TANESCO inaweza ikatengeneza faida kubwa sana endapo wataanza kukopesha units za LUKU. Hii ni ngumu kwa mteja kukwepa marejesho

Dinazarde

JF-Expert Member
Jan 1, 2014
38,626
2,000
Mbona serikali inakopa?

IMG_7880.jpg

Friji kama linatakiwa lile umeme kiasi gani
Kama likiwashwa 24 hours ?
 

edwayne

JF-Expert Member
Apr 5, 2013
5,392
2,000
Tanesco hawafanyi biashara ipo kutoa service ya umeme kwa raia.. Inatakiwa isijiendeshe kwa hasara na faida ireinvest kuzalisha umeme zaidi
 

Auz

JF-Expert Member
Apr 6, 2016
8,786
2,000
Habari za wakati huu kaka na dada zangu wa humu JamiiForums.

Kwanini TANESCO haikopeshi units za umeme wa LUKU kwa wateja wake? Mimi ninaona kama mchakato huu utawawezesha kupata faida kubwa sana kama riba kwa maana ni ngumu sana kwa mteja kukwepa marejesho.

Tofauti ya mteja wa TANESCO na mteja wa mtandao wa simu za mikononi kama Vodacom na Tigo ni kwamba, mteja wa mitandao hii ana nafasi kubwa sana ya kutokulipa deni kwa maana anaweza kubadili simcard au anaweza kufa kisha deni likawa limepotea tofauti na mteja wa TANESCO ambaye deni linakuwa limebebwa na nyumba kiasi kwamba hata akifa, deni litakatwa wakati wa ku-transfer property ownership.

Mteja wa mitandao ya simu za mikononi anaweza akakopa Vodacom kisha akahama mtandao akaanza kutumia Tigo, lakini mteja wa TANESCO hawezi kubadili number yake ya mita ya LUKU. Kama alikopa umeme wa 20,000/= kwa kutumia M-PESA inakuwa ngumu sana kukopa tena kwa kutumia mtandao mwingine kama vile TIGO PESA kwa maana atatumia number ile ile ya mita hivyo computer system itakataa kufanya muamala wa kumpa units.

TANESCO wanaweza kufanya special arrangement na kampuni husika ya mtandao wa simu kama Vodacom au Tigo kutoka mkopo wa pesa mahususi kwa kununua units za umeme tu na sio muamala mwingine wowote. Ukitumia pesa hiyo kwa muamala mwingine inakataa.

Mathalana TANESCO wanaweza kukukopesha umeme wa 15,000. Halafu utakatwa labda 25% kila utakaponunua tena mpaka deni liishe. Au ukiamua unalipa 100%.

Wataalam wa masuala ya uchumi pamoja na ICT mnaweza kulifafanua hili zaidi kwa maana hiyo sio taaluma yangu lakini ninapendekeza number itakayoruhusiwa kukopa iwe moja tu (Mmiliki wa nyumba) hususan kwa nyumba zenye wakazi (wapangaji) wengi

NB: Ndugu zangu waislam, Mungu awatangulie na kuwasimamia katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani. Siku zote 30 za mfungo zikawe za kheri na baraka kwenu. Wishing you courage and strength so that you win every challenge of this life.

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
Kabla ya yote, kuna haja ya kuboresha mfumo wao wa malipo. Nasema hivi kwa kuwa kuna taasisi kwa ujumla wao zinadaiwa mabilioni ya shilingi, na haionekani kama kuna njia za kuwabana ili walipe. Sasa unachopendekeza kisije kikaliua shirika kabisa.
 

Haya_Land

JF-Expert Member
Dec 26, 2017
5,237
2,000
Wazo lako liko nyuma ya Muda sana .
Njia ya Tanesco kupata Faida nikuondoa corruption and embezzlement +ccm chama chakavu
 

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
13,863
2,000
..Ushauri wangu kakope kwa wakopeshaji ili ukanunue umeme kwani kuna taasisi zinajinadi kukopesha. La sivyo itafikia hadi kukopa sadaka kanisani pia itakua uzi
Mkuu, itoshe kusema tu ya kwamba hauna hoja zaidi za kupanic. Umepanic sana sasa sijui unampanikia nani?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom