Kilawo
JF-Expert Member
- Nov 15, 2016
- 1,487
- 2,454
Acha uchonganishi bwana mdogo
Salio la songesha unaweza ukalifanyia miamala mingi tofauti na Songesha - LUKU ambayo utanunua LUKU pekee na huwezi kufanya muamala mwingine.ina tofauti gani na wanachofanya kampuni za simu tayari kama Vodacom wana songesha ambapo wanaweza kukukopesha ukanunua salio?
Wrong
Usifananishe serikali na mwananchi wa kawaida mkuu biashara ya kukopesha inaingiza faida kubwa saaaana fanya utafiti kwenye banks kisha utaleta majibu hapa...Mkuu serikali yenyewe hailipi madeni ya Tanesco sembuse Raia,
Kama yeye ni wrong, sema wewe hiyo right. JF siku hizi imevamiwa na maharamiaWrong
Naogopa kutaja eneo, ila shirika lina under go loss?
Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
Ulisoma report yote ya CAG?Hivi huku CAG mbona hatujamsikia ?
TANESCO waliweka limit ya kiwango cha matumizi na malipo? Unamruhusu mtu atumie umeme mpaka wa 400,000/= unategemea nini?Usiwarudishe nyumba. Walianza na mita za kawaida (unalipa baada ya matumizi), but watu walikuwa hawalipi kwa wakati au hawalipi kabisa.
Sisi wa TZ mtu anaweza kopo,akishindwa kulipa anaiharibu meter.hapo ni hasara kwa shirika.Kukopa kopa sio kuzuri bora ibaki hivi.
Mtu anaharibu meter kwa deni la 10,000?Sisi wa TZ mtu anaweza kopo,akishindwa kulipa anaiharibu meter.hapo ni hasara kwa shirika.
Mimi ni mpangaji,nakaa nyumba Luku yangu kila kitu sishei na mtuUnawezaje kukwepa deni la 20,000/= la LUKU?
Naunga mkono hoja kwa 100%Habari za wakati huu kaka na dada zangu wa humu JamiiForums.
Kwanini TANESCO haikopeshi units za umeme wa LUKU kwa wateja wake? Mimi ninaona kama mchakato huu utawawezesha kupata faida kubwa sana kama riba kwa maana ni ngumu sana kwa mteja kukwepa marejesho.
Tofauti ya mteja wa TANESCO na mteja wa mtandao wa simu za mikononi kama Vodacom na Tigo ni kwamba, mteja wa mitandao hii ana nafasi kubwa sana ya kutokulipa deni kwa maana anaweza kubadili simcard au anaweza kufa kisha deni likawa limepotea tofauti na mteja wa TANESCO ambaye deni linakuwa limebebwa na nyumba kiasi kwamba hata akifa, deni litakatwa wakati wa ku-transfer property ownership.
Mteja wa mitandao ya simu za mikononi anaweza akakopa Vodacom kisha akahama mtandao akaanza kutumia Tigo, lakini mteja wa TANESCO hawezi kubadili number yake ya mita ya LUKU. Kama alikopa umeme wa 20,000/= kwa kutumia M-PESA inakuwa ngumu sana kukopa tena kwa kutumia mtandao mwingine kama vile TIGO PESA kwa maana atatumia number ile ile ya mita hivyo computer system itakataa kufanya muamala wa kumpa units.
TANESCO wanaweza kufanya special arrangement na kampuni husika ya mtandao wa simu kama Vodacom au Tigo kutoka mkopo wa pesa mahususi kwa kununua units za umeme tu na sio muamala mwingine wowote. Ukitumia pesa hiyo kwa muamala mwingine inakataa.
Mathalana TANESCO wanaweza kukukopesha umeme wa 15,000. Halafu utakatwa labda 25% kila utakaponunua tena mpaka deni liishe. Au ukiamua unalipa 100%.
Wataalam wa masuala ya uchumi pamoja na ICT mnaweza kulifafanua hili zaidi kwa maana hiyo sio taaluma yangu lakini ninapendekeza number itakayoruhusiwa kukopa iwe moja tu (Mmiliki wa nyumba) hususan kwa nyumba zenye wakazi (wapangaji) wengi
NB: Ndugu zangu waislam, Mungu awatangulie na kuwasimamia katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani. Siku zote 30 za mfungo zikawe za kheri na baraka kwenu. Wishing you courage and strength so that you win every challenge of this life.
USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
hili ndio hata mimi nalitaka litokeee iwe kama tunavyolipia vifurushi vya ving'amuzi tuKwann mnapenda sana mkopo? Hii system ya TANESCO kutokopesha ni nzuri. Kuna nyumba za kupanga au fremu za biashara.
Mtu anakopa umeme wa laki moja ukiisha anahama. Mzigo unamwangukia mwingine
Naona waweke tu mfumo,ukinunua umeme kwa mfano wa 5000 unajijaza wenyewe. Hakuna kwenda kujaza kwenye mita
Sio kila nyumba ya kupanga ina watu wengi, kuna nyumba mpangaji anamiliki luku yake peke akeNi wapi nimezungumzia mkopo wa laki moja? Vodacom wanatoa mkopo wa laki moja kwa mara moja? Ndio maana nimesema anayeweze kuruhisiwa kukopa ni mtu mmoja tu.
Mnazingua kinoma hadi nahisi hii Account yenu huku JF pamoja na kuwa Verified nahisi kuna mtu binafsi kakaa geto anatuzingua,sioni kbisa msaada wenu nyie viumbe zaidi yakujibu kama ulivyojibu hapo juu.Tumepokea ushauri tunashukuru sana mpendwa mteja wetu
TANESCO , Makao Makuu