GE2025 Waraka wa Katibu Mkuu CHADEMA, John Mnyika juu ya Hotuba ya Rais na Maombolezo ya wafia Demokrasia

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

CHADEMA

Political Party
Joined
Apr 13, 2013
Posts
495
Reaction score
2,540
Ujumbe wa Katibu Mkuu Na. 3 wa 2025: Juu ya Hotuba ya Rais Haramu ya 3/11/2025 na maombolezo ya wafia demokrasia, uhuru na haki ya tarehe 5 mpaka 11 Novemba 2025.

Makamanda, wapendwa na ndugu nawasalimu kwa salamu zote za Chama na salamu za imani zenu kwa Mungu.

Naomba mrejee taarifa kwa umma niliyotoa tarehe 2 Novemba 2025, hotuba ya Rais Haramu ya tarehe 3 Novemba 2025 na tangazo la Mkurugenzi wa Mawasiliano Chadema la tarehe 4 Novemba 2025.

Kwa mara nyingine nitoe pole kwa familia za marehemu wafia haki, uhuru na demokrasia kutokana na uchafuzi wa mwaka 2025 kabla, wakati na baada ya uchafuzi huo.

Nakuomba wewe unayesoma ujumbe huu uungane nami kusimama dakika moja kwa heshima ya marehemu wetu na tumwombe Mwenyezi Mungu azilaze roho zao katika haki, amani na furaha ya milele.

Kwa wagonjwa nawatakia heri katika matibabu na ni sala yangu kuwa Mwenyezi Mungu awajalie neema ya uponaji.

Kimsingi hakukuwa na uchaguzi 2025. Na tunawashukuru Watanzania kwa kutekeleza kwa namna mbalimbali maamuzi ya No Reforms No Election. Mwenyezi Mungu awajaze rehema na baraka kwa majitoleo yenu.

Natambua kwa Chadema tuko kwenye kipindi cha maombolezo ya wiki moja kuanzia tarehe 5 mpaka 11 Novemba 2025 ambapo bendera za Chama zinapepea nusu mlingoti. Nashukuru wote walioungana nasi kutangaza maombolezo ya Kitaifa. Naiasa Serikali dhalimu nayo kutangaza maombolezo ya Kitaifa. Na nawaomba wadau wote wa haki, demokrasia na uhuru nanyi kutangaza maombolezo kila mmoja kwa namna yake. Nawaomba viongozi wa dini, kiroho na wote mnaothamini uhai na utu nanyi kutangaza maombolezo ya Kitaifa. Taifa letu linahitaji toba na uponyaji na hatua mojawapo muhimu katika mchakato huo ni maombolezo ya marehemu wa maafa ya kinachoitwa na watawala haramu na vyombo vyao "Uchaguzi Mkuu 2025".

Pamoja na kuwa katika kipindi cha maombolezo nimelazimika kuandika ujumbe huu kutokana na upotoshaji unaoendelea kufuatia hotuba ya Rais Haramu ya tarehe 3 Novemba 2025 kabla haijaleta taathira na madhara zaidi.

Ni udhalimu na udhaifu kwa Rais Haramu kuanza hotuba yake ya mara baada ya kuapa kwa kushika Quran kuanza kwa kusema uongo kwa kuipongeza Tume ya Uchaguzi isiyokuwa huru kwa "kuendesha uchaguzi kwa ufanisi usiotiliwa shaka". Toba na tiba kwa Taifa inaanza kwa kuwa wakweli mbele ya Mungu na watu ambao ni Sauti ya Mungu. Rais Haramu anapaswa kujirudi kwa kukiri ukweli hadharani kwa kuwa uongo wake umefanya vyombo vyake na wafuasi wake kuchukua mwelekeo wa kuwa hakuna tatizo kwenye taifa letu lenye kuhitaji suluhisho la haraka.

Rais Haramu amehamisha lawama ya mgawanyiko wa uchafuzi mkuu 2025 bila kujitazama ndani na kujikumbusha ukweli kuwa mgawanyiko huo ni matokeo ya kiburi chake, cha Serikali yake na Chama chake CCM kukataa kusikiliza sauti ya watu, sauti ya vyama vya kweli vya upinzani na sauti za wadau wengine muhimu waliotaka reforms kabla ya uchaguzi mkuu 2025 kwa kufanya marekebisho ya kikatiba, kisheria na kitaasisi kuweka mazingira ya kuwa na chaguzi huru na haki. Sauti ambazo zimepazwa kwa nyakati na njia mbalimbali toka aliporithi urais Machi 2021.

Mwito wa kutaka maisha yaendelee kama kawaida ni mwito wenye nia ovu ya kufunika kombe mwanaharamu apite. Maisha hayapaswi kuendelea kama yalivyokuwa kwa kiwango cha mauaji kilichofanyika na uwepo wa Viongozi Haramu madarakani wasiotokana na kura za kweli za wananchi wengi na walioapishwa kwa matokeo ya uongo bila hatua za haraka za toba na tiba kwa Taifa.

