Histohisia inapogeuzwa historia basi historia inapoteza maana yake!!! Maandishi ya Mohammed Said yamejaa histohisia zaidi kuliko historia!
Hii Speed 120 hadi kwenye kona tunayokwenda nayo ni kali sana,
Hebu twende pole pole kidgo,
Huu ni mjadala,na suala linalozungumziwa hapa ni historia ya nchi hii na namna mashujaa wake wanavokumbukwa,
Ukoloni wakati unaingia uliikuta Tanzania ni nchi yenye watu na iman zao,za dini na kimila na utamaduni,
Miongon mwa Agents wa colonialism tunakumbuka walikuwapo missionaries,
Pindi missionaries wanafika huku kwetu tayar walishakuta watu na iman zao mbali mbali,
Hatusemi kwamba kipindi hicho taifa hili lilikuwa ni dola ya kiislam la hasha,lilikua ni dola la watu wenye iman mbali mbali lakin walioish kwa aman na upendo,history inasema ivo,
Sasa hoja iko hivi,ngoja mimi nikufafanulie vyema uielewa Mwanakijiji,,
Hoja ni hii hapa:
Wakati wakoloni wanaingia kwenye ardhi zetu kulikua na harakati za jamii ya watu mbali mbali kuupinga ukolon huo kwa vipindi tofaut tofauti,watu wenye iman za dini,watu wenye iman za kimila na kiafrika na kadhalika,
Wakati ukoloni unaingia ndan ya ardhi hii kulikuwapo waislam kama wana jamii wa taifa hili,hawa nao kwa wakati na nafas zao walipigana na ukoloni kwa namna mbali mbali,na hawakupigana ili waje kusimamisha dola ya kiislam bali walipigana kupinga uovu huo wa ukoloni na madhila yake,
Sasa kwanin wale mashujaa waliopigania nchi hii na waliopigana kuutomeza ukoloni kwa ngao ya utaifa wafutwe au washindwe kuenziwa kama mashujaa wengine?
Au kwa kuwa wao wameonekana kuwa walikuwa ni waumin wa iman flan tuseme ni waislam?
Badala yake baadhi tuh wamekuja kupewa coverage na kuonekana kama hao ni ma-heroes wa taifa hali ya kuwa uhalisia hauko ivo,je vizaz vijavyo vitakuja kusoma historia ya namna gani ya taifa lao?
Kwan tunajua kila taifa lina historia yake,na hapa tunawekana sawa kuhusu uhalisia wa historia ya taifa letu.hatupiganii uislam wala hatupiganii ukristo,wala hatuweki hisia,,,
Mbona sijaona mahala katika uchambuz wa Moh Said alipoelezea kwamba harakati za wale wazee zilikuwa ni kuweka uislam ndan ya taifa hili?
Ila ameeleza kwamba asilimia kubwa ya wale wazee ambao walikuwa washirika wa nyerere na watu wengine walikuwa waislam,sasa kwanin historia ikawafuta na kuwapuuza?imefanya hivyo kwa kuwa wao ni waislam?
Hapo ndipo kwenye hoja kuu,
Hoja sio histohisia,wala sio uchochez na choko choko,sema mara nyingi ukweli huwa unakuwa mchungu au unakuwa ni kitu kigeni machoni mwa wengi,lakin uzuri zaid mwandish kaweka rejea mbali mbali hapo waweze kuzipitia na kujionea.