Tamko la CHADEMA - Aprili 14, 2013

Tamko la CHADEMA - Aprili 14, 2013

Status
Not open for further replies.
mmhh! tunakoenda sio salama, kama CDM waweza kuyajua haya, kikwete anafanya nini Ikulu, mbona naona yupo uchi?

Wote tunashanga hilo labda hatuba yake mwisho wa mwezi itakuwa ya kutangaza kujiuzulu. Tangu sakata la Richmond walimstahi tuu sasa kansa ya kuwahujumu watanzania inaendelea kumtafuna, nasema haya kwa sababu suala hili lazima Rais analijua na kama halijui basi si yeye anayeongoza nchi hii.
 
Lengo la chadema kutoa haya matamko ni kwamba wanataka wajibiwe na serikali au CCM halafu mwanaharakati wao mwanakijiji na wenzake weaendeshe haraki za kutaka kesi ifutwe.

Wote mlishuhudia Mbowe alivyoenda kuungumzia kesi Bungeni halafu mwanakijiji very quickly akaanzisha harakati za kutka kesi ifutwe. Kwa sababu harakati zile hazijafanikiwa sasa wameamua kuja nje ya Bunge ili kusiwe na kinga ya Bunge.

Mkuu ZeMarcopolo

Mbona unajichanganya sana. Hebu jisome vizuri tena.
 
Asante mkuu kwa kuweka bayana hili suala la namba.

Binafsi naona CHADEMA, kwa mara nyingine tena wamefanya "wrong move".

Matamko na press conference zimezidi mpaka mwelekeo haueleweki. Kila kiongozi anazungumza anavyojua yeye. Ni aibu kwa chama kinachojinasibu kuwa makini.

Ulitueleza hapa kuwa mmekubaliana kuwa katika suala la kesi ya Lwakatare mzungumzaji kwa niaba ya chama atakuwa ni Mh. Lissu peke yake. Lakini haijapita hata wiki Marando naye anakuja na vioja vyake.

Umakini wa taasisi yoyote ujidhihirisha wakati wa majaribu. Katika hili sio siri Chadema mumefeli.

Kwenye ukweli lazima tuelezane wazi wazi.

Suala lipo mahakmani, kama mna ushahidi substantial si muupeleke mahakamani.

Au ndo chama kinatafuta public sympathy?

asante sana mkuu...umesema sana, kama wanatumia kichwa kufikiri wamesikia
 
Ndugu zangu wana JF

Namba hiyo iliyotajwa hapo juu imewahi kuwa namba yangu ya Simu. Namba hii nimeacha kuitumia toka mwezi Juni/Julai mwaka 2012. Hata hivyo namba hii bado inaonekana kwenye businesscard yangu na kwenye email zangu sehemu ya anuani. Namba hii haijawahi kuwa ya Zoka. Imewahi kuwa ya Zitto Zuberi Kabwe peke yake. Namba hii haitumiki toka katikati ya mwaka 2012.

Kama JF inataka kuthibitisha hili waunde jopo la wanaJF watakaopata taarifa za namba hii popote wanapoweza kupata.

Mambo 2, ama namba hii imewekwa kwa bahati mbaya kwenye tamko tajwa au imewekwa makusudi kwa sababu maalumu zenye lengo la kutoa ujumbe fulani kwa watu.

Kwa namna namba hii ilivyochomekwa kwenye tamko hili au hapa JF au vyote kwa pamoja, ni dhahiri kuna juhudi za kunihusisha na upuuzi huu wa ugaidi na unyama dhidi ya binaadamu.

Napenda kusisitiza kwamba, sihusiki kwa namna yeyote ile katika kuwaza, kupanga au kutekeleza mipango yeyote ya kudhuru mtu ama kwa njia za kigaidi au za kijinai. Sihusiki kwa namna yeyote ile kupanga mpango wowote ule wenye lengo la kuhusisha chama changu na vitendo vyovyote vya kigaidi au kudhuru mtu yeyote yule. Juhudi zozote zinazofanywa na maadui wa chama changu za kunihusisha na mambo haya zitashindwa kwani siku zote ukweli huwa bayana.