Amri yake ya vyombo vya dola kuchunguza ina nia ovu ya kuficha ukweli na kuhamisha mzigo wa tuhuma za mauaji na kukwepa uwajibikaji. Tayari matokeo ya amri hiyo ni kamata kamata inayoendelea ya viongozi wa Chadema na hatari ya kupika ushahidi. Tayari Makamu Mwenyekiti wa Chadema John Heche aliyekuwa mahabusu kabla hata ya uchaguzi kwa tuhuma za makosa ya Uhamiaji yenye dhamana amebadilishiwa makosa na sasa anatuhumiwa kwa ugaidi. Amri hiyo imekuwa na itakuwa na athari mbaya zaidi kwa walioko mahabusu za polisi kabla, wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu 2025.

Vyombo vya dola havipaswi kuachiwa kujichunguza kwa kuwa ni watuhumiwa wakuu wa vitendo vya utekaji vya kabla ya uchaguzi na mauaji ya wakati na baada ya uchaguzi. Hivyo, Wananchi na wadau tuungane kutaka hatua tatu za pamoja na sambamba:
1. Kuundwa kwa Tume ya Ukweli, Haki na Upatanishi kwa mapendekezo kutoka Taasisi za kitaifa za dini, za kiraia na kisiasa zenye kuaminika.
2. Tume ya Kijaji ya Uchunguzi na 3. Kuja kwa Vyombo vya Kimataifa vya Uchunguzi vya Umoja wa Mataifa (UN) na Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC) kama nilivyotoa mwito kupitia taarifa kwa umma ya tarehe 2 Novemba 2025.

Rais Haramu hana uhalali kutoa onyo kwa wanaotuhumiwa kufanya vurugu bila yeye mwenyewe kwanza kujipa onyo kwa mipango yake na ya vyombo vyake kabla, wakati na baada ya uchaguzi iliyosababisha vurugu za vyombo vya dola na vikundi vingine haramu dhidi ya wananchi waliopanga kufurahia haki na uhuru wao wa kuandamana kwa amani na raia wengine waliouwawa ambao hawakuwa wanashiriki maandamano. Adhabu ya kutuhumiwa kuvunja sheria haikupaswa kuwa kuuliwa kwa risasi: hizi ni vurugu za dola zinazohitaji wahusika katika vyombo vya dola kuchukuliwa hatua. Ni nani wa kumuonya na kumchukulia hatua yeye aliyekuwa Amiri Jeshi Mkuu wa vyombo hivyo wakati wote wa vurugu hizo na mauaji hayo?

Juu ya kauli tupu ya Rais Haramu ya kutaka mazungumzo ni vyema akakumbuka na umma ukakumbuka kuwa Chadema wakati wote imekuwa tayari kwa mazungumzo. Ndio maana tuliomba mazungumzo 2019 na aliyekuwa Rais Magufuli baada ya uporaji wa uchaguzi wa Mitaa, Vijiji na Vitongoji 2019 tukapuuzwa. Tuliomba tena mazungumzo na Rais Samia 2021 mara baada ya Mwenyezi Mungu kufungua Ukurasa Mpya kwa Nchi yetu na tukakubali kushiriki mazungumzo 2022 na 2023. Hata hivyo ni Rais Samia, na Serikali yake na Chama chake ndio walikwamisha mazungumzo wakati huo kwa kukataa mapendekezo yote ya kukwamua na kukamilisha mchakato wa katiba mpya na pia kukataa mapendekezo yote ya marekebisho ya katiba na marekebisho ya maana ya sheria na kitaasisi kuwezesha chaguzi za 2024 na 2025 kuwa huru na haki.

Iwapo kauli ya sasa ya Rais Haramu sio ya kinafiki basi itanguliwe na na toba na tiba ya sasa ya mazungumzo ihusishe pia wasuluhishi na usuluhishi wa haraka kwa kuwa Taifa liko katika mgogoro mkubwa. Mazungumzo ya sasa yatengeneze mazingira ya dharura ya pamoja na mambo mengine kuwezesha kufanyika kwa uchaguzi huru na haki. Chadema tuko tayari kwa mazungumzo ya kweli, huru na ya haki kwa kuwa kwa mujibu wa Katiba ya Chadema ibara ya 3.2 katika itikadi yake ya mrengo wa kati Chadema inaamini katika siasa zilizo juu ya Vyama zenye kuzingatia zaidi maslahi ya Taifa. Katika mazungumzo hayo uhusika wa umma ama moja kwa moja au kupitia wawakilishi wenye kuaminika na kukubalika upewe kipaumbele tukirejea falsafa yetu ya people's power (Nguvu ya Umma).

Kitendo cha Rais Haramu kunukuu kipande cha hotuba ya Hayati Rais Mkapa ya mwaka 2000 ya kukataa kutekeleza maagizo ya waangalizi wa kimataifa wa Uchaguzi haramu uliosababisha mauaji Zanzibar 2001 kunaashiria kuwa hayuko tayari kutekeleza mapendekezo yaliyotolewa na waangalizi wa kimataifa ambao wamekwisha tangaza kupitia taarifa zao za awali kuwa unaoitwa uchaguzi mkuu wa 2025 Tanzania haukuwa huru wala wa haki.

Rais Haramu alipaswa kuzingatia kuwa Rais Mkapa katika kitabu cha maisha yake alichoandika kabla ya kufariki kwake alijutia matendo yake na ya Serikali yake mintaarafu uchaguzi wa Zanzibar wa 2000 hivyo hakupaswa kuitumia hotuba yake kama rejea kuhalalisha udhalimu wa mwaka 2025.

