Uingereza kuibeba bendera ya Tanzania kutangaza fursa za uwekezaji, biashara zilizopo sekta ya madini

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,813
11,991
#Madini mkakati yapewa kipaumbele na Uingereza

#Wafanyabiashara wa madini Uingereza kushiriki Jukwaa la Kimataifa Sekta ya Madini mwezi Oktoba


Wizara ya Madini na Serikali ya Uingereza kupitia Ubalozi wake nchini zimekutana leo Agosti 1, 2023 katika ofisi za Wizara Mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma ili kujadiliana kuhusu fursa mbalimbali za uwekezaji katika Sekta ya Madini nchini na kuzitangaza kwa wawekezaji kutoka nchini humo.

Aidha, mkutano huo umejadili uwezekano wa nchi zote mbili kuwa na ushirikiano katika maeneo mbalimbali katika Sekta ya Madini.

Akizungumza katika kikao hicho, kiongozi wa Ujumbe wa Serikali ya Uingereza ambaye pia ni Mkurugenzi wa Nchi Kitengo cha Biashara nchini Bi. Anna-Maria Mbwette na ujumbe wake alipokutana na kuzungumza wa wataalam wa Wizara ya Madini kuhusu fursa mbalimbali za uwekezaji katika sekta ya madini nchini ikiwemo uendelezaji wachimbaji wadogo.

Kupitia majadiliano hayo, Serikali ya Tanzania na Uingereza zimejadili uwezekano wa kushirikiana kwenye maeneo mbalimbali katika Sekta ya Madini, hususani shughuli za uongezaji thamani madini; uendelezaji wachimbaji wadogo; uchimbaji; uchenjuaji na uongezaji thamani na biashara ya madini hususani madini mkakati na kujenga uwezo wa Taasisi chini ya Wizara katika usimamizi wa Sekta.

‘’Mambo haya tuliyozungumza ni muhimu sana katika kuendelea kuimarisha mahusiano na katika biashara na uwekezaji wa shughuli za madini kati ya Tanzania na Uingereza.Tunaahidi kushirikiana na Wizara ya Madini na Serikali kwa ujumla katika kutangaza fursa mbalimbali zilizopo hapa nchini,’’ amesema Mbwette.

Ameongeza kuwa, nchi ya Uingereza imevutiwa na vipaumbele vya Wizara ya Madini hususan katika uendelezaji wa madini muhimu na madini mkakati nchini. Amesema Serikali ya nchi hiyo itaweka nguvu katika kuvutia wawekezaji wengi kuwekeza katika madini hayo ya mkakati kama vile madini ya nickel, Cobalt, graphite, lithium, niobium,Rare Earth Elements (REE)

Vile vile, amesisitiza kuwa, Uingereza inatarajia kuweka nguvu katika kuwajengea uwezo wadau wa Sekta ya Madini kuweza kushiriki ipasavyo katika uchumi wa madini. Pia ubalozi utashirikiana na Tanzania kwa kutumia uzoefu wao katika maandalizi ya kuandaa Mpango Mkakati wa miaka 10 katika Wizara ya Madini.

Katika hatua nyingine, Mbwette amesisitiza kuwa, Uingereza itaweka nguvu kubwa katika kutangaza Jukwaa la Kimataifa katika Sekta ya Madini linalotarajiwa kufanyika Oktoba 25 na 26, 2023 jijini Dar es Salaam ili wafanyabishara na wadau wa Sekta ya Madini waweze kufahamu na kushiriki kwa wingi katika kongamano hilo ili kuendeleza mahusiano ya biashara na uwekezaji.

Naye, Kaimu Kamishna wa Madini Maruvuko Msechu amesema ushirikiano huo kati ya Tanzania na Uingereza utainufaisha nchi yetu kwa kuongeza uzalishaji na hatimaye mchango wa sekta ya madini kwenye pato la Taifa. Amesema vipaumbele hivyo ni muhimu sana kwa sasa hususan duniani kwenye uhitaji mkubwa wa madini hayo muhimu.

Kwa upande wake, Kamishna Msaidizi Uendelezaji Migodi Terence Ngole amesema kuwa lengo la mazungumzo hayo ni kuanzisha ushirikiano baina ya nchi hizi mbili, kuangalia namna kampuni za nchini Uingereza zinavyoweza kunufaika na fursa mbalimbali za uwekezaji katika Sekta ya Madini nchini.

Aidha, Kamishna Ngole ameeleza kwamba pamoja na fursa nyingi zilizopo katika Sekta ya Madini nchini, hata hivyo majadiliano hayo yalijikita zaidi katika maeneo ya uongezaji thamani madini, uendelelezaji wachimbaji wadogo, kujenga uwezo kwa wataalamu kwenye weledi mbalimbali zinazohitajika katika Sekta (capacity building in relevant Mining Sector skills and technologies) na Utafutaji, uchimbaji na uchenjuaji na uongezaji thamani na biashara ya madini kwa ujumla yakiwemo madini ya mkakati (critical minerals development strategy).

Katika kikao hicho, Uingereza imeikaribisha Wizara ya Madini katika Mkutano mkubwa wa madini (Mining Investment Forum) utakaofanyika Oktoba 16, 2023 nchini humo. Mkutano huo utawakutanisha wawekezaji na wadau mbalimbali katika Sekta ya Madini duniani.
IMG-20230801-WA0024.jpg
IMG-20230801-WA0027.jpg
IMG-20230801-WA0025.jpg
IMG-20230801-WA0026.jpg
IMG-20230801-WA0028.jpg
IMG-20230801-WA0029.jpg
IMG-20230801-WA0030.jpg

Mkurugenzi wa Nchi Kitengo cha Biashara na Uwekezaji kutoka Ubalozi wa Uingereza nchini Bi. Anna-Maria Mbwette akizungumza alipokutana na wataalam wa Wizara ya Madini kuhusu fursa mbalimbali za uwekezaji katika sekta ya madini nchini ikiwemo uendelezaji wachimbaji wadogo jijini Dodoma
IMG-20230801-WA0031.jpg
IMG-20230801-WA0032.jpg
 
Hii mikataba isipofanyiwa utafiti kuna siku mtajikuta mmeuza maeneo ya JW na magereza.
 
Back
Top Bottom