Tamko la CHADEMA - Aprili 14, 2013

Tamko la CHADEMA - Aprili 14, 2013

Status
Not open for further replies.
Ninatoa agizo kwa wote wenye kuitaki mema nchi hii,tufunge kwa siku tatu ili MUNGU atuwekee wazi kilichofichika ktk kesi hii,MUNGU usituache tukatekwa na hawa ibilisi
 
Mkuu.
Sina cha kusema kuhusiana na uwepo wa namba ya Zitto kwenye mlolongo wa mawasiliano hayo, mimi sio msemaji wa chama, kwa kuwa Zitto mwenyewe yupo humu naamini ata wiwa kutoa maelezo ya kina yasiyo acha nyayo za mashaka nyuma yake.
Haya haya........
 
Mabere kafanya ufafanuzi mzuri, ila umma wa watanzania tunajua nini kilimpata DR. Ulimboka na Kibanda, na nini kinatakiwa kufanyika kuimaliza CDM.

CDM mwendo mdundo, CCM wameshagawanyika, TISS wameshagawanyika -- chama cha majambazi hiki kinataka kutawala kwa kutumia nguvu za giza.

Dua kuliombea taifa letu

Eee baba wa taifa huko uliko endelea kushusha mzimu wako duniani uyalaani haya majitu yaumbuke, yanayotoa roho za watu, kuwapa watu vilema vya maisha as if yataishi milele hapa duniani.

Baba wa taifa uliyakabidhi nchi iliyokuwa na misingi bora ya usawa na haki, sasa Baba yetu yameanza kututoa meno na kucha. tunaangamia ndani ya nchi yetu uliyotuachia. yashushie Laana kubwa utuokoe sisi watanzania uliotupenda sana enzi za uongozi wako.
 
chadema kila wiki wana tamko last week ilikuwa iringa wik hii marando may be wiki ijayo mushumbuzi kimekuwa chama cha matamko,maandamano.ugaidi,sumu,ukabila,ukanda bila kusahau propaganda badala ya hoja mbadala kwa ccm

Wewe unaweweseka baada ya kuvuliwa nguo kutokana na ugaidi wa magamba sasa ndio mtajua kuwa unaweza kufanya vitu gizani lakini ukaumbuka siku moja mchana kweupe.
 
Nchemba usihangaike kwenda kuomba voda wafute mawasiliano yako, si kwa kujiona kidume kutembea na wake za watu ulidhani utakuwa kidume pia kwa CDM. UTAJUTA KUIJUA NAMBA DOGO.
 
mpaka wanasema hvyo ujue CDM tayari wanazo taarifa zote za no. zote hzo za simu. hvyo wanawambia kuwa wasije wakafikhria walichokifanya ni kizuri kwao na ni kidogo kumbe wametengeneza ishu zito tena ya kigaidi ambayo wanatakiwa kujibia.

hujui unachokiongea, wewe unadhani wamekurupuka? Hilo benchi la mawakili wote ni vichwa..najua hawataruhusu maana inawahusi wakubwa mpaka raisi anahusika..
 
Mohamedi Mtoi
Nadhani mnajitahidi sana kutafuta mchawi; kwanza mlidai video ni fake; baada ya kupata uhalisia wa video mnataka kuipaka matope serikali; kinachomuweka kitanzini Lwakatare ni maneno/kauli yake mwenyewe yeye alikuwa akitoa maelekezo namna ya kufanya uharamia; sasa serikali inahusika vipi? Nadhani umesahau kitu hiki “law abide citizen” raia mmoja anayeitakia mema nchi hii ndiye aliyemnasa Lwakatare na ndiye aliyetoa taarifa kwa vyombo husika; Lwakatare ni mhalifu sioni unachotetea.
Chama

Hayo mawasiliano yaliyofanyika kwa hizo cm zilizotajwa ndo yatathibitisha ufake au uhalali wa hiyo video,just relax,everything is under control-hakuna pa kutokea coz kwa Uli the easy way ilikuwa kuifungia mwanahalisi,this time-NO WAY!
 
Last edited by a moderator:
Swali dogo tu,mkanda ule feki au orijinol?me nimeuona unatisha na unapanga mauaji.tunajua historia ua MABERE, lkn hivi karbuni alikuwa anawatetea wezi wa EPA Mahakamani lkn chama chake kinaimba Ufisadi,kama alivyosema MWIGULU wanaroga haohao lkn mtu akifa wanalia haohao,mchana watu usiku "nyau nyau".
 
There are currently 1444 users browsing this thread. (184 members and 1260 guests)
 
Swali dogo tu,mkanda ule feki au orijinol?me nimeuona unatisha na unapanga mauaji.tunajua historia MABERE, lkn hivi karbuni alikuwa anawatetea wezi wa EPA Mahakamani lkn chama chake kinaimba Ufisadi,kama alivyosema MWIGULU wanaroga haohao lkn mtu akifa wanalia haohao,mchana watu usiku "nyau nyau".
 
Wadau, siamini kama tamko hili limetolewa na mwanasheria ambaye si tu amebobea katika fani yake bali pia ni mtu ambaye aliwahi kufanya kazi katika idara ya usalama wa taifa kutokana na ushahidi wa tamko lake hili. Cha kusikitisha zaidi, ameongea mambo ambayo anajua kuwa anayo fursa kupitia mahakama kueleza yote hayo ambako ninaamini ndiko kwenye msaada mkubwa kuliko kuongea na waandishi wa habari ambao wataishia kuandika tu. ninajua kwa sasa chadema wanatafuta huruma za wananchi kupitia matamko yao hayo kwa vile wamechungulia na kuona kuwa hawawezi kushinda kesi ya lwakatare.

