I'm Speechless!.
Ila pia tumepiga hatua kubwa sana za kimaendeleo ya kimawasiliano na kisheria, ambapo mawasiliano ya simu binafsi za watu ambayo ni siri, na yamepatikana kinyume cha sheria, yanapowekwa wazi kwa waandishi wa habari pamoja na namba za simu!, haya ni maendeleo makubwa sana kimawasiliano!.
Pia kwa kawaida, maombi huwasilishwa kwanza mahakamani ndipo umma ukatangaziwa ni maombi gani yamewasilishwa, lakini sasa kumbe unaweza kuwasilisha maombi kwa kuwatangazia wanahabari, hadi clasified information ulizonazo, ambazo zimepatikana kinyume cha sheria, kwa kutangaza details za hizo info, na ndipo kuziombea rasmi kibali cha mahakama ili ziwe releazed legally, haya pia ni maendeleo makubwa katika tasnia ya sheria!.
Kiukweli hii ni very high profile case, nadhani kwa kumbukumbu zangu, it the highest kwa hapa nchini, kwa mshatakiwa mmoja, kutetewa na mawakili 7!, wakati mshtakiwa mwenza bado hana wakili hata mmoja!.
Please watch out kwa twists and turns za hii kesi hapo mahakamani hiyo kesho!, mambo matatu haya yanaweza kutokea.
- Kesi inaweza kufutwa na kufunguliwa upya, washtakiwa wakaongezeka au kupunguzwa ukiwemo uwezekano mkubwa sana wa Ludo kuondolewa mashtaka na kugeuzwa shahidi No.1 wa serikali!.
- Kesi inaweza kufutwa na kufunguliwa upya ikijumlisha kosa la utekaji wa Kibanda.
- Kesi mpya ya shitaka la Kibanda inaweza kufunguliwa au hivyo kuzifanya hizi kesi kuwa ni kesi mbili tofauti.
- Kesi inaweza kuendelea kutajwa kama kawaida bali kwa kuongeza mshakiwa yule "Bukoba Boy!".
- Lolote kati ya hayo linaweza likafanyi, au yote yakafanyika au yote yasifanyike!.
Pasco.