Tanganyika inadhalilika: Viko wapi vile vikundi lukuki vilivyoapa kumtetea mama?

Tanganyika inadhalilika: Viko wapi vile vikundi lukuki vilivyoapa kumtetea mama?

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
359,879
Reaction score
828,434
Tunadhalilika duniani
Tunadhalilika mitandaoni
Tunadhalilika Afrika
Tunadhalilika ndani ya jumuiya ya Afrika mashariki mashariki

Hakuna haja ya kurudia chanzo cha haya yote.. Haisaidii tena.. Maana maji yameshamwagika.. Tukitaka kuzoa tutazoa tope

Kazi hiyo ya udhalilishaji inafanywa na makundi mbalimbali hapo nchi jirani ya Kenya yakiongozwa na vijana wao maarufu kama Gen-Z.. Hawafanyi haya kama uchokozi la hasha ipo sababu ya wazi kabisa

Sasa basi kuna vikundi vingi vilibuka hapa bongo vikiongozwa na kile maarufu kama CHAWA WA MAMA! Hivi vilijiapiza kuwa vitakula sahani moja na yeyote yule atakayemzogoa mama kwa lolote like

Ni wiki sasa inaisha Gen-Z kila uchao wanakuja na kituko kipya cha udhalilishaji, matusi, kejeli, kashfa.. Nknk.. Sijaona hata kikundi kimoja kikitoa walau waraka wa sentence moja ya kukemea.. Je vinafurahia haya yanayoendelea?

Hebu tuvitaje vile vikundi vyote hapa.. Tuvitengenezee petition ya kufutwa na kuadhibiwa maana vimeshindwa kazi

Udhalilishaji unaoendelea hauishii kwa mhusika tuu Bali mpaka kwetu sisi tusio na kosa lolote... Wakianza kutukana hawana breki aisee .. Inaumiza sana
downloadfile-1.jpg
 
Chawa wa myamya wamepigwa magoli 10 Kwa zero.angalau tumepata wakutusemea maana tukisema sisi watanzania kuhusu maovu ya hii serikali tunatekwa kama walivyomteka mzee kibao na mdude mchana kweupe mbele ya umati wa watu
 
Na kweli kule Tiktok Rais wetu anadhalilishwa haswa, labda mama samia atoe tamko la kuomba msamaha,kilichowaumiza ni kwamba Wameharibu nchi yao then wanakuja kuharibu Tz kingine ni mateso na deportation ya activists,
 
Angeliamsha tu
Kufanya deportation ya walimu, wapishi, mabaamedi, wenye asili ya kikenya.

Strictly control ya mpaka wa Kenya, na ikiwezekana Ile miezi ikifika fungia sembe isitoke.

Worst case scenario Mkenya akitaka kuja Tanzania walipie visa kwa kiasi Cha dollar 100 maana lishakuwa Taifa korofi kwetu.
 
Back
Top Bottom