TANESCO wataweza kuendesha Mradi wa kuzalisha umeme wa Rufiji kwa faida au tutatafuta wawekezaji wakuja kuusimamia?

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
877
4,106
TPA wameshindwa kuendesha bandari na sasa imekodishwa kwa wawekezaji.

SGR imekwama kukamilika kwa wakati kwa nchi kukosa wasimamizi wa ujenzi wenye ujuzi wanaothamini ukamilikaji wa miradi kwa wakati kuepusha hasara au kuongezeka kwa gharama

Mwendo kasi wamejenga barabara nyingi huko DSM lakini barabara moja tu iliyokamilika imetushinda kusimamia ilete tija.

Je, Mradi wa kuzalisha umeme wa mwalimu Nyerere tutauweza au tunakabidhi kwa mwekezaji aendeshe?
 
TPA wameshindwa lini kuendesha bandari? Walipewa hadi tuzo ya taasisi bora kuliko zote nchini inayochangia 40% ya pato la serikali, wahuni wachache wanaotaka kula keki ya taifa ndo eti wanaingia mkataba wa kimangungo
 
Back
Top Bottom