Tanga: Mbunge wa Lushoto na Mwenyekiti wa Halmashauri wadaiwa kuwindana kwa Risasi

Pfizer

JF-Expert Member
Mar 25, 2021
304
518
Mbunge wa Lushoto mjini Shaban Shekilindi almaarufu Boznia anahusishwa na tuhuma za kufanya njama ya kumpiga risasi Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya Lushoto Mbaruku Matei.

Kuhusishwa kwa mbunge huyo, kunatokana na kukamatwa vijana wanne waliokuwa waende kutekeleza mpango huo lakini pia mke wa mbunge huyo kukamatwa kisha kuachiwa kwa dhamana.

Kwa mujibu wa mwenyekiti wa halmashauri ya Lushoto, Matei alisema amehudhunishwa mno na tukio hilo na kuvitaka vyombo vya dola kuchukua hatua za kisheria dhidi ya wale wote wanaotajwa katika tukio hilo.

Hata hivyo, Mwenyekiti alisema wamekuwa kwenye mgongano wa kimawazo na Mbunge huyo wa muda mrefu hasa katika mipango ya maendeleo analotaka mbunge wakimpinga analeta nongwa.

Pia alidai kuwa mbunge huyo anamuhisi kuwa anajiandaa kugombea ubunge kwenye jimbo hilo jambo ambalo si kweli.

Kwa mujibu wa Mbaruku ambaye alizungumza kwa njia ya simu juu ya tuhuma hizo alisema, kitendo hicho kimemtia hofu na kuomba vyombo vya dola kuingilia kati kwa ajili ya usalama wake na familia yake.

"Nimesikia taarifa ya namna hiyo Mimi nilikuwa turget, sikushangaa kwasababu huyo mtu tumekuwa tukipishana kwenye mambo mbalimbali ya maendeleo lakini pia ni mambo ya siasa ya kulinda Ubunge," alisema Matei.

Alisema hajatamka mahali popote pale kwamba atagombea Ubunge mwaka 2025 anashangaa Mbunge huyo amepata wapi maneno hayo.

"Mimi sijasema nitagombea Ubunge sijui huo wasiwasi wake ameutoa wapi, hili suala ni jambo baya nafikiri vyombo vya usalama vilivyopokea jambo hili vinapaswa kulishughulikia kwa umakini kabisa na vyombo vinavyohusika kujua ukweli wake

Alipoulizwa na waandishi wa habari juu ya tuhuma hizo, kamanda wa polisi Mkoa wa Tanga Alimachius Mchunguzi alisema "Ni kweli tukio hilo tunalo, tunaendelea na uchunguzi, tutatoa taarifa rasmi tutakapokamilisha uchunguzi wetu wa tukio hili," alisema Kamanda huyo wa polisi.

Kwa upande wake mbunge wa Lushoto alipoulizwa kuhusu tukio hilo alisema ni uongo mtupu na ni habari za kuzusha kuleta taaharuki kwa wapiga kura wake kumtengenezea ajali isiyokuwepo.

Alisema tangu aelezwe Kuhusu uwepo wa tukio hilo amekuwa akiendelea na shughuli zake za kibunge mjini Dodoma bila kukamatwa au kuwekwa ndani.

"Uongo mtupu Mimi nipo Dodoma, sina ninachojua kuhusu hilo ndugu yangu, wametoa Roma's tu hata mimi nashangaa, sasa hivi nipo kwenye kamati tangia juzi wamesema nipo tu, simu zangu zinapatiakana nipo huru hata wapiga kura wangu wananipigia wanauliza Mheshimiwa umekamatwa nawaambia nimekamatwa wapi," alisema Boznia.

Hata hivyo, mbunge huyo hataki kujua habari hizo zimetoka wapi kwasababu anadai watu wa Lushoto wameshazoea kupiga Short hivyo hawezi kuwazuia kwakuwa midomo ni mali yao na hawailipii hata Vat.

"Sasa utawazuia kama wameamua kupepesa midomo yao, naomba unielewe siyo kweli, halipo na nimeshawaambia wapiga kura wangu kwamba hilo suala halipo, sitaki kujua kama ni mambo ya siasa lakini najua mdomo haulipi VAT kama mtu ameamua kuchafua atakuchafua tu, ndiyo maana sitaki kujua nani ameongea wataendelea tu hivyo, mradi mambo yangu yanaenda nawahudumia wananchi wangu na wanajua nipo salama sasa tatizo lipo wapi hapo, nitashughulika na mtu hapo badala ya kuwashughulikia wananchi wangu," alisema.

