johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 83,968
- 141,976
Baraza la wazee wa Chadema limetoa tamko lake la kumtetea Mwenyekiti wa chama hicho dhidi ya njama ovu zinazotekelezwa na wabunge waliohamia CCM wakimtumia Mwita Waitara aliyewahi kuwa mlinzi wa Mbowe.
Katika tamko lake baraza la wazee limetaja sifa kuu 3 za Mbowe:
Mosi Mbowe ni mwenyekiti pekee wa chama cha siasa barani Afrika ambaye hapokei posho wala malipo yoyote kutoka kwenye chama chake anaitumikia Chadema kwa kujitolea.
Pili, Mbowe ndiye Mwenyekiti pekee wa chama cha siasa nchini anayeaminiwa na chama pamoja na wanachama ambao wameamchagua mara zote na amedumu katika uongozi kwa takribani miaka 25.
Tatu, Mbowe ndiye kiongozi pekee nchini aliyeingia katika uongozi akiwa tajiri na serikali kumfanyia figisu hadi anafilisika bila kuogopa wala kukata tamaa tofauti na wenyeviti wa CCM mzee Mwinyi, mzee Mkapa na mzee Kikwete ambao waliingia wakiwa maskini na kuondoka wakiwa matajiri.
Mwisho wazee hao wamemtaka Mwita Waitara kama ni mzalendo na siyo mnafiki anayejipendekeza, aanze kuhoji ufisadi unaofanywa na viongozi wa CCM.
Source: Ayo TV
Maendeleo hayana vyama