za biashara kwenda Benki Kuu (BoT).

Ingawa taasisi hizo zilianza kwa faida, bado ilikuwa chini ya iliyopatikana mwaka jana. Hili linathibitishwa na taarifa za benki za NMB na CRDB ambazo zinaongoza kwa amana na idadi ya wateja, ukubwa wa mtaji na mtandao wa matawi ndani na nje ya nchi.

Kwenye robo ya pili; Aprili mpaka Juni, Benki ya NMB ilipata faida ya Sh35.29 bilioni ikiwa ni chini kulinganisha na ile iliyopatikana kwenye robo ya kwanza au kipindi kama hicho mwaka jana. Kwenye robo iliyoishia Machi, benki hiyo ilipata faida ya Sh40.9 ambayo inafanya faida kuwa nusu mwaka huu, ambayo ni Sh76.2 bilioni ikiwa ni pungufu kwa Sh8.1 bilioni ya iliyopatikana kwenye kipindi kama hicho mwaka jana.

Ndani ya muda huo, NMB imeongeza watumishi 103 kutoka 3,316 waliokuwapo mwaka jana. Ndani ya muda huo pia, imeongeza matawi kutoka 178 mpaka 201. Ingawa ipo chini ya kiwango kinachopendekezwa na kanuni za BoT, uwiano wa mikopo isiyolipika na ile ghafi imeongezeka kutoka asilimia 4.6 mwaka jana, mpaka asilimia 4.9 mwaka huu.

Kwa upande wa Benki ya CRDB yenye thamani ya Sh5.49 trilioni, faida yake baada ya kodi, imepungua kwa zaidi ya asilimia 50 kutoka Sh27.47 bilioni mwaka jana mpaka Sh13.39 bilioni kwenye robo ya pili. Pamoja na matawi yake yaliyopo Burundi, faida hiyo imepungua pia kutoka Sh28.5 bilioni mpaka Sh13.74 bilioni mwaka huu. Uhakiki wa watumishi hewa pamoja na kusitishwa kwa mishahara ya wenye vyeti feki, kumeendelea kujidhihirisha kwenye taasisi za fedha nchini. Kiwango cha uwiano wa mikopo isiyolipika kwa Benki ya CRDB kimeendelea kuwa juu ya asilimia tano zinazopendekezwa na kanuni za BoT. Ingawa uwiano huo umeshuka kutoka asilimia 14 zilizokuwapo mwaka jana mpaka asilimia 13 mwaka huu, lakini bado upo juu ya unaoshauriwa.

Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk Omary Mbuta alisema mwenendo huo unamaanisha mambo mengi ya kuzingatiwa ikiwamo ushindani kutoka benki ndogo. “Hali hii inadhihirisha kwamba zilikuwa zinafanya zaidi biashara na Serikali hivyo kujiondoa kwake na mabadiliko mengine yaliyofanywa, kumeziathiri,” alisema Dk Mbura.

Kujiondoa kwa taasisi za serikali kwenye benki hizi, kulipunguza amana za wateja wa benki za biashara kwa zaidi ya Sh900 bilioni huku CRDB pekee ikipoteza zaidi ya Sh700 bilioni. Kutokana na ukweli huo, alizitaka kubadili mikakati ili kuendana na ukweli wa mwenendo wa soko. “Wafanyakazi wanaowaajiri wanatakiwa kuongeza ushindani sokoni hasa kuziona fursa zilizopo kwenye sekta binafsi,” alisema.

Hali ilikuwa tofauti Benki ya NBC ambayo imepata faida ya Sh5.2 bilioni kwenye robo ya pili ikiongezeka kutoka Sh3.39 bilioni iliyopatikana kwenye robo iliyoishia Machi mwaka huu. Ufanisi wa benki hii umetokana na kuongezeka kwa mapato yatokanayo ya riba; kutoka Sh28.8 bilioni za Juni 2016 mpaka Sh33.86 bilioni mwaka huu. NBC, CRDB na NMB ndizo benki zenye idadi na amana kubwa za wateja huku matawi yake yakifika maeneo mengi; NBC inayo 51 hivyo kwa pamoja kuwa na zaidi ya nusu ya matawi yote yaliyopo nchini.

Licha ya benki hizo mbili, hali imekuwa hivyo kwa Exim ambayo faida yake imepungua kwa zaidi ya robo tatu kwa miezi sita ya mwanzo. Benki hiyo imepata faida ya Sh13.95 bilioni kutoka Sh57.85 bilioni zilizopatika mpaka Juni mwaka jana.
 
voda wenyewe wapo hoi, wameuza hisa hata kutangaza hawataki.
Jamaa wamekaa kimya kabisa,hii ni mfano mbaya kwa kampuni za simu ambazo hazijauza hisa,Wateja watasita,

Mauzo yako chini sana

Halafu hii ya mtu kuanzisha kampuni kwa hela yake halafu unamlazimishia watu wengine wajiunge naye(hisa) imeanza lini?

Kampuni niianzishe na kuisotea halafu ikinoga uje unijazie watu tena kwa kunilazimisha?
 
Acha zife zote tutabaki na benki moja benki kuu ya taifa, hii itaipa serikali uwezo wa kudhibiti mzunguko wa fedha😀
 
Lakini pia watumishi wa idara hiyo walibweteka sana kwakuwa pesa zilikuwa zinakuja tuu toka mashirika ya UMMA, kazi yao kubwa ilikuwa ni kuangalia akaunti ipi inatoa hela ndogo kulingana na kilichopo kisha wanajikopesha wenyewe, siku ukitaka kutoa Zaidi....migogoro inaanza.

Sasa watoke kwenye viyoyozi waingie mtaani kuitafuta hiyo pesa.

Si lazima, chama lile tunalidai sana tuu.
 
Izi bank zilikua zinaweka pia pesa za wapiga dili sasa iyo ndio faida halisi na uwezo wao wa kuzalisha faida!
 
Back
Top Bottom