Hata hivyo, uchunguzi uliofanywa kwa watu waliokuwa karibu na watu wa usalama wilayani Lushoto wanasema vijana hao wanne ambao hadi sasa wanashikiliwa na polisi, walipobanwa walimtaja mbunge huyo kwamba amewatuma waende wakampige risasi Mwenyekiti huyo.

"Habari zipo wazi wale vijana wanasema kabisa wametumwa na mbunge, hata pesa walizoingiziwa kwenye simu zao zimetoka kwenye kibanda cha mbunge," alisema.

Attachments

  • Risasi Tanga 1.aac
    1.4 MB · Views: 2
  • risasi Tanga.aac
    1 MB · Views: 1
Na Mwandishi wetu.

Huu mchezo wa Matei na aliyekuwa DC Kalist bilashaka. Siasa SIHASA
 
Pumbavu kabisa hawa,kabla ya kushirikiana ili kutumia utajiri mkubwa ambao Mwenyezi Mungu kaipa wilaya hii,wao wanapigania matumbo yao na familia zao,ndio maana nchi hii inahitaji push back kubwa itakayowaleta new young graduates kwenye uongozi ili nchi isogee,guy's Lushoto ni Eden ya Tanzania,kuna lodge kule rate yake per nite ni zaidi ya 100,000.00tshs na inakua full booked,inasikitisha mno utajiri wa wilaya hii hauendani na maisha ya wakazi wake hasa vijana,vijana hawa yaani kila siku inaonyesha hakuna matumaini ya maisha bora
 
Kuelekea ktk uchaguzi wa mitaa tutegemee matukio kama haya ya wenyeviti wa mikoa ,wilaya na halmashauri kupishana na wabunge na wakuu wa mikoa KISA NI KUJARIBU KUWEKA WATU WAO KTK CHAGUZI ZA MITAA ili waje kuwasaidia mwakani ktk UCHAGUZI MKUU
 
Pumbavu kabisa hawa,kabla ya kushirikiana ili kutumia utajiri mkubwa ambao Mwenyezi Mungu kaipa wilaya hii,wao wanapigania matumbo yao na familia zao,ndio maana nchi hii inahitaji push back kubwa itakayowaleta new young graduates kwenye uongozi ili nchi isogee,guy's Lushoto ni Eden ya Tanzania,kuna lodge kule rate yake per nite ni zaidi ya 100,000.00tshs na inakua full booked,inasikitisha mno utajiri wa wilaya hii hauendani na maisha ya wakazi wake hasa vijana,vijana hawa yaani kila siku inaonyesha hakuna matumaini ya maisha bora
Lushoto shida ni wananchi wenyewe!
Wanaikumbatia CCM utadhani Luba na maendeleo hakuna. Unafiki umejaa hadi inashangaza

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
 
Yeah mkuu ila kama ni shida nchi nzima ni shida,angalia wilaya hii ilivyojaliwa kila kitu,weather nzuri kabisa,maji safi kabisa,mazingira ya kiasili yaliyo super,hii wilaya ingempata mbunge mwenye uchungu wa maendeleo ingekua mfano wa kuigwa,kwanza jenga ila pass ya kutoka Mombo hadi Mlalo,iwe super then zile look out zote jenga cable cars,watalii wa nje na ndani wangefurika mno Lushoto,na elewa kwa kila watalii 9 umesha create nafasi moja ya kazi,vijana wale wangejiwezesha kufanya maisha yao yawe bora kabisa
 
Na Mwandishi wetu.

Mbunge wa Lushoto mjini Shaban Shekilindi almaarufu Boznia anahusishwa na tuhuma za kufanya njama ya kumpiga risasi Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya Lushoto Mbaruku Matei.

Kuhusishwa kwa mbunge huyo, kunatokana na kukamatwa vijana wanne waliokuwa waende kutekeleza mpango huo lakini pia mke wa mbunge huyo kukamatwa kisha kuachiwa kwa dhamana.

Kwa mujibu wa mwenyekiti wa halmashauri ya Lushoto, Matei alisema amehudhunishwa mno na tukio hilo na kuvitaka vyombo vya dola kuchukua hatua za kisheria dhidi ya wale wote wanaotajwa katika tukio hilo.

Hata hivyo, Mwenyekiti alisema wamekuwa kwenye mgongano wa kimawazo na Mbunge huyo wa muda mrefu hasa katika mipango ya maendeleo analotaka mbunge wakimpinga analeta nongwa.

Pia alidai kuwa mbunge huyo anamuhisi kuwa anajiandaa kugombea ubunge kwenye jimbo hilo jambo ambalo si kweli.

Kwa mujibu wa Mbaruku ambaye alizungumza kwa njia ya simu juu ya tuhuma hizo alisema, kitendo hicho kimemtia hofu na kuomba vyombo vya dola kuingilia kati kwa ajili ya usalama wake na familia yake.

"Nimesikia taarifa ya namna hiyo Mimi nilikuwa turget, sikushangaa kwasababu huyo mtu tumekuwa tukipishana kwenye mambo mbalimbali ya maendeleo lakini pia ni mambo ya siasa ya kulinda Ubunge," alisema Matei.

Alisema hajatamka mahali popote pale kwamba atagombea Ubunge mwaka 2025 anashangaa Mbunge huyo amepata wapi maneno hayo.

"Mimi sijasema nitagombea Ubunge sijui huo wasiwasi wake ameutoa wapi, hili suala ni jambo baya nafikiri vyombo vya usalama vilivyopokea jambo hili vinapaswa kulishughulikia kwa umakini kabisa na vyombo vinavyohusika kujua ukweli wake

Alipoulizwa na waandishi wa habari juu ya tuhuma hizo, kamanda wa polisi Mkoa wa Tanga Alimachius Mchunguzi alisema "Ni kweli tukio hilo tunalo, tunaendelea na uchunguzi, tutatoa taarifa rasmi tutakapokamilisha uchunguzi wetu wa tukio hili," alisema Kamanda huyo wa polisi.

Kwa upande wake mbunge wa Lushoto alipoulizwa kuhusu tukio hilo alisema ni uongo mtupu na ni habari za kuzusha kuleta taaharuki kwa wapiga kura wake kumtengenezea ajali isiyokuwepo.

Alisema tangu aelezwe Kuhusu uwepo wa tukio hilo amekuwa akiendelea na shughuli zake za kibunge mjini Dodoma bila kukamatwa au kuwekwa ndani.

"Uongo mtupu Mimi nipo Dodoma, sina ninachojua kuhusu hilo ndugu yangu, wametoa Roma's tu hata mimi nashangaa, sasa hivi nipo kwenye kamati tangia juzi wamesema nipo tu, simu zangu zinapatiakana nipo huru hata wapiga kura wangu wananipigia wanauliza Mheshimiwa umekamatwa nawaambia nimekamatwa wapi," alisema Boznia.

Hata hivyo, mbunge huyo hataki kujua habari hizo zimetoka wapi kwasababu anadai watu wa Lushoto wameshazoea kupiga Short hivyo hawezi kuwazuia kwakuwa midomo ni mali yao na hawailipii hata Vat.

"Sasa utawazuia kama wameamua kupepesa midomo yao, naomba unielewe siyo kweli, halipo na nimeshawaambia wapiga kura wangu kwamba hilo suala halipo, sitaki kujua kama ni mambo ya siasa lakini najua mdomo haulipi VAT kama mtu ameamua kuchafua atakuchafua tu, ndiyo maana sitaki kujua nani ameongea wataendelea tu hivyo, mradi mambo yangu yanaenda nawahudumia wananchi wangu na wanajua nipo salama sasa tatizo lipo wapi hapo, nitashughulika na mtu hapo badala ya kuwashughulikia wananchi wangu," alisema.

Hata hivyo, uchunguzi uliofanywa kwa watu waliokuwa karibu na watu wa usalama wilayani Lushoto wanasema vijana hao wanne ambao hadi sasa wanashikiliwa na polisi, walipobanwa walimtaja mbunge huyo kwamba amewatuma waende wakampige risasi Mwenyekiti huyo.

"Habari zipo wazi wale vijana wanasema kabisa wametumwa na mbunge, hata pesa walizoingiziwa kwenye simu zao zimetoka kwenye kibanda cha mbunge," alisema.
Haya ni madogo.
Nilishasema hapo awali kwamba kauli zao zimeshazimwa na sasa hata matendo yao yanawaumbua.

Ni suala la muda tu. Wenye akili na uwezo wanavyoendelea kukaa kimya na kujiweka kando, basi asili itabeba kilicho chake
 
Back
Top Bottom