Tamko la CHADEMA - Aprili 14, 2013

Tamko la CHADEMA - Aprili 14, 2013

Status
Not open for further replies.
Pole sana mkuu, hakika hata mimi nimesoma kwa huzuni sana na bbada ya kumaliza nikajiuliza mimi natoa mchango katika mapambano haya jibu ni moja niaendelea kukiwezesha chama changu ili wanaoifanya kazi hii njema wazidi kuifanya....

Nami sintachoka katika ukomboziiii huu na nitachangia kila kitu na jambo ndani ya uwezo wangu katika chama.... na sasa nipo kibaha tunamalizia ufunguzi wa kanda.

inaumiza sanaaaaaa yan mwingulu nchembaaaaaaaaaaaaa..... kwaniniiiiiiiii hiviiiiii...
 
Mkuu Artorius, kama una uwezo to read in between the lines, authenticity ya video hapa haijazungumziwa tena!. Wameisha jiridhisha it is "bonafide genuine!" kitachotafutwa sasa ni kumnasua tuu Rwakatare kwa kujenga hoja mchezo mzima ulikuwa ni mtego wa TISS, wakimaanisha Ludo, Msaki, Mchemba na vijana wao lao ni moja, Rwaka ndio oddman out!.
Pasco.

Acha uongo , wamesema kuhusu video editing iliyofanywa na Michuzi
 
Inasikitisha sana na tena inauma sana,naomba kuwashauri wanawake wa tanzania na vikongwe wote kuwa ccm ya mwalimu nyerere ndo inayotuua na ninawashauri waamke waikubali chadema,,na muomba Jk awe mzalendo na akemee uozo kwani ninahakika anajua mwanzo mwisho,tanzania leo inafika mda mtoto anasababisha nchi iingie katika hali ya umasikini,,nakumbuka mwalimu nyerere alisha wafukuza kazi wale waliomtetea mtoto wake kwamba asifukuzwe shule,kakini mtoto anaingiza nchi katika mikataba isiyo kuwa na kichwa wala miguu,,,JAKAYA MRISHO KIKWETE NA JOPO LA WANA CCM MUNGU SIKU YA MWISHO ATAWALIPA KADRI YA MATENDO YENU....INAUMA SANA JK.
huo ni upande mmoja hatujapata upande wa pili je tunaaminije?
 
Nimelisoma tamko hadi nimesisimka! Kama hayo aliyo yasema Marando ni kweli na iliyo kweli tupu basi nachelea kusema kuwa taifa letu haliko kwenye mikono salama hata kidogo! Wenzetu mataifa mengine wanazitumia siasa kwa ajili ya ustawi wa nchi sisi tunaitumia siasa kufanya uharamia na ugaidi wa kupanga.

Naomba niweke hakiba ya maneno kwa kusema, ukweli huwa una tabia ya kukawia kufika lakini huwa hauachi kufika uliko kusudiwa kufika.

CC chama, Ritz, ZeMarcopolo zumbemkuu Elli.

mkuu hakika taifa letu haliko katika mikono salama. tunapata picha ya kwamba serikali inalinda wahalifu, kumbuka rais alivyounga mkono kufungiwa kwa gazeti la Mwanahalisi baada ya kumtaja Ramadhani Ighondo.
 
Sina kumbukumbu vema, hivi ipo siku Nape aliwahi uzungumzia hili suala? au ndo keshasoma mchezo na sasa anamwaachaa Lameck afe na kabma yake kwa shingo!

Wakati mwingine Nape ni mtu mjanja sana.
 
Mkuu Artorius, kama una uwezo to read in between the lines, authenticity ya video hapa haijazungumziwa tena!. Wameisha jiridhisha it is "bonafide genuine!" kitachotafutwa sasa ni kumnasua tuu Rwakatare kwa kujenga hoja mchezo mzima ulikuwa ni mtego wa TISS, wakimaanisha Ludo, Msaki, Mchemba na vijana wao lao ni moja, Rwaka ndio oddman out!. Pasco.
by reading between the lines you mean skipping some lines au the whole para?
(Ndugu waandishi wa habari; Hawa niliowataja ni watu muhimu sana katika upangaji wa mkakati wa utengenezaji wa video ya Lwakatare na vitendo vya kihalifu vya utekwaji wa Kibanda na tukio la kutekwa na kisha kutupwa msutuni kwa mwenyekiti wa Jumuiya ya madaktari nchini, Dr. Steven Ulimboka. Kwa mfano, simu ya Mwigullu Nchemba, namba 0714 xxxxx, 0756 xxxxx na 0757 xxxxx, zimefanya mawasiliano mara kadhaa na Ludovick Joseph, Saumu K. Malungu, Jack Zoka, Ali Shaali na Ramadhani Ighondo. Mawasiliano hayo yalifanyika katika kipindi ambacho mgomo wa madaktari ulishamiri; baadaye yakarudi tena kati ya 26 Desemba mwaka jana na 15 Machi mwaka huu. Miongoni mwa mawasiliano ambayo tunaona yanahusika na ujambazi huu, ni yale ya 28 Desemba, siku ambayo mkanda wa Lwakatare umerekodiwa; tarehe 4 hadi 6 Machi 2013, siku moja kabla ya Kibanda kutekwa na yale ya usiku wa manane (saa 8:17) wa 13 Machi 2013, ambako mchana uliofuata Lwakatare alikamatwa. Huyu Mwagha ndiye aliyekuwa anatumika kuwasiliana na Saumu Malungu, ambaye tulimtaja kuwa ndiye aliyekuwa amepewa kazi na Mwigulu na usalama wa taifa, kurubuni vijana wetu kwa fedha ili kutoa ushahidi wa uongo juu ya video ya Lwakatare. Vilevile, mawasiliano ya Mwiguluna Mwagha, katika kipindi hicho nayo tunayahitaji. Kwa sababu, huyu Mwagha anayetumia simu 0754xxxxx, mbali na kuwasiliana na Mwigulu, ndiye aliyekuwa anawasiliana na mmoja wa waliomteka Ulimboka; na ndiye aliyewasiliana na Saumu kati ya 20Januari na Machi 6 mwaka huu.)
 
Mchumia tumbo mwingine huyu mwenye chuki za hali ya juu dhidi ya CHADEMA, hana ushahidi wowote ule kuhusu sinema ya Mwigulu Nchemba lakini alithubutu kuandika hapa kwamba sinema ile ni ya kweli ili afurahie kukamatwa na kufunguliwa mashtaka kwa viongozi wa juu wa CHADEMA na hivyo kusambaratika kwa CHADEMA.

salamu kwa pasco wa jf,alituambia ile video ni ya ukweli,pasco tunakutaka hapa jamvini mara moja
 
Magaidi wa CCM washindwe katika juhudi zao za kupandikiza ushahidi dhidi ya viongozi wa juu wa CHADEMA kwa nia ya kuwachafua, kuwaweka rumande na hatimaye kuwafungulia kesi za kizushi ili kukisambaratisha CHADEMA.

Alutta continua!! continua!!

😛eace:😛eace:😛eace:

Chadema watafute namna ya kumpongeza huyu jamaa wao wa usalama wa CHADEMA ambaye alikataa milioni 30 na mshahara wa laki tano kwa mwezi just kwa maslahi ya chama. I wish tungekuwa na vijana wa aina hii hata watano tu, pengine tungekuwa tulishaingia Ikulu siku nyingi sana.
Just imagine huyu usalama wa taifa analipwa hela za walipa kodi, lakini ndiyo hizo anajitolea kuzitumia kwa maslahi ya CCM. CHADEMA tukiingia Ikulu, kitu cha kwanza, kabla ya lolote lile, Kikwete aende segerea.
 
Nilishasema wewe ni kigeugeu tuu huna jipya! Naona umekuja na sarakasi nyingine! Hahahahahaha

I'm Speechless!.
Ila pia tumepiga hatua kubwa sana za kimaendeleo ya kimawasiliano na kisheria, ambapo mawasiliano ya simu binafsi za watu ambayo ni siri, na yamepatikana kinyume cha sheria, yanapowekwa wazi kwa waandishi wa habari pamoja na namba za simu!, haya ni maendeleo makubwa sana kimawasiliano!.

Pia kwa kawaida, maombi huwasilishwa kwanza mahakamani ndipo umma ukatangaziwa ni maombi gani yamewasilishwa, lakini sasa kumbe unaweza kuwasilisha maombi kwa kuwatangazia wanahabari, hadi clasified information ulizonazo, ambazo zimepatikana kinyume cha sheria, kwa kutangaza details za hizo info, na ndipo kuziombea rasmi kibali cha mahakama ili ziwe releazed legally, haya pia ni maendeleo makubwa katika tasnia ya sheria!.

