Mwanafunzi darasa la saba ajinyonga kwa kutumia kamba ya chandarua

Mjanja M1

JF-Expert Member
Oct 7, 2018
3,660
12,306
Mwanafunzi wa darasa la saba shule ya msingi Lukobe, Stephen Robert (13) amekutwa amejinyonga nyumbani kwao, kwa kutumia kamba ya chandarua.

Akisimulia tukio baba mzazi wa mtoto huyo, Robert Kirugu ambaye ni dereva wa bodaboda, amesema wakati tukio hilo linatokea yeye alikwenda kwenye shughuli za utafutaji rizki na mama wa mtoto huyo alikwenda jijini Dar es Salaam kutafuta maisha, na kwamba mtoto huyo alikuwa akiishi na watoto wake wengine hapo nyumbani.

"Kabla sijatoka nyumbani kwenda kwenye utafutaji Stephen alinipa taarifa ya kuwepo kwa kikao shuleni kwao hivyo nilimwambia dada yake aende akasikilize kitakachoongelewa kwenye kikao hicho. Ilipofika mchana ndio nikapigiwa simu na kuambiwa Stephen amejinyonga na ameshafariki," ameeleza Kirugu.

Amesema kuwa hadi sasa bado hawajafahamu sababu zilichangia mtoto huyo kujinyonga, na alipokagua begi lake la shule pamoja na madaftari hawajakuta ujumbe wala kitu kitu chochote.

Kirugu amesema kuwa kwa zaidi ya miezi mitatu amekuwa akiishi na watoto wake saba bila ya uwepo wa mama yao na kuhakikisha wanapata mahitaji yote muhimu kama chakula na vifaa vya shule.

"Mimi ni bodaboda lakini pia ni mfanyabiashara, mara zote kabla sijatoka asubuhi nahakikisha nimeacha pesa kwa ajili ya chakula na pia nimekuwa nikifuatilia kwa karibu tabia na mienendo ya watoto wangu pamoja na maendeleo yao ya shule," amesema Kirugu.

Amesema kwa sasa ameliachilia Jeshi la Polisi liendelee na uchunguzi zaidi, hata hivyo taratibu za mazishi zinaendelea na wamepanga kuzika kesho Ijumaa Februari 23 katika makaburi ya Kihonda Youth mission.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Kamishna msaidizi mwandamizi wa Polisi, Alex Mkama amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, akisema kuwa uchunguzi bado unaendelea.

Source - Mwananchi
 
Aulize kwanza kikao shule kilikua kinahusu nini? Isijekua kuna sehemu kazingua, akachukua maamuzi amabyo bado ni ya kipuuzi.
 
Au mzee ni kauzu sana, dogo kafanya msala kaona bora kudedi kuliko mshua ajue.

Tuishi na watoto kama marafiki tutajua vingi vinavyowasibu, sometimes story za watoto huko shule huwa zinafurahisha wakikusimulia na utajua kirahisi mawazo yao, misimamo yao na imani zao juu ya kitu fulani.
 
Back
Top Bottom