Mkuu wa Wilaya ya Ulanga na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Lushoto washtakiwa kwa Ukiukwaji wa Maadili

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,120
Hatua hiyo inafuatia Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kupokea Malalamiko ya Ukiukwaji wa Maadili dhidi ya Julius Kenneth Ningu (Mkuu wa Wilaya ya Ulanga - #Morogoro) na Mathew P. Mbaruku (Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto - #Tanga)

Viongozi hao watajadiliwa Septemba 5 hadi 6, 2023 Jijini #Dodoma kwenye Ofisi ya Mkuu wa Mkoa katika Kikao cha Baraza la Maadili kitakachofanya Uchunguzi kuhusu Malalamiko yaliyotolewa juu yao

Kwa mujibu wa Taarifa ya Sekretarieti, uchunguzi utafanyika kwa uwazi kwa mujibu wa Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma ambapo Wananchi wanaalikwa kuhudhuria katika kikao hicho.

---
Mkuu wa Wilaya ya Ulanga mkoani Morogoro, Dkt. Julius Ningu ameshitakiwa katika Baraza la Maadili kwa tuhunma za kutoa lugha za matusi, vitisho na kuwaweka mahabusu watumishi wa umma.

Kikao hicho kimeketi chini ya mwenyekiti wa baraza hilo, Jaji Mstaafu Rose Teemba huku upande wa mlalamikaji ukiwakilishwa na Wakili wa Serikali, Emma Gelani ambaye amedai kiongozi huyo alitenda kosa hilo akiwa Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma katika ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo na kuwaweka rumande baadhi ya watumishi akiwemo mtendaji wa Kata ya Rwinga, Mario Fabian.

Kwa mujibu wa Wakili huyo, sheria inamtaka mkuu wa mkoa, au mkuu wa wilaya kutoa maelezo kwa njia ya maandishi kwa Jeshi la Polisi kabla au muda mfupi baada ya kuamuru kuwekwa ndani na kutoa sababu za msingi za kumuweka mahabusi mtuhumiwa.

“Dkt. Ningu hakutoa maelezo yoyote kwa Jeshi la Polisi kuhusiana na kukamatwa watumishi wa halmashauri na mafundi waliokuwa wanatekeleza miradi ya UVIKO-19 katika Wilaya ya Namtumbo, kinyume cha maelekezo ya sheria," amesema wakili.

Kwa upande wa mlalamikiwa amekana kutumia lugha hizo, na kwamba uamuzi wa kuwaweka rumande ulitokana na ushauri wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya na si uamuzi wake peke yake.

Baada ya baraza hilo kusikiliza pande zote mbili, mwenyekiti wa baraza amesema watakaa kujadili kwa kina na kisha watatoa taarifa kuhusu uamuzi utakaoamuliwa.
 
Mkuu wa Wilaya ya Ulanga na Mwenyekiti wa Wilaya ya Lushoto.

Wanaenda kujadiliwa mkoani Dodoma, kwenye Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Dodoma.

Hawa Wananchi wanaoalikwa kushiriki haya Majadiliano; wale wa Ulanga na Lushoto wanaohusika na hawa Viongozi wataweza kushiriki kweli?
 
Ndio mjipange vizur maana mama amesema anataka uchaguz ujao uwe wa uwazi na haki..
 
Mkuu wa Wilaya ya Ulanga mkoani Morogoro, Dkt. Julius Ningu ameshitakiwa katika Baraza la Maadili kwa tuhuma za kutoa lugha za matusi, vitisho na kuwaweka mahabusu watumishi wa umma.

Kikao hicho kimeketi chini ya mwenyekiti wa baraza hilo, Jaji Mstaafu Rose Teemba huku upande wa mlalamikaji ukiwakilishwa na Wakili wa Serikali, Emma Gelani ambaye amedai kiongozi huyo ailitenda kosa hilo akiwa Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma katika ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo na kuwaweka rumande baadhi ya watumishi akiwemo mtendaji wa Kata ya Rwinga, Mario Fabian.

Kwa mujibu wa Wakili huyo, sheria inamtaka mkuu wa mkoa, au mkuu wa wilaya kutoa maelezo kwa njia ya maandishi kwa Jeshi la Polisi kabla au muda mfupi baada ya kuamuru kuwekwa ndani na kutoa sababu za msingi za kumuweka mahabusi mtuhumiwa.

“Dkt. Ningu hakutoa maelezo yoyote kwa Jeshi la Polisi kuhusiana na kukamatwa watumishi wa halmashauri na mafundi waliokuwa wanatekeleza miradi ya UVIKO-19 katika Wilaya ya Namtumbo, kinyume cha maelekezo ya sheria,” amesema wakili.

Kwa upande wa mlalamikiwa amekana kutumia lugha hizo, na kwamba uamuzi wa kuwaweka rumande ulitokana na ushauri wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya na si uamuzi wake peke yake.

Baada ya baraza hilo kusikiliza pande zote mbili, mwenyekiti wa baraza amesema watakaa kujadili kwa kina na kisha watatoa taarifa kuhusu uamuzi utakaoamuliwa


Source: Swahili
 
Cheo chenyewe ni cha kuteuliwa! Kimepitwa na wakati! Maana ni kati ya vyeo ambavyo tulivikataa kwenye ile Rasimu ya Katiba ya Jaji Warioba!!

Halafu kuna watu eti wanapata kabisa ujasiri wa kuwanyanyasa watumishi wa umma na wananchi wengine katika hii nchi!
 
hutu tu vyeo twa kupewa hua tunawapa watu kiburi aise.

yaani ni weka ndani tu
 
Back
Top Bottom