Hotuba yake hii ya kwanza haijaonyesha majuto wala unyenyekevu wa kustahili kujiita kuwa ni "Mtumishi Mkuu wa Maendeleo Endelevu" bali inamfanya apate tuhuma mbele ya umma ya kuwa "Mhusika Mkuu wa ama Mauaji Endelevu au Matendo Maovu Endelevu". Kazi na utu haipaswi kuwa kazi ya uuaji. Hotuba yake haijazingatia misingi aliyoitaja ya kutaka tuwe na taifa lenye umoja, upendo na amani. Ni jambo la kushangaza na kusikitisha kwamba hakutaja kabisa msingi mkuu wa haki ambao ni wa lazima kwa taifa kuwa na upendo, utu, umoja, matumaini, furaha na amani.

Rais Haramu ametoa tafsiri potofu kuwa Demokrasia sio uchaguzi bali matendo ya baada ya uchaguzi. Umma ni vyema uzingatie kuwa Demokrasia ikiwa ni utawala unaoundwa na watu kwa ajili ya watu ni vyote viwili- nani wamechaguliwa na wanatawala namna gani. Hivyo jaribio lolote la kuwaghilibu na kuwarubuni Wananchi kusahau uwepo wa utawala Haramu madarakani linapawa kupuuzwa na wapenda haki, demokrasia, mabadiliko, uhuru, ukweli na uadilifu ndani ya nchi yetu na katika Jumuiya ya Kimataifa. Hatua ya kuponya inapaswa kutanguliwa na kutambua kuwa kuna ugonjwa.

Nakubaliana naye kuwa Tanzania ni kubwa kuliko mtu. Hivyo, Serikali iliyopo (kwa maana ya utumishi halali na wa haki wa umma wenye ueledi na Maadili) , Viongozi wa Dini wenye Roho ya Ucha Mungu, vyama vya siasa vyenye kuheshimu sauti za watu, Jumuiya Huru zisiingie kwenye mtego na kumtetea Rais Haramu na Viongozi wengine haramu kwa kuwafanya kuwa wakubwa kuliko Tanzania.

Badala yake waendelee kuheshimu sauti za watu na nguvu ya umma inayotaka Reforms, Reconciliation na Rebuilding kupitia Katiba Mpya na uwepo madarakani viongozi wa kuchaguliwa na Wananchi kupitia kufanyika kwa uchaguzi huru na haki kwa haraka.

Ni udhalimu na kinyume na utu kwa Rais Haramu kuanzia hotuba yake bila walau kutaka watu kusimama dakika moja kwa heshima kwa maafa ya Mauaji yaliyotokana na uchafuzi wake; lakini ni udhalimu zaidi na uovu kumaliza hotuba yake bila kutangaza maombolezo ya Kitaifa na kuagiza bendera kupepea nusu mlingoti sanjari na kuagiza misaada ya mazishi kutolewa kwa familia za waliouwawa kuwawezesha kusitiriwa kwa haraka.

Narejea kuwaomba tuendelee na maombolezo tukiweka kumbukumbu za wafia haki, uhuru na demokrasia wote wa matukio na matokeo ya tarehe 29 Oktoba mpaka sasa.

Katika kipindi hiki ambacho bado pia Chadema tunazuiwa kukusanyika na kufanya vikao kutokana na zuio ovu la tarehe 10 Juni 2025.

Nihitimishe ujumbe huu kuendelea kutaka na kusisitiza:

Mosi, Waliouwawa wapewe mazishi yenye heshima, kumbukumbu zao zihifadhiwe na familia zao zilipwe fidia.

Pili, Vyombo huru vya Uchunguzi vya Kimataifa vije kuchunguza udhalimu iliofanyika kabla, wakati na baada ya uchaguzi.

Tatu, hakuna uchaguzi halali iliofanyika Tanzania tarehe 29 Oktoba 2025 hivyo matokeo yaliyotangazwa tarehe 1 Novemba 2025 ni batili na haramu.

Nne, Mwenyekiti Tundu Lissu, Makamu Mwenyekiti John Heche, viongozi wengine na wananchi waliofanywa mahabusu na wafungwa wa kisiasa kufuatia msimamo wa Chadema na wa umma wa No Reforms No Election waachiwe huru bila masharti yoyote.

Tano, Taasisi ya Chadema iliyo kwenye kifungo cha kisiasa kwa kuzuiwa kutumia rasilimali zake na kufanya shughuli za kisiasa tangu tarehe 10 Juni 2025 iachiliwe huru kwa maombi yenye nia ovu kufutwa ili kutuwezesha kutumia haki zake na zetu za kikatiba na kutimiza majukumu yake na yetu kwa taifa kwa Taifa katika wakati huu muhimu kwa mustakabali mwema wa nchi yetu.

Haki huinua Taifa (Mithali 14:34) na haki na amani vinabusiana (Zaburi 85:10) wenye kutoa hukumu dhidi yetu na dhidi ya wengine watoe hukumu kwa haki (Quran 4:58) na Haki ifanywe kipaumbele (Quran 16:90) tudumishe Tanzania ya uhuru na umoja na zaidi tujenge Tanzania mpya yenye haki na furaha ambavyo ni vilele vya amani ya kweli.

John Mnyika
Katibu Mkuu
05/11/2025
 
Rais Haramu aliyejaa ulaghai. Hakuna jambo lolote analoaminiwa juu yake, uongo kwake ni desturi.

