Tangazo la king'amuzi cha Continental linanichefua

Tangazo la king'amuzi cha Continental linanichefua

Laiti Watanzania Tungekuwa Nasi Tuna Ujuzi Huu Huu Wa Kuangalia Makosa Ya Wenzetu Haswa Ktk Maisha Yetu Ya Kila Siku Wote Naamini Tungekuwa WATAKATIFU Ila Watanzania Ni Wazuri Sana Kukosoa Makosa Ya Wenzao! Inafurahisha Mno Na Ndiyo Maana Naipenda Tanzania Na Watanzania Pia!

Wakosoaji wote nikiwamo mimi tuko sahihi kukosoa, hata wazungu wanakosoa na sio Watanzania tu, hujasikia watu wanaitwa movie critics kwa wazungu? Tangazo baya sana lile,
 
Wajifunze kwa Vodacom....la ule mtu aliyevaa suti na lile la kwenye TV show,halafu kwenye matangazo sio lazma watu waongee
 
Wakosoaji wote nikiwamo mimi tuko sahihi kukosoa, hata wazungu wanakosoa na sio Watanzania tu, hujasikia watu wanaitwa movie critics kwa wazungu? Tangazo baya sana lile,

Nyie Mlitaka Liweje? Toa Mwongozo Tafadhali.
 
Ila yule dada ana figure matata! Hapo tu ndipo panaponikosha:becky::becky::becky:
 
tangazo ni refu sana kimaudhui sema kwa kutaka lichukue dakika chache walipunguza sana.
pale walimaanisha jamaa kwa kutokuijua continental kagongewa demu na kwa vile wanakaa kotas wakati anaambiwa nilikuwa kwa jirani hakuweza kutambua ni nyumba ipi kwani wakati anaingia alimwona tu mkewe kwani msela alizuga shaa na kurudi ndani.wakati wanazozana msela karudi baada ya kujua jamaa hakubaini kama ni yeye na ku7mpa ushauri ambapo baada ya kuupokea mkewe(macho juu)alitulia nyumbani.
baadhi ya makosa ni kutokuwa na u serious usoni kwa jamaa mwenye mke na ufupicho mkubwa wa story.
 
Kwa lile tangazo la tv mie bado sioni uhusiano wa kifaa au king'amuzi cha continental na maudhui ya tangazo lenyewe.
 
Lile tangazo ni zuri sana, huwa napenda lirudiwe kila saa
 
Pana msemo 'siku njema huonekana asubuhi'. Ki ukweli tangazo la king'amuzi cha 'continental' ni hovyo hovyo kabisa, sijui walioliandaa hawalisikii au vipi? Hebu wajaribu kusikiliza/wajifunze jinsi matangazo ya CRDB yanavovutia. Kwa tangazo hili linanishawishi niamni kuwa hata king'amuzi chenyewe ni kibovu.

Linasemaje mkuu maana ndo nimepata ajira luninga bado sijapata
 
Nakubaliana na wewe mkuu, nadhan labda bajeti ya kufanya tangazo ilikuwa finyu sana ama walitaka tangazo liwe la dakika fupi sana hadi wakaharibu... unajua matangazo yanalipiwa kwa dakika.. ama umakin tu ulikosekana pale....
Ila kiujumla sisi walaji hatujaridhishwa na maandaliz...Hiv Star TV hawapo humu ndan?

Tangazo linahusu king'amuzi chao so suala la gharama si wanamaliza wao kwa wao?
 
Tangazo linahusu king'amuzi chao so suala la gharama si wanamaliza wao kwa wao?
Sawa kabisa. Ni sawa na mifuko ya suruali, kitu kiko mfuko wa upande wa kulia unakihamishia mfuko uliopo upande wa kushoto.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom