Tangazo la kifo cha Benjamin Mkapa, Kurungenzi ya Mawasiliano Ikulu lawamani. Inahitaji kusaidiwa kumsaidia Rais - Jicho Letu Ndani ya Habari

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,498
113,601
Wanabodi,

Naangalia Kipindi cha Jicho Letu Ndani ya Habari, kipindi kinajadili Msiba wa Benjamin Mkapa.



Tangazo la Msiba lililotolewa na Rais Magufuli, Kurungenzi ya Mawasiliano Ikulu imelaumiwa kwa kutokumsaidia rais kikamilifu kutoa tangazo hili, hali inayotafsiriwa kuwa katika baadhi ya matukio, Kurengenzi hiyo inahitaji kusaidiwa na manguli wazoefu ili waweze kumsaidia rais Magufuli katika baadhi ya matukio.

Manguli wa Mwanza, Dotto Bulendu, Edwin Soko na Moses Mathews, wamesema kwa vile hii ni shocking news, kulipaswa kuwepo kwa muda kidogo wa kumuandaa rais Magufuli kutoa tangazo hilo kulitangazia kuanzia, timing, dress code na content za tangazo lenyewe.


Timing
Kwa vile msiba umetokea usiku, kutoa tangazo saa 6:30 usiku was not the right timing kwa Watanzania, news ya msiba ingekuwa held, halafu Wahariri wakaitwa Ikulu usiku ule, halafu Tangazo litolewe live saa 12:00 asubuhi, rais akiwa na VP na PM.
TCRA kutoa taarifa vyombo vyote vya habari vya k electronic kujiunga na TBC ili hiyo live itangazwe Tanzania nzima.

Dress Code.
Kuna mavazi ya kawaida mtu anaweza kuvaa katika tukio lolote, yaani kuvaa casual, lakini kuna matukio lazima uvae, formal dress code, kutangaza msiba wa taifa, dress code should have been formal.

Wabobezi hao wanasema rais Magufuli alipaswa kushauriwa kutoa tangazo hilo akiwa ame dress formal na sio casual dress code ya tangazo hilo.

Contents za Tangazo
Tangazo la msiba wa kiongozi wa kitaifa linaongozwa na sheria ya Vifo vya viongozi, sheria imeweka contents za kisheria ambazo lazima liwe na vitu 6, likianza na National Anthem na kumalizika na National Anthem.
  1. Jina la Kiongozi ni nani
  2. Kifo kimetokea lini
  3. Kifo kimetokea wapi nchini, mkoani, safarini, nje ya nchi
  4. Mahali mahsus, kimetokea nyumba, hospitalini, safarini,
  5. Kama ni hospitalini, hospitali gani
  6. Sababu za kifo, kimesababishwa na nini, maradhi, ajali, usingizini, etc
Tangazo la rais Magufuli kutangaza kifo cha Mkapa, lilikosa, baadhi ya taratibu za tangazo muhimu kama hilo ikiwemo wimbo wa taifa, na taarifa muhimu za kisheria, hivyo kuleta sintofahamu kwa jamii.

Hajawahi kusikika kuwa Benjamin Mkapa anasumbuliwa na maradhi yoyote, hivyo taarifa kuwa amefariki hospitali ni shocking, hospitali gani na ameumwa nini, ni maswali ambayo taarifa ya rais ilikosa.

My Take
Kwa vile taarifa ya msiba ni shocking news, flaws ndogo ndogo katika tangazo la msiba huo, zinavumilika.

Namalizia kwa kutoa pole kwa Rais wa JMT, Dr. John Pombe Magufuli, Familia ya Mkapa na Watanzania kwa ujumla, kwa msiba huu mkubwa wa rais Mstaafu, Benjamin Mkapa.

Paskali

Update
Kumbe sababu ya kifo cha Mkapa ni Cardiac Arrest. Asante sana mwanafamilia William Erio kumaliza sintofahamu hii
Kumbe Sababu ya Kifo cha Mkapa ni Cardiac Arrest. Asante Sana Mwanafamilia William Erio Kumaliza Sintofahamu Hii!.

Kama Tangazo la kifo lingezingatia sheria tangu pale mwanzo, wala kusingetokea sintofahamu yoyote!.

Hivyo japo haijasemwa ni JF, lakini amini usiamini, mabandiko kama haya

Tangazo la kifo cha Benjamin Mkapa, Kurungenzi ya Mawasiliano Ikulu lawamani. Inahitaji kusaidiwa kumsaidia Rais - Jicho Letu Ndani ya Habari

Japo yanalaumiwa kwa kuonekana watu wana mind vitu vidogo vidogo ambayo sio vya msingi, lakini yanasaidia.

Chanzo cha kifo cha ghafla cha any state leader ambaye hajawahi kutamkwa kusumbuliwa na maradhi yoyote, automatically kita send a shock wave kwenda viral.

Baada ya kauli hii, sasa minongo yote kuhusu chanzo cha kifo imemalizwa rasmi.

RIP, Mhe. Rais Mstaafu, Benjamin William Mkapa.

Paskali

Wasaidizi wa Rais, Please Msaidieni Rais Wetu Kwenye Public . Msimuachie Kila Kitu Peke Yake!
 

Attachments

  • The_National_Leaders_Funerals_Act,_2006_(Act_No_sw.pdf
    337.3 KB · Views: 32
Pascal Mayalla,

Mkuu umeeleweka lakini sidhani kama wasaidizi wake hawakuliona hilo mapema (Kumbuka wao ndio walimpa taarifa za msiba).Ila naona umesahau hulka za "Jiwe" labda nikukumbushe tu jaribu kukumbuka ile "press conference" yake mwanzo kabisa baada ya kutangaza baraza lake mawaziri la kwanza mwaka 2015 jinsi "alivyokushushua" na kushindwa kabisa kujibu swali lako vipi ungekuwa wewe ndio msaidizi wake leo. Tushukuru kwa alichokiongea kwani angeweza kuharibu zaidi.
 
Una uhakika hawakupendekeza hayo? Mtu ambaye hapangiwi Cha kufanya unafikiri anashaurika? Kwataarifa yako watendaji wa rais wanatembea na beat ya rais ili wasitumbuliwr. Chamuhimu taarifa umepata inatosha hayo mengine utawaponza wenzio. Au mzee baba mnaitaka nafasi ya msigwa?
 
Hata mm niliona kama hakujiandaa as if ametoka kugegedana chap akaibukia live kutangaza kifo. Proper way ingekuwa SAA 12 ASUBUHI AKIWA SAMBAMBA NA VIONGOZI WAANDAMIZI WENGINE. ILE AMEKAA KWENYE SOFA LAKE LA CHUMBANI HAIKUWA SAWA.

NAUNGA MKONO HOJA.
 
Inawezekana yote hayo alishauriwa ila Jiwe being Jiwe, aliamua kufanya kivyake. Inawezekana aliandaliwa sana na vile alivyoonekana ndio ilikuwa afadhari ya alivyokuwa mwanzo.

Labda waliona watangaze tu haraka kuepuka rumours spreading around kabla ya taarifa official.
 
Back
Top Bottom