Napenda kuweka wazi kwamba Mhariri wa Mwananchi ndugu Dennis Msacky ni rafiki yangu wa karibu sana. Ninaamini kabisa kwamba katika suala hili Dennis Msacky ni victim. Juhudi zozote zile za kutaka kumgeuza 'victim' kuwa mtuhumiwa lazima zitashindwa tu kwani siku zote HAKI hutamalaki.

Mtu yeyote anayetaka kutumia urafiki wangu na Dennis Msacky kutaka kujifurahisha kisiasa ajue kuwa furaha yake hiyo itakuwa ni ya muda mfupi sana maana ukweli ukidhihiri atapata aibu kubwa sana.

Ni muhimu sasa mambo haya tuiachie mahakama itende haki.

Sasa umekuja kutoa ufafanuzi wa namba au kupinga tamko la chama chako??
 
Hili tamko lenye taarifa za kutunga ni tisa, kumi ni uhalisia wa video ya kigaidi ya lwaka, mwanasheria wakili shshushu amekichimbia chama kwenye shimo la takataka
 
Mkuu ZeMarcopolo

Mbona unajichanganya sana. Hebu jisome vizuri tena.

Makene,

Twende kwanza tukajadili lengo lililowafanya muingize namba ya Zitto kwenye tamko.

Je, mnataka kumchafua Zitto?

Je, harakati zenu za kumfanya Msacky aonekane mtuhumiwa zina lengo gani?

Tukutane kwenye ile thread ya Zitto...
 
Ndugu zangu wana JF

Namba hiyo iliyotajwa hapo juu imewahi kuwa namba yangu ya Simu. Namba hii nimeacha kuitumia toka mwezi Juni/Julai mwaka 2012. Hata hivyo namba hii bado inaonekana kwenye businesscard yangu na kwenye email zangu sehemu ya anuani. Namba hii haijawahi kuwa ya Zoka. Imewahi kuwa ya Zitto Zuberi Kabwe peke yake. Namba hii haitumiki toka katikati ya mwaka 2012.

Kama JF inataka kuthibitisha hili waunde jopo la wanaJF watakaopata taarifa za namba hii popote wanapoweza kupata.

Mambo 2, ama namba hii imewekwa kwa bahati mbaya kwenye tamko tajwa au imewekwa makusudi kwa sababu maalumu zenye lengo la kutoa ujumbe fulani kwa watu.

Kwa namna namba hii ilivyochomekwa kwenye tamko hili au hapa JF au vyote kwa pamoja, ni dhahiri kuna juhudi za kunihusisha na upuuzi huu wa ugaidi na unyama dhidi ya binaadamu.

Napenda kusisitiza kwamba, sihusiki kwa namna yeyote ile katika kuwaza, kupanga au kutekeleza mipango yeyote ya kudhuru mtu ama kwa njia za kigaidi au za kijinai. Sihusiki kwa namna yeyote ile kupanga mpango wowote ule wenye lengo la kuhusisha chama changu na vitendo vyovyote vya kigaidi au kudhuru mtu yeyote yule. Juhudi zozote zinazofanywa na maadui wa chama changu za kunihusisha na mambo haya zitashindwa kwani siku zote ukweli huwa bayana.

Napenda kuweka wazi kwamba Mhariri wa Mwananchi ndugu Dennis Msacky ni rafiki yangu wa karibu sana. Ninaamini kabisa kwamba katika suala hili Dennis Msacky ni victim. Juhudi zozote zile za kutaka kumgeuza 'victim' kuwa mtuhumiwa lazima zitashindwa tu kwani siku zote HAKI hutamalaki.

Mtu yeyote anayetaka kutumia urafiki wangu na Dennis Msacky kutaka kujifurahisha kisiasa ajue kuwa furaha yake hiyo itakuwa ni ya muda mfupi sana maana ukweli ukidhihiri atapata aibu kubwa sana.

Ni muhimu sasa mambo haya tuiachie mahakama itende haki.

mkuu inamaana Marando kaandaa na kutoa tamko hilo bila wewe kuhusishwa? kama ndivyo basi naamini kuwa CHADEMA kuna vurugu inaendelea kubwa na mwisho wake utakuwa mbaya.

Leka dutigite kwa sasa
 
Duuu baada ya kuchamba kwingi leo wameshika MAVI. X
 
Kuna watu watavuliwa nguo au watavua nguo kwa kuchanganyikiwa wenyewe mchana kweupe...... The truth will always come to the surface
 
Sasa umekuja kutoa ufafanuzi wa namba au kupinga tamko la chama chako??

tulieni dawa iingie vizuri mamburula...mmeingizwa choo cha kike na shushushu marando ambaye anakula mshahara wa serikali hata hamshtuki mnapiga mayowe tu hapa
 
CHADEMA MUOGOPENI MUNGU

Muendelezo wa matamko yasiyokuwa na mashiko ya chadema juu ya mambo mbalimbali nchini sasa yanapaswa kupuuzwa kwani wanajaribu kuwahadaa wananchi. Wanatoa Majibu mepesi kwenye maswali magumu ambayo wanaharakati na wapenda maendeleo wa nchi hii wanauliza mathalani kwa nini chama kinachojiita CHA demokrasia Leo hii kimekuwa kinakandamiza demokrasia mfano 1. Pindi mh Zitto alisema atagombea uraisi kupitia chadema kukajitokeza kundi la watu ndani ya chama hicho wakasema Zitto anakivuruga chama na wakati huo huo mwenyekiti aw chama hicho akawatangazia watu wa KARATU kuwa Mungu akimpa uhai DKT SLAA ndiye atakuwa mgombea wa uraisi!! Watu wanajiuliza Mchakato wa kumpata SLAA ulifanyika lini, wapi, kwa katiba ipi?
Aidha pia wakati Watanzania wakiwa na msononeko, mfadhaiko wa moyo kuwa chama kinachojipambanua kuwa kinapigania maslahi ya wananchi kimegeuka kuwa TISHIO kwa umma, kinapanga na kuratibu na kutekeleza mauaji ya watu wasio na hatia!! Video clip iliyotapakaa kila kona ya websites za mitandao mbalimbali inaonyesha kuwa KIONGOZI wa juu wa chadema anayeshughulika na masala ya ulinzi na usalama bwana Lwakatare anapanga namna ya utekelezaji wa mauaji ya WAANDISHI habari ambao wao kwao ni tishio kwa uhai wa CHADEMA! Lakini pia anaelezea namna mipango mingine ya mauaji yaliwahi kupangwa na kwa namna hayakuweza kuzaa matunda Kama alivyosema swala la Igunga, na Iringa. Hizi ni tuhuma nzito ambazo zinahitaji tafakuru ya kina ya wananchi juu ya usalama wao na ni nini hasa maana ya dhana ya demokrasia ambayo inaendeshwa na vyama pinzani!
Tamko la CHADEMA kupitia kwa mwanasheria wake bwana MARANDO ni dhahiri chama hicho kimepoteza dira, kinamchoko wa kifikra na sasa kinatafuta kila njia na hila kijisafisha machoni mwa Watanzania kuwa sio chama cha kigaidi. Kama bwana marando anaushaidi wa kimawasiliano ya watu anaohisi wametengeneza clip ya Lwakatare ( ugaidi) ni vyema akapeleka ushaidi huo mahakamani kwani ndipo Haki utafutwa na kupatikana na aache kuwahadaa wananchi kwa matamko yasiyokuwa na tija. Watanzania wanaimani na Mahakama yao hata chadema wameshawahi kukiri wanaimani na Mahakama kwani hata wao wamekuwa wakishinda kesi nyingi tu kupitia Mahakama lakini wakati mwingine wanasema Mahakama si Huru.

RAI yangu kwa Chadema
Kuitisha kikao cha haraka kwa viongozi wa juu wa chama kutathimini, kutafakari maamuzi yake ya kupanga, kuratibu, na kutekeleza mateso ya kigaidi,kinyama Kama sera ya kuhadaa wananchi kuwa Ccm na vyombo vya dola vinapanga mauaji, na Mateso ya wapigania Haki! Kwani ukweli sasa umejulikana. Pili viongozi wa juu aw chadema watubu na kuomba radhi kwa Watanzania juu ya mipango yake ovu ya mateso na mauaji na mwisho kabisa waombe kwa Mungu wawe na HOFU YA MUNGU.
 
Habari za usiku wanabodi.

Mimi natoa yaliyo moyoni kwa mawazo yangu HURU.

Mimi DONYONGIJAPE, mzawa wa SIMANJIRO, naamini kabisa kwamba mtu mbaya kwa CHADEMA ni LWAKATARE. Inaonekana kabisa amefanya lile Tukio akijua kabisa anarekodiwa, na ndio maana akaongea hayo aliyoongea eili kuiharibia CHADEMA. NDIYO, ana uwezo huo, tena inaonekana alijipanga kabisa kuongea hayo yeye na huyo Ludovick. Ndio maana walikuwa wakipeana leading Questions.

Ninachokiona ni kwamba, Bw. Lwakatare amekula njama na Mwigulu, Ludo, Zoka, Zitto etc ili waichafue CHADEMA. Huyu siyo mtu wa kutetea kabisa katika sakata hili. Ni mtu aliyekuwa anafanya kile anachojua na ni MSALITI.

CHADEMA isipoteze nguvu na MUDA kumtetea huyu MSALITI, kwa maana mwisho wa siku ATAKIRI na CHADEMA itashindwa kesi kwa KISHINDO na NDIO itakuwa MWISHO WAKE.
 
Asante mkuu kwa kuweka bayana hili suala la namba.

Binafsi naona CHADEMA, kwa mara nyingine tena wamefanya "wrong move".

Matamko na press conference zimezidi mpaka mwelekeo haueleweki. Kila kiongozi anazungumza anavyojua yeye. Ni aibu kwa chama kinachojinasibu kuwa makini.

Ulitueleza hapa kuwa mmekubaliana kuwa katika suala la kesi ya Lwakatare mzungumzaji kwa niaba ya chama atakuwa ni Mh. Lissu peke yake. Lakini haijapita hata wiki Marando naye anakuja na vioja vyake.

Umakini wa taasisi yoyote ujidhihirisha wakati wa majaribu. Katika hili sio siri Chadema mumefeli.

Kwenye ukweli lazima tuelezane wazi wazi.

Suala lipo mahakmani, kama mna ushahidi substantial si muupeleke mahakamani.

Au ndo chama kinatafuta public sympathy?

THINK AGAIN... uamuzi wao wa kuja na hizi taarifa uta pre-empty any stupid move ambayo walengwa walikuwa wanafikiria kutoka nayo.
 
kuna tamko umesoma, au umetumwa kuja kupima upepo....

mungu bariki tanzania no 2
mungu bariki chadema
 
CHADEMA MUOGOPENI MUNGU

Muendelezo wa matamko yasiyokuwa na mashiko ya chadema juu ya mambo mbalimbali nchini sasa yanapaswa kupuuzwa kwani wanajaribu kuwahadaa wananchi. Wanatoa Majibu mepesi kwenye maswali magumu ambayo wanaharakati na wapenda maendeleo wa nchi hii wanauliza mathalani kwa nini chama kinachojiita CHA demokrasia Leo hii kimekuwa kinakandamiza demokrasia mfano 1. Pindi mh Zitto alisema atagombea uraisi kupitia chadema kukajitokeza kundi la watu ndani ya chama hicho wakasema Zitto anakivuruga chama na wakati huo huo mwenyekiti aw chama hicho akawatangazia watu wa KARATU kuwa Mungu akimpa uhai DKT SLAA ndiye atakuwa mgombea wa uraisi!! Watu wanajiuliza Mchakato wa kumpata SLAA ulifanyika lini, wapi, kwa katiba ipi?
Aidha pia wakati Watanzania wakiwa na msononeko, mfadhaiko wa moyo kuwa chama kinachojipambanua kuwa kinapigania maslahi ya wananchi kimegeuka kuwa TISHIO kwa umma, kinapanga na kuratibu na kutekeleza mauaji ya watu wasio na hatia!! Video clip iliyotapakaa kila kona ya websites za mitandao mbalimbali inaonyesha kuwa KIONGOZI wa juu wa chadema anayeshughulika na masala ya ulinzi na usalama bwana Lwakatare anapanga namna ya utekelezaji wa mauaji ya WAANDISHI habari ambao wao kwao ni tishio kwa uhai wa CHADEMA! Lakini pia anaelezea namna mipango mingine ya mauaji yaliwahi kupangwa na kwa namna hayakuweza kuzaa matunda Kama alivyosema swala la Igunga, na Iringa. Hizi ni tuhuma nzito ambazo zinahitaji tafakuru ya kina ya wananchi juu ya usalama wao na ni nini hasa maana ya dhana ya demokrasia ambayo inaendeshwa na vyama pinzani!
Tamko la CHADEMA kupitia kwa mwanasheria wake bwana MARANDO ni dhahiri chama hicho kimepoteza dira, kinamchoko wa kifikra na sasa kinatafuta kila njia na hila kijisafisha machoni mwa Watanzania kuwa sio chama cha kigaidi. Kama bwana marando anaushaidi wa kimawasiliano ya watu anaohisi wametengeneza clip ya Lwakatare ( ugaidi) ni vyema akapeleka ushaidi huo mahakamani kwani ndipo Haki utafutwa na kupatikana na aache kuwahadaa wananchi kwa matamko yasiyokuwa na tija. Watanzania wanaimani na Mahakama yao hata chadema wameshawahi kukiri wanaimani na Mahakama kwani hata wao wamekuwa wakishinda kesi nyingi tu kupitia Mahakama lakini wakati mwingine wanasema Mahakama si Huru.

RAI yangu kwa Chadema
Kuitisha kikao cha haraka kwa viongozi wa juu wa chama kutathimini, kutafakari maamuzi yake ya kupanga, kuratibu, na kutekeleza mateso ya kigaidi,kinyama Kama sera ya kuhadaa wananchi kuwa Ccm na vyombo vya dola vinapanga mauaji, na Mateso ya wapigania Haki! Kwani ukweli sasa umejulikana. Pili viongozi wa juu aw chadema watubu na kuomba radhi kwa Watanzania juu ya mipango yake ovu ya mateso na mauaji na mwisho kabisa waombe kwa Mungu wawe na HOFU YA MUNGU.
 
ndugu zangu wana jf

namba hiyo iliyotajwa hapo juu imewahi kuwa namba yangu ya simu. namba hii nimeacha kuitumia toka mwezi juni/julai mwaka 2012. hata hivyo namba hii bado inaonekana kwenye businesscard yangu na kwenye email zangu sehemu ya anuani. Namba hii haijawahi kuwa ya zoka. Imewahi kuwa ya zitto zuberi kabwe peke yake. namba hii haitumiki toka katikati ya mwaka 2012.

kama jf inataka kuthibitisha hili waunde jopo la wanajf watakaopata taarifa za namba hii popote wanapoweza kupata.

Mambo 2, ama namba hii imewekwa kwa bahati mbaya kwenye tamko tajwa au imewekwa makusudi kwa sababu maalumu zenye lengo la kutoa ujumbe fulani kwa watu.

