Mbeya: Mwanafunzi wa Shule ya Msingi afariki Dunia kwa kujinyonga, yadaiwa chanzo ni kukaripiwa

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,458
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, ACP Benjamin Kuzaga amesema Februari 27, 2023 majira ya saa 02:00 usiku katika Mtaa wa Mwafute uliopo Kata ya Ilemi, Tarafa ya Sisimba, Jijini Mbeya, Mwanafunzi wa darasa la VI katika Shule ya Msingi Lyoto aitwaye IBRAHIM EDSON [12] alikutwa akiwa amefariki baada ya kujinyonga kwa kutumia kamba ya katani chumbani kwake kwenye nyumba ya baba yake.

Mwili wa marehemu ulikutwa juu kwenye kenchi la nyumba hiyo ukiwa umefungwa Kamba.

Chanzo cha tukio hili kinachunguzwa japo uchunguzi wa awali umebaini kuwa ni hasira zilizotokana na kukalipiwa na wazazi/walimu.

Kamanda Kuzaga amesema Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linatoa wito kwa wanafunzi kuacha kujihusisha na mambo mengine ambayo hayahusiani na masomo na badala yake wajikite kwenye masomo.

Amesema “Tunatoa wito kwa wazazi na walezi kujenga tabia ya kuwa karibu na watoto wao kwa kuhakikisha wanafuatilia maendeleo yao ya Shule na kujua changamoto mbalimbali zinazowakabili ili kutafuta suluhisho la haraka kabla ya kutokea madhara makubwa.”

AKAMATWA AKITOROSHA MADINI YA DHAHABU
Aidha, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia BITIAS GUDAGA [31] Mkazi wa Kibaoni Wilayani Chunya kwa tuhuma za kutorosha madini aina ya dhahabu.

Ni kwamba mnamo tarehe 24.02.2023 majira ya saa 12:00 jioni huko katika kizuizi cha Polisi Sangambi Kijiji cha Chalangwa Wilaya Chunya, mtuhumiwa alikamatwa akiwa anatorosha madini aina ya dhahabu yenye uzito wa gramu 22.8 na thamani ya shilingi Milioni mbili na laki mbili [2,200,000/=] akiwa amepakia kwenye gari yenye namba za usajili T.116 DFJ aina ya Toyota Klugger. Mara baada ya upelelezi kukamilika, mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria.
 
Back
Top Bottom