. Hata Mungu anayetaka watu waamini anafuata mafundisho yake kwake anafikiri anaweza kumhadaa!

Hatuwezi kuwa na taifa lenye misingi hiyo ya maisha.
 
Ujumbe wa Katibu Mkuu Na. 3 wa 2025: Juu ya Hotuba ya Rais Haramu ya 3/11/2025 na maombolezo ya wafia demokrasia, uhuru na haki ya tarehe 5 mpaka 11 Novemba 2025.

Haki huinua Taifa (Mithali 14:34) na haki na amani vinabusiana (Zaburi 85:10) wenye kutoa hukumu dhidi yetu na dhidi ya wengine watoe hukumu kwa haki (Quran 4:58) na Haki ifanywe kipaumbele (Quran 16:90) tudumishe Tanzania ya uhuru na umoja na zaidi tujenge Tanzania mpya yenye haki na furaha ambavyo ni vilele vya amani ya kweli.

John Mnyika
Katibu Mkuu
05/11/2025
Haramu, isiyo halali na halali ni hoja za kisheria, sio kila kisicho halali ni haramu, kuna vitu sio halali lakini sio haramu. Na ili haramu iwe ni haramu kweli, ni haiwi haramu mpaka kwanza iharimishwe, haramu isipo harimishwa huhesabika ni halali.
Na haramu iki halalishwa inageuka kuwa ni halali japo sio haki.

Halali ni legal, haramu ni void isiyo halali ni voidable.

Ni kweli uchaguzi mkuu wetu haukuwa haramu, bali ulikuwa sio halali, voidable. Tume Huru ya Uchaguzi pia sio tume haramu ya uchaguzi, ni tume isiyo halali ya uchaguzi.

Kitendo cha INEC kumtangaza Rais Samia ndie ameshinda uchaguzi kinamfanya Rais Samia kuwa mshindi halali hata kama uchaguzi sio halali na tume ya uchaguzi INEC sio halali

Tangazo la INEC kumtangaza mshindi, limehalisha haramu yote iliyofanyika kwa kanuni ya the end justify the means.

Na japo uchaguzi mkuu haukuwa halali, huru na wa haki, laikini haukuwa haramu na tume ya uchaguzi INEC pia sio halali lakini sio haramu, lakini kwa mujibu wa Katiba yetu ya JMT, tangazo la mshindi wa urais akiisha tangazwa na tume, mshindi huyo anakuwa ni rais mteule halali aliyehalalishwa na tume isiyo halali ila sio haramu.

Mahakama ni mamlaka halali, mshindi akiisha apishwa na mamlaka halali, Jaji Mkuu wa Tanzania, ule ukosefu wa uhalali unakuwa umebatilishika, hivyo anakuwa ni rais halali wa Tanzania.

Hili la Chadema kutoyatambua matokeo, na kutomtambua rais hayakuanza leo, uchaguzi wa 2010 pia mlijidai kutomtambua hatimaye Thread 'CHADEMA yakubali yaishe! yamtambua Rais, yampongeza Rais' CHADEMA yakubali yaishe! yamtambua Rais, yampongeza Rais

Na baadaye tukawashuhudia mkitinga Ikulu na kufakamia juice na misosi huku na broad smiles na vicheko meno 32 nje! Thread 'Kikao Cha Kikwete na Wapinzani, Kinastahili Pongezi? Au Kubezwa?!-"Ukimya Dawa! (Silence is Golden!)' Kikao Cha Kikwete na Wapinzani, Kinastahili Pongezi? Au Kubezwa?!-"Ukimya Dawa! (Silence is Golden!)

Uchaguzi Mkuu wa 2025 pia mkatangaza kutoyatambua matokeo na kutomtambua rais,
Nikawashauri Thread 'ENL, CHADEMA na UKAWA, Tuyakubali Matokeo!, Tushukuru Kwa Yote!, Life Goes On!.' ENL, CHADEMA na UKAWA, Tuyakubali Matokeo!, Tushukuru Kwa Yote!, Life Goes On!.

Mkagoma na kutoa tamko
Thread 'Tamko la Edward Lowassa Baada ya NEC Kumtangaza Dr Magufuli Kuwa Mshindi wa Kiti cha Urais' GE2015 - Tamko la Edward Lowassa Baada ya NEC Kumtangaza Dr Magufuli Kuwa Mshindi wa Kiti cha Urais
Baada ya tamko nikawashauri Thread 'Ushauri wa Bure kwa Lowassa: Hata kama ni kweli uliibiwa kura; Kaa kimya, Mungu ndiye akupiganie!' Ushauri wa Bure kwa Lowassa: Hata kama ni kweli uliibiwa kura; Kaa kimya, Mungu ndiye akupiganie!

Ila nikawaunga mkono Thread 'Kama hii ni kweli, then Serikali yetu ni dhalimu na haramu? Hukumu ya karma ijuu yake!' GE2015 - Kama hii ni kweli, then Serikali yetu ni dhalimu na haramu? Hukumu ya karma ijuu yake!