Ungejiuliza kwanza kwanini mkanda uliletwa JF alafu ndo Lwakatare akakamatwa na wao walitaka huruma za wananchi? Kama wanalipeleka kisiasa na sisi tunalipeleka kisiasa. Mwigulu anasema CDM ifutwe ni chama cha kigaidi na siisi tunawaambia wananchi waamue chama kipi ndo cha kigaidi? Goes around comes around
 
Mungu yupo upande wetu CHADEMA. naamin katika uchunguzi huu makini mawasiliano ya Zitto hayawezi kukosa sema chama kimeamua kutokuweka ukweli wote bayana kwa maslahi mapana ya chama na taifa, Maana kuanzia alivyokurupuka ktk swala la kutaka lwakatare awajibishwe na kuvujisha barua mitandaoni basi ni wazi kwamba the guy Zitto yupo nyuma ya saga hili sema kwa ajili ya hekima huenda chama kimeacha kumuhusisha.

Cc Lukolo, Lwesye, Greenwhich
Hata mimi niliposoma tu hiyo orodha ya namba za simu, nilijua kabisa kwamba ya Zitto imeachwa kwenye hiyo orodha kwa ajili ya usalama wa CHAMA. Lakini Dr. Slaa ameshatuaminisha kwamba CHADEMA ipo makini kuliko serikali, makini kuliko CCM na makini kuliko usalama wa taifa. Tuamini kwamba tupo salama.
 
Mwanakijiji it'S 'bout time video ya Lwakatare irudi hapa kwa elimu zaidi!
 
Hakuna kumumunya maneno. Hii namba +255 756 809 535 ni ya Zitto Zuberi Kabwe. Mmoja wa washiriki wakuu wa mpango wa kukiua CHADEMA !

Kwani ni nani asiyejua hili ? mawasiliano yake na Bwana Msaky wa Mwananchi na pia Usalama wa taifa mbona ulishawekwa wazi siku nyingi ???

Kumbuka : Kikulacho kii nguoni mwako.

Ndugu zangu wana JF

Namba hiyo iliyotajwa hapo juu imewahi kuwa namba yangu ya Simu. Namba hii nimeacha kuitumia toka mwezi Juni/Julai mwaka 2012. Hata hivyo namba hii bado inaonekana kwenye businesscard yangu na kwenye email zangu sehemu ya anuani. Namba hii haijawahi kuwa ya Zoka. Imewahi kuwa ya Zitto Zuberi Kabwe peke yake. Namba hii haitumiki toka katikati ya mwaka 2012.

Kama JF inataka kuthibitisha hili waunde jopo la wanaJF watakaopata taarifa za namba hii popote wanapoweza kupata.

Mambo 2, ama namba hii imewekwa kwa bahati mbaya kwenye tamko tajwa au imewekwa makusudi kwa sababu maalumu zenye lengo la kutoa ujumbe fulani kwa watu.

Kwa namna namba hii ilivyochomekwa kwenye tamko hili au hapa JF au vyote kwa pamoja, ni dhahiri kuna juhudi za kunihusisha na upuuzi huu wa ugaidi na unyama dhidi ya binaadamu.

Napenda kusisitiza kwamba, sihusiki kwa namna yeyote ile katika kuwaza, kupanga au kutekeleza mipango yeyote ya kudhuru mtu ama kwa njia za kigaidi au za kijinai. Sihusiki kwa namna yeyote ile kupanga mpango wowote ule wenye lengo la kuhusisha chama changu na vitendo vyovyote vya kigaidi au kudhuru mtu yeyote yule. Juhudi zozote zinazofanywa na maadui wa chama changu za kunihusisha na mambo haya zitashindwa kwani siku zote ukweli huwa bayana.

Napenda kuweka wazi kwamba Mhariri wa Mwananchi ndugu Dennis Msacky ni rafiki yangu wa karibu sana. Ninaamini kabisa kwamba katika suala hili Dennis Msacky ni victim. Juhudi zozote zile za kutaka kumgeuza 'victim' kuwa mtuhumiwa lazima zitashindwa tu kwani siku zote HAKI hutamalaki.

Mtu yeyote anayetaka kutumia urafiki wangu na Dennis Msacky kutaka kujifurahisha kisiasa ajue kuwa furaha yake hiyo itakuwa ni ya muda mfupi sana maana ukweli ukidhihiri atapata aibu kubwa sana.

Ni muhimu sasa mambo haya tuiachie mahakama itende haki.
 
nawaomba sana watanzania waamke na wajitambue na waache ushabiki haya mambo si mazuri kama unaweza kuua watanzania wenzetu bila hatia na kuanza kusisingizia chadema ni hatari sana lakini naomba niuweke ukweli huu kwamba tuko tayari kupambana na mtu yeyote anayehujumu chadema au mtanzania mwenzetu asiyekuwa na hatia ccm your in danger go on
 
Mungu ibariki tanzania kama haya niyakweli CCM na TISS wamevuliwa nguo mbele za wakwe.
 
Thanx so much guys for following up closely. Watu wengi wanafuatilia na kujadili. Mijadala ni muhimu. Tafakuri ni afya kwa ubongo. Naona wamepungua kidogo, kabla sija copy na ku paste, walikuwa 1411.

There are currently 1403 users browsing this thread. (174 members and 1229 guests)
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom