Tangu alipofariki Shujaa wa Afrika John P Magufuli taifa la Tanzania lina mpasuko mkubwa kisiasa, kidini na hata Ideologically

Tangu alipofariki Shujaa wa Afrika John P Magufuli taifa la Tanzania lina mpasuko mkubwa kisiasa, kidini na hata Ideologically

Nyankurungu2020

JF-Expert Member
Joined
Oct 2, 2020
Posts
4,281
Reaction score
7,061
Mwenye akilpi ndogo kama punje ya haradali atabisha.

Ukweli ni kwamba rais Magufuli alikuwa ameliunganisha taifa kwa kila namna. Na ndio maana hata aliposema tuweke siasa kando hata Wananchi wa kawaida hawakulalama. Maana waliona anapiga kazi kwa wananchi wote.

Aliunganisha wananchi wote wa kila dini. Ndio maana alipambana kuhakikisha ule msikiti mkubwa unakamilika maeneo ya Kinondoni.

Ideologically taifa liliungana na kuwa kitu kimoja maana hata wale wanyonge walianza kupata confidence kuwa taifa lao lipo mikononi mwao.

Tangu amefariki kwa kutatanisha maana alipotea zaidi ya wiki nne bila kuonekana hadharani. Taifa limeganyika.
 
Haya yanatokea sasa, ni matokeo ya ulevi wa madaraka wa Magufuli. Hakuna namna utamtoa Magufuli na huu upuuzi wa sasa. Inshort tumeangukia kwa Samia, lakini tukijikwaa wakati wa dhalimu Magufuli.
 
Magufuli ndio muasisi wa mauaji Tanzania,wengine wanatemba na model baada ya kuona alifanya Magufuli na hakuna kilichotolea.
Magufuli alikuwa anapenda sana maendela na Tanzania but alikuwa hana leadership skills na alikuwa hana exposure.
Usukuma a.k.a ushamba ulimugjramu sana
 
Mpasuko upo. Na kwa maoni yangu sababu ni wana CCM kutomtaka Samia. Hii imesababisha mashirikiano ya kutumiana baina ya CCM wasiomtaka Samia na Chadema.
 
Haya yanatokea sasa, ni matokeo ya ulevi wa madaraka wa Magufuli. Hakuna namna utamtoa Magufuli na huu upuuzi wa sasa. Inshort tumeangukia kwa Samia, lakini tukijikwaa wakati wa dhalimu Magufuli.
Ukiachana na chuki zako kwa shujaa wa Afrika. Unakiri wazi kuna mpasuko. Pia unakiri utawala wa Magufuli ulikuwa bora.
 
Ukiachana na chuki zako kwa shujaa wa Afrika. Unakiri wazi kuna mpasuko. Pia unakiri utawala wa Magufuli ulikuwa bora.
Mpasuko ulianzishwa na Magufuli kushurutisha nchi hii kutawaliwa na ccm. Usitake kutuona hatujui huu upuuzi wa ccm chanzo chake ni nani.
 
Mpasuko ulianzishwa na Magufuli kushurutisha nchi hii kutawaliwa na ccm. Usitake kutuona hatujui huu upuuzi wa ccm chanzo chake ni nani.
Kuwa analytical. Mbona kulikuwa hakuna mpasuko kwa wananchi na walimuunga mkono. Wewe peke yako ukakaza makalio kumpinga na ukaonekana mpuuzi
 
Kwa sasa kuna mpasuko mkubwa wa udini hasa seeikalini,waislamu wanaona huu ndio wakati wao wa kugandamiza wakristo
je unamaanisha na wao walikua wanagandamizwa hapo kabla? --- nataka nikupe mifano miwili tusaidiane kufikiri kwamba je kuna tatizo tulilifumbia macho hapo kabla au ni double standards za kila siku katika jamii tu

1. Leo hii akiteuliwa mzanzibar kwenye nafasi yeyote unasikia maneno anateua wazanzibari wenzake au unasikia wanzanzibar awamu hii wanasikika sana --- swali langu je walivyoteuliwa wasiokua wazanzibari na raisi ambaye hakua mzanzibari inamaana wabara/tanganyika walikua wanapendeleana?

2. Leo hii akiteuliwa muislamu kwenye nafasi yeyote unasikia maneno anateua waislamu wenzake au unasikia waislamu awamu hii wanasikika sana --- swali langu je walivyoteuliwa wasiokua waislamu na rais ambaye hakua muislamu inamaana wakristo walikua wanapendeleana?
 
Kuwa analytical. Mbona kulikuwa hakuna mpasuko kwa wananchi na walimuunga mkono. Wewe peke yako ukakaza makalio kumpinga na ukaonekana mpuuzi
Kipimo cha kiongozi anayekubalika ni kuheshimu uhuru wa maonu ni kuheshimu uchaguzi, Magufuli hakuwa na sifa yoyote kwenye hayo. Hakukuwa na mpasuko wakati Samia kaingia wimbo ukawa ni kulileta taifa pamoja, au unadhani upuuzi huu wa Samia utatusahaulisha ukatili wa dhalimu Magu?
 
Haya yanatokea sasa, ni matokeo ya ulevi wa madaraka wa Magufuli. Hakuna namna utamtoa Magufuli na huu upuuzi wa sasa. Inshort tumeangukia kwa Samia, lakini tukijikwaa wakati wa dhalimu Magufuli.
Sure, muasisi wa kesi za kubambika,utekaji na kupoteza watu ni huyu!

Thou alifanya maendeleo makubwa sana ndani ya muda mfupi kuliko watangulizi wake ila hiki kikombe hawezi kukikwepa.
 
Back
Top Bottom