Tamko la wazee Chadema: Mbowe ndiye kiongozi pekee barani Afrika asiyelipwa posho wala malipo yoyote na chama chake, anajitolea!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,962
141,961
Baraza la wazee wa Chadema limetoa tamko lake la kumtetea Mwenyekiti wa chama hicho dhidi ya njama ovu zinazotekelezwa na wabunge waliohamia CCM wakimtumia Mwita Waitara aliyewahi kuwa mlinzi wa Mbowe.

Katika tamko lake baraza la wazee limetaja sifa kuu 3 za Mbowe:

Mosi Mbowe ni mwenyekiti pekee wa chama cha siasa barani Afrika ambaye hapokei posho wala malipo yoyote kutoka kwenye chama chake anaitumikia Chadema kwa kujitolea.

Pili, Mbowe ndiye Mwenyekiti pekee wa chama cha siasa nchini anayeaminiwa na chama pamoja na wanachama ambao wameamchagua mara zote na amedumu katika uongozi kwa takribani miaka 25.

Tatu, Mbowe ndiye kiongozi pekee nchini aliyeingia katika uongozi akiwa tajiri na serikali kumfanyia figisu hadi anafilisika bila kuogopa wala kukata tamaa tofauti na wenyeviti wa CCM mzee Mwinyi, mzee Mkapa na mzee Kikwete ambao waliingia wakiwa maskini na kuondoka wakiwa matajiri.

Mwisho wazee hao wamemtaka Mwita Waitara kama ni mzalendo na siyo mnafiki anayejipendekeza, aanze kuhoji ufisadi unaofanywa na viongozi wa CCM.

Source: Ayo TV


Maendeleo hayana vyama
 
Tunataka TAKUKURU ifanye uchunguzi kwa ccm na viongozi wake,hofu yao ya uchaguzi isiwe kigezo cha kutumia vyombo vya dola kuhujumu vyama vingine. Kama takukuru ina nia ya dhati kusimamia fedha za vyama vya siasa Basi isioneshe upendelea wenye nia hasi, cuf tuliambiwa walitoa fedha kwenye akaunti ya chama na kuweka kwenye akaunti binafsi lkn hatukusikia takukuru wakifuatilia,ccm kumeibuliwa madudu hatukuona wakifuatilia, na hata serikalini pia iweje Leo iwe kwa chadema? Kuna mpango gani?
 
Michango ya wabunge bilioni 8.9 azirudishe kwanza kisha ndo tujadili huo uvumilivu wake.
 
Yaaani hiyo sababu ya kutolipwa posho ndo anatakiwa achunguzwe zaidi maana ina motive behind. Anakwapua nyingi zaidi. Toka lini hela zijae?
 
Back
Top Bottom