Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,812
- 11,989
Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) wamewasili Visiwani Zanzibar kushiriki kwa mara ya kwanza Maonesho ya Biashara ya Kimataifa yaliyofunguliwa tarehe 10.01.2024 na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussen Ali Mwinyi eneo la Dimani - Fumba Zanzibar ili kunadi vivutio na fursa za uwekezaji zinazopatikana ndani ya hifadhi hizo zilizoenea takribani mikoa yote ya Tanzania Bara.
Akifungua Maonesho hayo, Rais wa Zanzibar Mhe. Dkt. Hussen Mwinyi alisema, "Mbali na maonesho hayo kuwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar pia ni fursa adhimu ya kuwakutanisha wafanyabiashara wa ndani na nje ya nchi kubadilishana uzoefu na kujua masoko mapya ya biashara na utalii".
"Aidha, tumeshuhudia watalii wengi wanaopenda fukwe wakiwasili Zanzibar kwa wingi, hivyo tutatumia fursa hii ya maonesho kuongea na Makampuni ya Utalii, Mawakala wa usafirishaji na waongoza watalii wa Zanzibar wawe na vifurushi vya kutembelea Hifadhi za Taifa zilizoko Tanzania Bara", aliongeza Afisa Mwandamizi huyo.
TANAPA inayoshiriki maonesho hayo ya Kumi kwa mara ya kwanza Visiwani Zanzibar, inawakilishwa na Maafisa na Askari kutoka Kanda za Mashariki, Kusini, Nyumba ya Kumbukizi ya Mwl. Nyerere iliyopo Dar es Salaam na Caravan Serai - Bagamoyo.