Mara tukaona mtu wenu ameitwa Ikulu, alipotoka akadai ameitwa kurubuniwa kurejea nyumbani CCM, kiukweli tulimbalasa sana Blaza humu Thread 'Kama hiki ndicho Lowassa alichoitiwa Ikulu, Then tuna Rais wa ajabu! Kama ni Uongo, Lowassa ashitakiwe kwa Uchochezi!' Kama hiki ndicho Lowassa alichoitiwa Ikulu, Then tuna Rais wa ajabu! Kama ni Uongo, Lowassa ashitakiwe kwa Uchochezi!

Nikamshauri Eddo Thread 'Ushauri wa bure kwa Lowassa, japo it's now just a matter of time kabla... Tafadhali sana tunakuomba kwanza kanusha tamko hili!' Ushauri wa bure kwa Lowassa, japo it's now just a matter of time kabla... Tafadhali sana tunakuomba kwanza kanusha tamko hili!

Eddo anarejea CCM, Chadema mkamtambua JPM maisha wakaendelee.

Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020, mkasusia matokeo na kuuita uchafuzi, mkagoma kumtambua rais na kulitambua Bunge, Nikawashauri Thread 'CHADEMA kubalini matokeo na m-survive, or shupazeni shingo. You go to hell 6ft under Hao Makamanda 19 ni mashujaa, kuendelea Ubunge wao' CHADEMA kubalini matokeo na m-survive, or shupazeni shingo. You go to hell 6ft under Hao Makamanda 19 ni mashujaa, kuendelea Ubunge wao

Hatimaye mlikubali matokeo, mkafanya maridhiano mkautambua uchaguzi, mkamtambua rais, mkalitambua Bunge na Kumtambua Mbunge wenu Aida Khenani.Thread 'J Mnyika, Aunguruma Channel TEN, Athibitisha maridhiano yameisaidia Sana CHADEMA, Sasa Inayatambua Matokeo, Inalitambua Bunge na Kumtambua Mbunge Wake' J Mnyika, Aunguruma Channel TEN, Athibitisha maridhiano yameisaidia Sana CHADEMA, Sasa Inayatambua Matokeo, Inalitambua Bunge na Kumtambua Mbunge Wake

Ushauri
Japo uchaguzi Mkuu huu umesababisha madhara makubwa kwa vifo na uharibifu wa mali, hivyo kugharamiwa kwa gharama ya machozi, jasho na damu za Watanzania hivyo watu wana machungu na hasira, tusichochee moto kwa kunyoosheana vidole, and calling each other names rais haramu au waandamanaji wahalifu, let's start hearing process.

Nakuomba usimuite Rais Samia ni Rais Haramu, hata kama amepatikana kwa uchaguzi Mkuu usio halali, baada ya kuapishwa ni rais halali kama nilivyo shauri

Mungu Ibariki Tanzania

Paskali
 
Nakuomba JJ. Mnyika usimuite Rais Samia ni Rais Haramu, hata kama amepatikana kwa uchaguzi Mkuu usio halali.

Hili la Chadema kutoyatambua matokeo, na kutomtambua rais hayakuanza leo, uchaguzi wa 2010 pia mlijidai kutomtambua hatimaye Thread 'CHADEMA yakubali yaishe! yamtambua Rais, yampongeza Rais' CHADEMA yakubali yaishe! yamtambua Rais, yampongeza Rais

Na baadaye tukawashuhudia mkitinga Ikulu na kufakamia juice na misosi huku na broad smiles na vicheko meno 32 nje! Thread 'Kikao Cha Kikwete na Wapinzani, Kinastahili Pongezi? Au Kubezwa?!-"Ukimya Dawa! (Silence is Golden!)' Kikao Cha Kikwete na Wapinzani, Kinastahili Pongezi? Au Kubezwa?!-"Ukimya Dawa! (Silence is Golden!)

Uchaguzi Mkuu wa 2025 pia mkatangaza kutoyatambua matokeo na kutomtambua rais,
Nikawashauri Thread 'ENL, CHADEMA na UKAWA, Tuyakubali Matokeo!, Tushukuru Kwa Yote!, Life Goes On!.' ENL, CHADEMA na UKAWA, Tuyakubali Matokeo!, Tushukuru Kwa Yote!, Life Goes On!.

Mkagoma na kutoa tamko
Thread 'Tamko la Edward Lowassa Baada ya NEC Kumtangaza Dr Magufuli Kuwa Mshindi wa Kiti cha Urais' GE2015 - Tamko la Edward Lowassa Baada ya NEC Kumtangaza Dr Magufuli Kuwa Mshindi wa Kiti cha Urais

Tena mimi nikawaunga mkono
P
Ipo siku utajutia maneno yako haya na utakosa wa kulia na wewe.
 
Haki huinua Taifa (Mithali 14:34) na haki na amani vinabusiana (ZabuNri 85:10) wenye kutoa hukumu dhidi yetu na dhidi ya wengine watoe hukumu kwa haki (Quran 4:58) na Haki ifanywe kipaumbele (Quran 16:90) tudumishe Tanzania ya uhuru na umoja na zaidi tujenge Tanzania mpya yenye haki na furaha ambavyo ni vilele vya amani ya kweli.

John Mnyika
Katibu Mkuu
05/11/2025
Nikuoingeze

Katibu Mkuu apewe pongezi Kwa uratibu nzuri wa MO29 Mlijua kujipanga
Screenshot_20251028-185522.png
 
Haramu, isiyo halali na halali ni hoja za kisheria, sio kila kisicho halali ni haramu, kuna vitu sio halali lakini sio haramu. Na ili haramu iwe ni haramu kweli, ni haiwi haramu mpaka kwanza iharimishwe, haramu isipo harimishwa huhesabika ni halali.
Na haramu iki halalishwa inageuka kuwa ni halali japo sio haki.