Kiukweli hii ni very high profile case, nadhani kwa kumbukumbu zangu, it the highest kwa hapa nchini, kwa mshatakiwa mmoja, kutetewa na mawakili 7!, wakati mshtakiwa mwenza bado hana wakili hata mmoja!.

Please watch out kwa twists and turns za hii kesi hapo mahakamani hiyo kesho!, mambo matatu haya yanaweza kutokea.

  1. Kesi inaweza kufutwa na kufunguliwa upya, washtakiwa wakaongezeka au kupunguzwa ukiwemo uwezekano mkubwa sana wa Ludo kuondolewa mashtaka na kugeuzwa shahidi No.1 wa serikali!.
  2. Kesi inaweza kufutwa na kufunguliwa upya ikijumlisha kosa la utekaji wa Kibanda.
  3. Kesi mpya ya shitaka la Kibanda inaweza kufunguliwa au hivyo kuzifanya hizi kesi kuwa ni kesi mbili tofauti.
  4. Kesi inaweza kuendelea kutajwa kama kawaida bali kwa kuongeza mshakiwa yule "Bukoba Boy!".
  5. Lolote kati ya hayo linaweza likafanyi, au yote yakafanyika au yote yasifanyike!.

Pasco.
 
Hivi unajua maana ya ku edit? Si lazima mkanda mzima ufanyiwe editing!

vipi kuhusu zile chafya na kujifuta makamasi kwenye nguo, nazo ni editing??????tumia kichwa kufikiri badala ya kufuga nywele
 
Tamko hili lilitolewa baa gani na je mtoaji alkuwa ktk hali gani amelewa au?
 
mkuu umenichekesha kweli.....rukaruka ya kufa nadhani iko tofauti kidogo, mfano ni kama hii ya chadema...waambieni watulie wapeleke ushahidi mahakamani

tatizo la chadema ni kuongozwa kwa mawazo ya watu wachache wengine hawapewi nafasi ya kutoa mawazo yao hence wanapanga kuuwa halafu wanaandaa mikakati ya kujinasua.
 
"Kwa kauli hii, ambayo ameandika kiongozi wa upinzani, viongozi wanaowasiliana nao waunganishwe katika kesi ya ugaidi kuanzia leo wakamatwe na polisi, hapa simuoni kiongozi wa Kambi ya Upinzani, labda wameshamkamata," alisema Mwigulu.

Katika mazungumzo yake, Mwigulu ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM, alitaka Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Wilbrod Slaa, akamatwe kwa kuwa alihusika kumtetea Lwakatare.

Kwa mujibu wa Mwigulu, aliyekuwa akipanga njama za ugaidi huo ni mwanachama wa Chadema na kwamba fedha zilizotumika katika kufanikisha mpango huo, ni za chama hicho.

"Mnasubiri nini polisi, mtu ameshaomba kuunganishwa mwenyewe katika kesi?"

"Mkishapanga maovu mnawahi kwenda kutetea kama vile mchawi ambaye akishaua, anawahi kwenda kulia na kugalagala msibani. Mimi kwenye hili suala la mauaji, nawaomba Chadema mfanye vitu viwili, kwanza kimbieni haraka zaidi kwenye makanisa ama misikiti mliyokaribu nayo ili mkatubu kuwa mmepanga kuwauwa watu wasio na hatia.

"Baada ya kuomba toba, mrudi kutubu kwa wananchi, yaani mnataka uongozi halafu unawaza kuuwa watu, look at you,"
 
Nami sintachoka katika ukomboziiii huu na nitachangia kila kitu na jambo ndani ya uwezo wangu katika chama.... na sasa nipo kibaha tunamalizia ufunguzi wa kanda.

inaumiza sanaaaaaa yan mwingulu nchembaaaaaaaaaaaaa..... kwaniniiiiiiiii hiviiiiii...

mkuu mwigulu mwiba nini make hum jf ni mwigulu tu nadhan cdm hawalali kuhusu mwigulu.
 
Nilishasema wewe ni kigeugeu tuu huna jipya! Naona umekuja na sarakasi nyingine! Hahahahahaha

Yaani katika vitu ninavyomuadmire kiasi kwamba l wish ningekuwa navyo kimoja wapo ni 'kukosa haya'; jamaa hana haya kabisa wala haoni ubaya, maana some of us tunashindwa ku-dare kusupport au kufanya ujinga kwa 'haya' tulizoumbwa nazo!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom