Nawapa pongezi Mkurugenzi na Wafanyakazi wa TANTRADE kwa kujitahidi kuendana na kasi ya Dunia kutangaza fursa

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
891
4,162
TANTRADE ni moja ya taasisi ambazo kwa kiasi kikubwa imeweza kuendana na mahitaji ya biashara kwa Dunia ya sasa. Wameondoka kuendesha maonyesho ya sabasaba na sasa wanaangalia fursa za maonyesho nje na kuwapa opportunity hata wale ambao wanashindwa kuvuka mipaka kupeleka bidhaa zao.

Uimara wa TANTRADE unao mchango mkubwa sana katika kuwalinda wazalishaji na wauzaji wa ndani kwenye masoko ya nje. Ukisafiri kwenda Duniani kwa mwamvuli wa TANTRADE means serikali ipo nyuma yako na unakokwenda pia wanakuheshimu.

Nadhani hawa watu wakiungana na watu wa Wizara ya Mambo ya Nje wenye business mind, bidhaa zetu zitafanikiwa kupenya masoko ya nje na hivyo kukuza export.
 
Back
Top Bottom