Halali ni legal, haramu ni void isiyo halali ni voidable.

Ni kweli uchaguzi mkuu wetu haukuwa haramu, bali ulikuwa sio halali, voidable. Tume Huru ya Uchaguzi pia sio tume haramu ya uchaguzi, ni tume isiyo halali ya uchaguzi.

Kitendo cha INEC kumtangaza Rais Samia ndie ameshinda uchaguzi kinamfanya Rais Samia kuwa mshindi halali hata kama uchaguzi sio halali na tume ya uchaguzi INEC sio halali

Tangazo la INEC kumtangaza mshindi, limehalisha haramu yote iliyofanyika kwa kanuni ya the end justify the means.

Na japo uchaguzi mkuu haukuwa halali, huru na wa haki, laikini haukuwa haramu na tume ya uchaguzi INEC pia sio halali lakini sio haramu, lakini kwa mujibu wa Katiba yetu ya JMT, tangazo la mshindi wa urais akiisha tangazwa na tume, mshindi huyo anakuwa ni rais mteule halali aliyehalalishwa na tume isiyo halali ila sio haramu.

Mahakama ni mamlaka halali, mshindi akiisha apishwa na mamlaka halali, Jaji Mkuu wa Tanzania, ule ukosefu wa uhalali unakuwa umebatilishika, hivyo anakuwa ni rais halali wa Tanzania.

Hili la Chadema kutoyatambua matokeo, na kutomtambua rais hayakuanza leo, uchaguzi wa 2010 pia mlijidai kutomtambua hatimaye Thread 'CHADEMA yakubali yaishe! yamtambua Rais, yampongeza Rais' CHADEMA yakubali yaishe! yamtambua Rais, yampongeza Rais

Na baadaye tukawashuhudia mkitinga Ikulu na kufakamia juice na misosi huku na broad smiles na vicheko meno 32 nje! Thread 'Kikao Cha Kikwete na Wapinzani, Kinastahili Pongezi? Au Kubezwa?!-"Ukimya Dawa! (Silence is Golden!)' Kikao Cha Kikwete na Wapinzani, Kinastahili Pongezi? Au Kubezwa?!-"Ukimya Dawa! (Silence is Golden!)

Uchaguzi Mkuu wa 2025 pia mkatangaza kutoyatambua matokeo na kutomtambua rais,
Nikawashauri Thread 'ENL, CHADEMA na UKAWA, Tuyakubali Matokeo!, Tushukuru Kwa Yote!, Life Goes On!.' ENL, CHADEMA na UKAWA, Tuyakubali Matokeo!, Tushukuru Kwa Yote!, Life Goes On!.

Mkagoma na kutoa tamko
Thread 'Tamko la Edward Lowassa Baada ya NEC Kumtangaza Dr Magufuli Kuwa Mshindi wa Kiti cha Urais' GE2015 - Tamko la Edward Lowassa Baada ya NEC Kumtangaza Dr Magufuli Kuwa Mshindi wa Kiti cha Urais
Baada ya tamko nikawashauri Thread 'Ushauri wa Bure kwa Lowassa: Hata kama ni kweli uliibiwa kura; Kaa kimya, Mungu ndiye akupiganie!' Ushauri wa Bure kwa Lowassa: Hata kama ni kweli uliibiwa kura; Kaa kimya, Mungu ndiye akupiganie!

Ila nikawaunga mkono Thread 'Kama hii ni kweli, then Serikali yetu ni dhalimu na haramu? Hukumu ya karma ijuu yake!' GE2015 - Kama hii ni kweli, then Serikali yetu ni dhalimu na haramu? Hukumu ya karma ijuu yake!

Mara tukaona mtu wenu ameitwa Ikulu, alipotoka akadai ameitwa kurubuniwa kurejea nyumbani CCM, kiukweli tulimbalasa sana Blaza humu Thread 'Kama hiki ndicho Lowassa alichoitiwa Ikulu, Then tuna Rais wa ajabu! Kama ni Uongo, Lowassa ashitakiwe kwa Uchochezi!' Kama hiki ndicho Lowassa alichoitiwa Ikulu, Then tuna Rais wa ajabu! Kama ni Uongo, Lowassa ashitakiwe kwa Uchochezi!

Nikamshauri Eddo Thread 'Ushauri wa bure kwa Lowassa, japo it's now just a matter of time kabla... Tafadhali sana tunakuomba kwanza kanusha tamko hili!' Ushauri wa bure kwa Lowassa, japo it's now just a matter of time kabla... Tafadhali sana tunakuomba kwanza kanusha tamko hili!

Eddo anarejea CCM, Chadema mkamtambua JPM maisha wakaendelee.

Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020, mkasusia matokeo na kuuita uchafuzi, mkagoma kumtambua rais na kulitambua Bunge, Nikawashauri Thread 'CHADEMA kubalini matokeo na m-survive, or shupazeni shingo. You go to hell 6ft under Hao Makamanda 19 ni mashujaa, kuendelea Ubunge wao' CHADEMA kubalini matokeo na m-survive, or shupazeni shingo. You go to hell 6ft under Hao Makamanda 19 ni mashujaa, kuendelea Ubunge wao

Hatimaye mlikubali matokeo, mkafanya maridhiano mkautambua uchaguzi, mkamtambua rais, mkalitambua Bunge na Kumtambua Mbunge wenu Aida Khenani.Thread 'J Mnyika, Aunguruma Channel TEN, Athibitisha maridhiano yameisaidia Sana CHADEMA, Sasa Inayatambua Matokeo, Inalitambua Bunge na Kumtambua Mbunge Wake' J Mnyika, Aunguruma Channel TEN, Athibitisha maridhiano yameisaidia Sana CHADEMA, Sasa Inayatambua Matokeo, Inalitambua Bunge na Kumtambua Mbunge Wake

Ushauri
Japo uchaguzi Mkuu huu umesababisha madhara makubwa kwa vifo na uharibifu wa mali, hivyo kugharamiwa kwa gharama ya machozi, jasho na damu za Watanzania hivyo watu wana machungu na hasira, tusichochee moto kwa kunyoosheana vidole, and calling each other names rais haramu au waandamanaji wahalifu, let's start hearing process.

Nakuomba usimuite Rais Samia ni Rais Haramu, hata kama amepatikana kwa uchaguzi Mkuu usio halali, baada ya kuapishwa ni rais halali kama nilivyo shauri

Mungu Ibariki Tanzania

Paskali
Ngonjera ndefu but zero content.

Huwezi kuwa na uchaguzi usio halali halafu ukasema aliyetangazwa mshindi wa uchaguzi usio halali, eti ni halali, labda uwe huna akii kabisa!!
 
Sheria, halali, batili, isiyo halali,haramu na haki ni vitu tofauti na vyote ni vya kisheria.

Kitu ambacho sio halali kinaweza kuhalalishwa

Mfano mzuri ni mfano wa ndoa, kuna ndoa halali, ndoa batili na ndoa batilifu,

Ili ndoa iwe halali, kwanza ni muungano wa hiyari, consent kuna ndoa nyingi hazina consent lakini ni ndoa halali.

Ndoa inahalalishwa kwa tendo la consummation, ndoa inaweza kufungwa kihalali, lakini bila kufanyika tendo la consummation, ndo hiyo inakuwa batilifu mpaka tendo litakapo fanyika, na likishindwa kabisa kufanyika ndoa hiyo inakuwa ni ndoa batili.

Kwa vile ndoa imeishafungwa, ili kuijua kama ni halali, batili au batilifu, lazima mwana ndoa mmoja aseme, asiposema inaonekana ni ndoa halali kumbe ni just a mare sham

Ubakaji ni kosa la jinai, ukimbaka mwanamke asiposema kabakwa, atahesabika ame consent, akipata ujauzito hana pa kwenda. kaja kwako ukampokea mkaishi kinyumba kwa zaidi ya miezi 6, atahesabika ni mkeo halali.

Vivyo hivyo ushindi wa kishindo wa CCM ni ushindi batilifu wa kubaka demokrasia, kule kutangazwa na INEC kuwa Samia ameshinda huko ni tangazo la ndoa na kuapishwa ni kufunga ndoa na consummation hivyo rais Samia ni rais halali kabisa kisheria ila sio wa haki kwasababu uchaguzi mkuu wetu haukuwa huru na wa haki.

P
 
Haramu, isiyo halali na halali ni hoja za kisheria, sio kila kisicho halali ni haramu, kuna vitu sio halali lakini sio haramu. Na ili haramu iwe ni haramu kweli, ni haiwi haramu mpaka kwanza iharimishwe, haramu isipo harimishwa huhesabika ni halali.
Na haramu iki halalishwa inageuka kuwa ni halali japo sio haki.

Halali ni legal, haramu ni void isiyo halali ni voidable.

Ni kweli uchaguzi mkuu wetu haukuwa haramu, bali ulikuwa sio halali, voidable. Tume Huru ya Uchaguzi pia sio tume haramu ya uchaguzi, ni tume isiyo halali ya uchaguzi.

Kitendo cha INEC kumtangaza Rais Samia ndie ameshinda uchaguzi kinamfanya Rais Samia kuwa mshindi halali hata kama uchaguzi sio halali na tume ya uchaguzi INEC sio halali

Tangazo la INEC kumtangaza mshindi, limehalisha haramu yote iliyofanyika kwa kanuni ya the end justify the means.

Na japo uchaguzi mkuu haukuwa halali, huru na wa haki, laikini haukuwa haramu na tume ya uchaguzi INEC pia sio halali lakini sio haramu, lakini kwa mujibu wa Katiba yetu ya JMT, tangazo la mshindi wa urais akiisha tangazwa na tume, mshindi huyo anakuwa ni rais mteule halali aliyehalalishwa na tume isiyo halali ila sio haramu.

Mahakama ni mamlaka halali, mshindi akiisha apishwa na mamlaka halali, Jaji Mkuu wa Tanzania, ule ukosefu wa uhalali unakuwa umebatilishika, hivyo anakuwa ni rais halali wa Tanzania.

