Ney wa Mitego achana na siasa, wewe ni wa kuonewa huruma, CHADEMA watakutumia na kukuacha

Nesi mkunga

JF-Expert Member
Nov 28, 2022
701
1,842
BASATA MSAMEHENI NEY WA MITEGO HAJUI MAMBO MENGI NI WA KUELIMISHWA.

Na Thadei Ole Mushi.

Tuanze na Mstari upi kwenye amkeni? ngoja tuanze na huu👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻

“ Hata ripoti ya CAG hakuna aliyechukuliwa hatua” ni moja ya mstari katika wimbo wa Ney wa Mitego wa Amkeni. Watanzania wengi hawana taarifa na uelewa wa baadhi ya mambo. Twende sawa kwenye Mstari huu kabla hatujagusa mistari Mingine.

1. Ofisi ya CAG ni kama Mkono wa Pili wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Yaani bila Ofisi ya CAG bunge haliwezi kutimiza majukumu yake ipasavyo.

2. Kazi za bunge zinajulikana ni kupitisha bajeti ya Serikali na kuisimamia bajeti hiyo. Bunge likishaidhinisha matumizi ya Serikali kwa mujibu wa Sheria na CAG kama sehemu ya Bunge huenda kufanya ukaguzi fedha zilizoidhinishwa kama zimetumika ipasavyo.

3. CAG akishakamilisha kazi yake ya Ukaguzi wa mahesabu ya matumizi ya fedha za Serikali anamkabidhi Rais ripoti hiyo yeye wa kwanza. Anafanya hivyo kwa Sababu matumizi yaliyokaguliwa ni Ya Serikali ambayo Rais ndiye anayeiongoza.

4. Rais hatakiwi hata kufungua ripoti aliyokabidhiwa anachopewa na CAG ni briefing ya kilichopo ndani ya ripoti. Akishasomewa kwa muhtasari ana nafasi ya ku Comment kwenye summary hiyo lakini haruhusiwi kisheria kufanya maamuzi yoyote kwa kutumia Ripoti hiyo.

5. Rais akishaipokea Ripoti husika hupelekwa kwa Spika wa bunge ambaye yeye na Bunge lake ndio wenye Ripoti hiyo. Kisheria Ripoti si ya Rais bali ni ya Bunge na ndio wenye mamlaka ya kuisoma na kutoa mapendekezo yao nini kifanyike.

6. Spika akishaipokea anaitable kwenye Bunge na hapo Spika anatoa taarifa kwa wabunge kuwa Ripot ya CAG imepokelewa hivyo wakachukue vitabu.

7. Wakishachukua hawajadili wakati huo huo,hutolewa Muda wa wabunge na kamati za Bunge pamoja na wataalamu kuzipitia na kutoa Ushauri na Mapendekezo. Na wakati kamati za bunge zinapopitia zinakuwa na wataalamu toka kwa ofisi ya CAG ili waweze kupata tafsiri sahihi ya kilichomo ndani.

8. Wakati wabunge na kamati zinapitia ndio wakati ambao wizara na idara zenye hoja za kikaguzi hupewa nafasi ya kujibu hoja zao kabla ya Maamuzi hayajatolewa. Inawezekana wakati wa ukaguzi Idara au wizara ilishindwa kuwasilisha baadhi ya nyaraka lakini baada ya Muda nyaraka zinapatikana na kuwasilishwa hivyo hoja husika kufutika.

9. Baada ya Kamati za bunge kumaliza kuchakata taarifa hiyo huletwa Bungeni kile walicholiona na kuwapa wabunge fursa ya kuchangia kama kuna maoni ya Ziada.

10. Baada ya uchambuzi huo ndio Rais sasa anachukua mapendekezo ya Bunge na kuyafanyia kazi. Na bado katika ngazi hii hawezi kuchukua hatua moja kwa moja bila kushirikisha vyombo vya kiuchunguzi kama TAKUKURU.

Ripoti hii ya 2022/2023 itajadiliwa kwenye bunge lijalo la September. Kwa sasa idara na wizara zinakimbizana kujibu hoja zilizopo kwenye ripoti hiyo, kwa sasa Uchambuzi unaendelea kwa kutumia kamati ya Bunge na wataalamu toka ofisi ya CAG.

Na zilizopita zilipitia utaratibu huo huo na zimefanyiwa kazi kwa mujibu wa Sheria na waliopaswa kuwajibika wamewajibika. Tatizo la watu wengine ni kutaka Serikali ikurupuke ifanye kazi kama wanavyotaka hili haliwezekani…. Maamuzi yote ya Serikali yana miongozo yake ya nini cha kufanya.

Alichokufanya Ney katika mstari huu kutokujua utaratibu, sio kosa lake anapaswa kuelimishwa ili aelewe. Lakini kupitia mstari huo unatusaidia wengine kupata elimu na utaratibu unaotumika katika kushughulika na Ripoti ya CAG. Mtu kama Ney akikosea jambo la kitaalamu kama hili unamsamehe lakini kwa Graduate anatakiwa asikosee bali ajaribu kutafuta maarifa zaidi.

Ole Mushi
0712702602
 
Ney ni mtanzania ,huyo mushi Kwa nini asimshauri diamond,zuchu,KONDE boy waache kuwaharibu watoto wenu Kwa MATUSI,kuvaa ovyo,kusuka ovyo??
 
Nini maana ya kuweka namba ya simu hapa ?all in all that's life he chose ,let him enjoy finghting for others who fear to speak .
 
Well, je ni akina nani washawahi chukuliwa hatua stahiki pamoja na kupelekwa Mahakama kupitia report za CAG? Au ndo kwamba suggestions zote za CAG hua ni wrong?

NB; Unaposema Ney anatumiwa na CDM well, je ni kiongoz gan Nchi ashachukuliwa hatua kutokana na ufisadi? Madudu ni mengi san halina ubishi. Mtanzania akikosoa juu ya mamb ya kifisadi tumuunge mkono!!!
 
Back
Top Bottom