Tamko la CHADEMA - Aprili 14, 2013

Tamko la CHADEMA - Aprili 14, 2013

Status
Not open for further replies.
C'MON CCM -- come to the point na ukiweza pangua hoja hizo hapo -- hata 30% tu. Hamuwezi chochote siku hizi zaidi kuwatia Watz umasikini, labda na uzinzi! SEMENI, KITU GANI MNAWEZA?

Changamoto kubwa inayoikabili CCM sasa hivi ni kwamba chama hichi hakijui kama haijui chochote.
 
Main ishu ni hizo kumbukumbu za kwenye mitandao ya simu....nashauri cdm watumie ushushushu wao kuzipata mapema.

Wafanyakazi wa voda, tigo , airtel ambao ni wazalendo mtusaidie ili taifa lipone.

Kisimani hata mm nilikuwa na hofu kama yako issue ni kuwa washazidaka, issue za kuomba mahakama iruhusu ni kwa ajili ya kufuata taratibu tu!
 
Kumekucha...Mwili mzima umetetemeka...!

mkuu molemo hii imenikumbusha toleo la mwisho la mwanahalisi na habari ya rama. Tamko linajieleza ngoja watanzania wajionee wenyewe labda wanunue magazeti yote kesho
 
Mkuu wa JF nakupongeza kwa msimamo wako wa kulinda maslahi mapana ya watanzania kwa kutoshirikiana na maafisa usalama wa Taifa waovu waliotaka kuitumia JF na wewe mwenyewe kuwadhuru wananchi wasio na hatia.

Nakuomba uendelee kushikilia msimamo huo huo Mungu ataendelea kukulinda na kukupigania na kukuepusha na hila zote za policcm, usalama wa ccm na waovu wote walioko ccm na serikalini.

Kwa kamanda Mabere Nyaucho Marando, ahsante sana kwa kuwa-beep wapanga mipango ya uhalifu nchini. Sasa kwakuwa kila siku wanapiga mayowe kuwa simu zao zimejaa 'credit' tunasubiri kuona mwenye jeuri ya kukupigia!
 
mmhh! tunakoenda sio salama, kama CDM waweza kuyajua haya, kikwete anafanya nini Ikulu, mbona naona yupo uchi?

nimekubali chadema wako makini kuliko usalama wa taifa. sikuwaelewa na sasa nimewaelewa
 
Mkuu wa JF nakupongeza kwa msimamo wako wa kulinda maslahi mapana ya watanzania kwa kutoshirikiana na maafisa usalama wa Taifa waovu waliotaka kuitumia JF na wewe mwenyewe kuwadhuru wananchi wasio na hatia.

Nakuomba uendelee kushikilia msimamo huo huo Mungu ataendelea kukulinda na kukupigania na kukuepusha na hila zote za policcm, usalama wa ccm na waovu wote walioko ccm na serikalini.

Kwa kamanda Mabere Nyaucho Marando, ahsante sana kwa kuwa-beep wapanga mipango ya uhalifu nchini. Sasa kwakuwa kila siku wanapiga mayowe kuwa simu zao zimejaa 'credit' tunasubiri kuona mwenye jeuri ya kukupigia! Nategemea Mwigulu Nchemba awe wa kwanza kukupigia kwakuwa ana credit ya kutosha kuliko wenzake.
 
Last edited by a moderator:
I'm Speechless!.
Ila pia tumepiga hatua kubwa sana za kimaendeleo ya kimawasiliano na kisheria, ambapo mawasiliano ya simu binafsi za watu ambayo ni siri, na yamepatikana kinyume cha sheria, yanapowekwa wazi kwa waandishi wa habari pamoja na namba za simu!, haya ni maendeleo makubwa sana kimawasiliano!.

Pia kwa kawaida, maombi huwasilishwa kwanza mahakamani ndipo umma ukatangaziwa ni maombi gani yamewasilishwa, lakini sasa kumbe unaweza kuwasilisha maombi kwa kuwatangazia wanahabari, hadi clasified information ulizonazo, ambazo zimepatikana kinyume cha sheria, kwa kutangaza details za hizo info, na ndipo kuziombea rasmi kibali cha mahakama ili ziwe releazed legally, haya pia ni maendeleo makubwa katika tasnia ya sheria!.

Kiukweli hii ni very high profile case, nadhani kwa kumbukumbu zangu, it the highest kwa hapa nchini, kwa mshatakiwa mmoja, kutetewa na mawakili 7!, wakati mshtakiwa mwenza bado hana wakili hata mmoja!.

Please watch out kwa twists and turns za hii kesi hapo mahakamani hiyo kesho!, mambo matatu haya yanaweza kutokea.

  1. Kesi inaweza kufutwa na kufunguliwa upya, washtakiwa wakaongezeka au kupunguzwa ukiwemo uwezekano mkubwa sana wa Ludo kuondolewa mashtaka na kugeuzwa shahidi No.1 wa serikali!.
  2. Kesi inaweza kufutwa na kufunguliwa upya ikijumlisha kosa la utekaji wa Kibanda.
  3. Kesi mpya ya shitaka la Kibanda inaweza kufunguliwa au hivyo kuzifanya hizi kesi kuwa ni kesi mbili tofauti.
  4. Kesi inaweza kuendelea kutajwa kama kawaida bali kwa kuongeza mshakiwa yule "Bukoba Boy!".
  5. Lolote kati ya hayo linaweza likafanyi, au yote yakafanyika au yote yasifanyike!.

Pasco.
 
aise hii taarifa imenitetemesha,kama ni kweli basi Chadema iko makini zaidi ya tunavyofikiria.
 
mwanzo mpaka mwisho nasoma uku nikilia sanaaaa na mpaka sasa naendelea kulia tuuuuuuuuu

Mungu bariki tanzania
mungu bariki chadema
 
CCM wako makini kwa mambo ya kiungebe kama haya, wangelikuwa na jitihada kama hizi kweny maendelep tucngelikuwa hapa tulipo,

(ee mola wasambaratishe haya magamba kama ulivyowasambaratisha maadui wa wana wa Israeli ktk bahari ya shamu kupitia tamko la Musa, naamini hutaruhusu kuteseka na kuuawa kw binadamu ulowaumba wewe kiasi ichi)
 
Mungu ibariki Tanzania, chadema. Tunaomba hawa mafedhuli uwaumbue zaidi na kuwanyang'anya dola. kwa kuwa wanatenda yasiyokupendeza. Tunaomba uelekeze hasira yako juu yao ili wasilisahau pigo lako kuu.
 
Kuhusu Msacky -- Kulikuwapo thread moja humu kama wiki moja iliyopita iliyomtaka Tido Muhando amhoji na kumsimamisha kazi Msacky kutokana na kutajwa sana katika sakata hili.

yeye Msacky awali alitajwa kama ni mmoja wa wale ambao wanatajwa katika video ya Lwakatare kwamba atadhuriwa -- ingawa sasa naona hii does not make sense. Mtu anayetarajiwa kudhuriwa na Ludovick wamekuwa wanawasiliana mara kadha!

Kwa upande mwingine mie namfahamu sana Msacky -- ni mtu ambaye hujipendekeza sana kwa CCM hivyo anweza kutumika katika sakata hili.

TIDO -- linda heshima yako -- msimamishe kwanza Msacky!
 
Ee mungu tunaomba utulinde na hawa wafuasi wa shetani kwa matendo yao, uwaangamize kabisa hata masalia yao tusiyaone. Watesi na watekaji wakuu.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom