Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 47,014
- 144,372
Eti leo Kamati ya Bunge ya Kusimamia Mashirika ya Umma(PAC), imekuja na taarifa kuwa TANROADS wametumia zaidi ya shilingi bilion 600 bila ya idhini ya Bunge na kwamba taarifa ya TANROADS inatia mashaka (kuna uongo).
Binafsi najiuliza katika hili ni nini cha ajabu?
Je,taarifa za aina hii zimeshatolewa mara ngapi na Bunge hili limewahi kuchukua hatua gani kwa wanaofanya matumizi bila idhini ya Bunge?
Hata hili la TANROADS kutumia zaidi ya bilioni 600 bila idhini ya Bunge nalo litapita tu kama yalivyopita mengine.
Nimeyakumbuka maneno ya Prof.Asaad yaliyopekea akaitwa kujieleza mbele ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge.