mjingamimi
JF-Expert Member
- Aug 3, 2015
- 39,286
- 44,842
Software kukodisha dola milioni 30?
kwa kuwa hakuna aliyenipeleka shule kujua hesabu acha nikae kimya
kwa kuwa hakuna aliyenipeleka shule kujua hesabu acha nikae kimya
Mkuu uwe unasoma nakuelewa basi unaambiwa $ wewe unatamka milion 30 kama shilingi! Upo meza kuu niniTAtizo la mtoa Uzi ni mshamba, mill 30 kwa software ni ya kawaida kwa kampuni kubwa kama TANESCO
Mmezoea kutumia software za uwizi unafikiri kampuni kubwa kama TANESCO nao watatumia hapana
Huyu Makamba ana tatizo la kurithi nadhani, hii ndoto yake ya urais italiumiza sana hili taifa.
si bora wangenunuaWizi mtupu.
Unatumia billion 65 kununua software huku vijiji 2000 havijapata umeme.
At Some pointWatanzania naona tulisahau kabisa ajenda ya ufisadi wakati wa Magufuli, mpaka sasa kuna ufisadi umefanyika fasta fasta bila ya watu hata kushtuka.
Mkataba uliosainiwa baina ya Serikali ya Tanzania (kupitia TANESCO) na kampuni ya Tech Mahindra ya India wenye thamani ya dola milioni 30 ni wa kukodisha software ya Enterprise Resources Planning (ERP) - ambayo wahindi hawa wenyewe wanaiita Corporate Management System (CMS), kama inavyosomeka kwenye bango pichani chini.
Software ya aina hii huwa inaunganisha vitengo vyote vya taasisi katika software moja kwa ajili ya urahisi wa kuendesha taasisi. Hivyo basi kwa lugha nyingine ni kwamba Wahindi hawa watafunguliwa milango ya kuingia kila mahali ndani ya TANESCO, na hivyo kuwa na siri zote za mfumo wetu wa umeme.
Jambo kama hili ni hatari sana kwa usalama wa taifa. Hakuna njia rahisi ya kuiangusha nchi bila ya kufyatua hata kombora moja kama kuangusha mfumo wa nchi wa umeme.
Software kama hizi serikali inatakiwa iwawezeshe wataalam wa ndani kupitia Mamlaka ya Serikali Mtandao kutengeneza, kama vile mfumo wa malipo serikalini ulivyotengenezwa na wataalam wetu wa ndani kwa kuwezeshwa na serikali.
Zabuni ya kukodisha software hii ilianzaga kwenye dakika za lala salama za utawala wa Kikwete. Hivyo basi kitendo cha zabuni hii kukaa benchi kwa miaka mitano ya Magufuli kinaonesha kuwa hakuwa amekubaliana nayo. Baada ya Magufuli kufa naona wadau wa zabuni hii wameiendeleza na kuimwagia wino fasta, kama wanavyotaka kufanya kuhusu bandari ya Bagamoyo.
Kwa nini haikua developed?Huo mkataba unanuka ufisadi.
Hiyo software ingeweza kuwa developed humuhumu nchini na kuleta ajira kwa watu wetu.
Kitu walichokifanya TANESCO ni kucreate ajira kwa wahindi badala ya watu wetu
Wangelipa shilingi ngapi?Yaani ndiyo walipe BILIONI 65 kwa ajili ERP software? we jinga kabisa
Julius nchi ilimshinda,kila siku ikawa kumsema mwinyiUtawala huu unanikumbusha utawala ya Mzee Mwinyi na Mama Sitti, mpaka Julius aliingilia kati. Expect more from this Lady
Jamani nchi yetu na Wahindi ! Jumamosi iliyopita nilisafiri na treni kutoka Dar mpaka Arusha. Tulipoondoka Dar nilikuwa naongea na staff mmoja fundi wa TRC nae alikuwa anasafiri tulipopita pale Ilala yard akanionyesha akasema mle ndani ya workshop kuna vile vichwa vya treni 12 vilvyoibuliwa na JPM pale bandarini kutoka India ambapo mwenye mali hajajitokeza mpaka leo na vichwa vimeegeshwa tu. Tunaambiwa ile ni dili ya viongozi wawili mmoja alishaondoka zake sijui kama serikali ililipia hivyo vichwa au la. Ninachosema hapa wahindi kwa magendo!!!!! hongereni na kukodisha software kumbe ile juhudi ya Kalemani kumalizia vijiji vyote kupata umeme ilikuwa inazuia dili za watu.....Hili tatizo linaanzia kule juu kabisa, unapokuwa na kiongozi asietaka kushughulisha akili yake kwa chochote zaidi ya kusubiri kuletewa taarifa na wasaidizi wake huyo ndie chanzo.
Wasaidizi wake wanaweza kumpelekea mawazo ya hovyo yenye malengo ya "kutupiga", na kwasababu kiongozi mwenyewe hawezi kuhoji chochote anayakubali tu mawazo hayo kutokana na namna pumba anazolishwa zitakavyokuwa zimepangiliwa.
Matokeo yake ndio haya, unaona habari ya kukodi software ya $ 30 milion, baada ya kutoka kule kwenye mradi wa LNG ambao nao naamini alipigwa sound akaukubali bila kujua chochote, wala asijue hao anaowatuma ndio wajanja wenyewe, anachofanya Rais ni sawa na kumkabidhi fisi bucha sasa tunavuna tulichopanda.
Hawataweza Kuueleza Umma Isipokuwa UpigajiHiyo ERP ina features gani special kushinda nyingine, wanatakiwa watueleze
Watu Hawawezi Kuacha MagendoNi hatari siyo kitoto
Wanipe mimi laki 5 niwaundie hiyo software
Dollar million 30 ndogo?TAtizo la mtoa Uzi ni mshamba, mill 30 kwa software ni ya kawaida kwa kampuni kubwa kama TANESCO
Mmezoea kutumia software za uwizi unafikiri kampuni kubwa kama TANESCO nao watatumia hapana
Acha kuropoka ropoka kama zwazwa, kama anapotosha wewe siusema ukweli ni nini.Huyo mto mada ndo mpotoshaji