Hili la Chadema kutoyatambua matokeo, na kutomtambua rais hayakuanza leo, uchaguzi wa 2010 pia mlijidai kutomtambua hatimaye Thread 'CHADEMA yakubali yaishe! yamtambua Rais, yampongeza Rais' CHADEMA yakubali yaishe! yamtambua Rais, yampongeza Rais

Na baadaye tukawashuhudia mkitinga Ikulu na kufakamia juice na misosi huku na broad smiles na vicheko meno 32 nje! Thread 'Kikao Cha Kikwete na Wapinzani, Kinastahili Pongezi? Au Kubezwa?!-"Ukimya Dawa! (Silence is Golden!)' Kikao Cha Kikwete na Wapinzani, Kinastahili Pongezi? Au Kubezwa?!-"Ukimya Dawa! (Silence is Golden!)

Uchaguzi Mkuu wa 2025 pia mkatangaza kutoyatambua matokeo na kutomtambua rais,
Nikawashauri Thread 'ENL, CHADEMA na UKAWA, Tuyakubali Matokeo!, Tushukuru Kwa Yote!, Life Goes On!.' ENL, CHADEMA na UKAWA, Tuyakubali Matokeo!, Tushukuru Kwa Yote!, Life Goes On!.

Mkagoma na kutoa tamko
Thread 'Tamko la Edward Lowassa Baada ya NEC Kumtangaza Dr Magufuli Kuwa Mshindi wa Kiti cha Urais' GE2015 - Tamko la Edward Lowassa Baada ya NEC Kumtangaza Dr Magufuli Kuwa Mshindi wa Kiti cha Urais
Baada ya tamko nikawashauri Thread 'Ushauri wa Bure kwa Lowassa: Hata kama ni kweli uliibiwa kura; Kaa kimya, Mungu ndiye akupiganie!' Ushauri wa Bure kwa Lowassa: Hata kama ni kweli uliibiwa kura; Kaa kimya, Mungu ndiye akupiganie!

Ila nikawaunga mkono Thread 'Kama hii ni kweli, then Serikali yetu ni dhalimu na haramu? Hukumu ya karma ijuu yake!' GE2015 - Kama hii ni kweli, then Serikali yetu ni dhalimu na haramu? Hukumu ya karma ijuu yake!

Mara tukaona mtu wenu ameitwa Ikulu, alipotoka akadai ameitwa kurubuniwa kurejea nyumbani CCM, kiukweli tulimbalasa sana Blaza humu Thread 'Kama hiki ndicho Lowassa alichoitiwa Ikulu, Then tuna Rais wa ajabu! Kama ni Uongo, Lowassa ashitakiwe kwa Uchochezi!' Kama hiki ndicho Lowassa alichoitiwa Ikulu, Then tuna Rais wa ajabu! Kama ni Uongo, Lowassa ashitakiwe kwa Uchochezi!

Nikamshauri Eddo Thread 'Ushauri wa bure kwa Lowassa, japo it's now just a matter of time kabla... Tafadhali sana tunakuomba kwanza kanusha tamko hili!' Ushauri wa bure kwa Lowassa, japo it's now just a matter of time kabla... Tafadhali sana tunakuomba kwanza kanusha tamko hili!

Eddo anarejea CCM, Chadema mkamtambua JPM maisha wakaendelee.

Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020, mkasusia matokeo na kuuita uchafuzi, mkagoma kumtambua rais na kulitambua Bunge, Nikawashauri Thread 'CHADEMA kubalini matokeo na m-survive, or shupazeni shingo. You go to hell 6ft under Hao Makamanda 19 ni mashujaa, kuendelea Ubunge wao' CHADEMA kubalini matokeo na m-survive, or shupazeni shingo. You go to hell 6ft under Hao Makamanda 19 ni mashujaa, kuendelea Ubunge wao

Hatimaye mlikubali matokeo, mkafanya maridhiano mkautambua uchaguzi, mkamtambua rais, mkalitambua Bunge na Kumtambua Mbunge wenu Aida Khenani.Thread 'J Mnyika, Aunguruma Channel TEN, Athibitisha maridhiano yameisaidia Sana CHADEMA, Sasa Inayatambua Matokeo, Inalitambua Bunge na Kumtambua Mbunge Wake' J Mnyika, Aunguruma Channel TEN, Athibitisha maridhiano yameisaidia Sana CHADEMA, Sasa Inayatambua Matokeo, Inalitambua Bunge na Kumtambua Mbunge Wake

Ushauri
Japo uchaguzi Mkuu huu umesababisha madhara makubwa kwa vifo na uharibifu wa mali, hivyo kugharamiwa kwa gharama ya machozi, jasho na damu za Watanzania hivyo watu wana machungu na hasira, tusichochee moto kwa kunyoosheana vidole, and calling each other names rais haramu au waandamanaji wahalifu, let's start hearing process.

Nakuomba usimuite Rais Samia ni Rais Haramu, hata kama amepatikana kwa uchaguzi Mkuu usio halali, baada ya kuapishwa ni rais halali kama nilivyo shauri

Mungu Ibariki Tanzania

Paskali
Unajisikiaje hapa wewe mzee mnafiki?
20251106_132648.jpg
 
Ipo siku utajutia maneno yako haya na utakosa wa kulia na wewe.
Wewe Mwl mbona hukutokea kwenye maandamano uliwapigachenga vijana wa watu wengine wakafa na leo wengine wamefikishwa mahakamani kwa uhaini.
 
Back
Top Bottom