Ile issue ya Dau NSSF imeanzisha mada nyingine kuhusu TANESCO!!!, kumbe aliyeileta ile mada aligonga Ikulu!!. Dawa ni utafutaji wa elimu kwa udi na uvumba, mambo ya dini sio ya kutumika kama uhalalishaji wa mtu au jamii fulani kushindwa kupambana maishani. Cha kushangaza ni kwamba wadhifa wa Chief Secretary haujawahi kushikwa na muislam tangu tupate uhuru, lakini sijawahi kusikia malalamiko. Waislam wawili wamekaa Ikulu kwa kipindi cha miaka 20 lakini CS ameendelea kuwa mkristo.
Tuachane na hizi mada nyepesi za udini. Matatizo yetu ni makubwa na mengi, tunahitaji kuzalisha watafiti wengi sana. Umeme unawafikia watanzania wasiozidi asilimia 50. Yapo mengi ya maana ambayo bado hayajafanyika, zipo fursa nyingi tu ambazo bado hazijatumika vizuri. Huu uislam na ukristo ni sababu tu ya kuhalalisha kutopiga hatua kwetu. Waungwana tubadilike, maendeleo ya dunia hii wala hayatusubiri.