Kwa namna namba hii ilivyochomekwa kwenye tamko hili au hapa jf au vyote kwa pamoja, ni dhahiri kuna juhudi za kunihusisha na upuuzi huu wa ugaidi na unyama dhidi ya binaadamu.

Napenda kusisitiza kwamba, sihusiki kwa namna yeyote ile katika kuwaza, kupanga au kutekeleza mipango yeyote ya kudhuru mtu ama kwa njia za kigaidi au za kijinai. Sihusiki kwa namna yeyote ile kupanga mpango wowote ule wenye lengo la kuhusisha chama changu na vitendo vyovyote vya kigaidi au kudhuru mtu yeyote yule. Juhudi zozote zinazofanywa na maadui wa chama changu za kunihusisha na mambo haya zitashindwa kwani siku zote ukweli huwa bayana.

Napenda kuweka wazi kwamba mhariri wa mwananchi ndugu dennis msacky ni rafiki yangu wa karibu sana. Ninaamini kabisa kwamba katika suala hili dennis msacky ni victim. Juhudi zozote zile za kutaka kumgeuza 'victim' kuwa mtuhumiwa lazima zitashindwa tu kwani siku zote haki hutamalaki.

Mtu yeyote anayetaka kutumia urafiki wangu na dennis msacky kutaka kujifurahisha kisiasa ajue kuwa furaha yake hiyo itakuwa ni ya muda mfupi sana maana ukweli ukidhihiri atapata aibu kubwa sana.

Ni muhimu sasa mambo haya tuiachie mahakama itende haki.

mbona unarudiarudia kwamba line uliacha kuitumia katikati ya mwaka jana?
Msacky hawezi kuwa adui wa chama chako hata kama ni rafiki yako?
 
mbona unarudiarudia kwamba line uliacha kuitumia katikati ya mwaka jana?
Msacky hawezi kuwa adui wa chama chako hata kama ni rafiki yako?

maadui wa chadema wanapaswa kutekwa na kuteswa? Look at u
 
tulieni dawa iingie vizuri mamburula...mmeingizwa choo cha kike na shushushu marando ambaye anakula mshahara wa serikali hata hamshtuki mnapiga mayowe tu hapa

rafiki hapa ni jamiiforum sio facebook, nimemuuliza swali ZK sasa wewe unakuja na maneno yako ya udaku. unapotaka quote watu jaribu kuwa selective na aina ya watu unao wa-quote.
 
tamko la chadema kuhusu njama za kukichafua zinazofanywa na genge la viongozi wakuu wa ccm na vyombo vya dola,
limetolewa jijini dar es salaam leo, machi 14, 2013 na mjumbe wa kamati kuu na mwanasheria wa chama, mh. Mabere nyaucho marando

ndugu waandishi wa habari;
leo tumewaita hapa ili kuwaomba mtufikishie ujumbe kwa watanzania, kwamba nikiwa mwanasheria na mtu ambaye nimepata ujuzi wa kazi za ushushu, nimefanya uchunguzi matukio haya ya utekaji na utesaji na kugundua mambo mengi mno.

Uchunguzi huu nimeufanya kabla na baada ya kukamatwa kwa mkurugenzi wetu wa ulinzi na usalama, willifred muganyizi lwakatare, ambaye hivi sasa anashitakiwa mahakamani kwa tuhuma za kupanga ugaidi.

Nimefanya hivyo kwa kuangalia maslahi mapana ya taifa langu na chama changu. Katika uchunguzi wangu huo, nimegundua mambo mengi ikiwamo kuwapo kwa genge la watu ndani ya serikali na chama cha mapinduzi (ccm), wanaopanga mipango hii ya kishetani na kisha kuwasingizia watu wengine.

Angalieni mfano huu: Unaoitwa na polisi na mwigulu nchemba, “mkanda wa lwakatare” unadaiwa uliwasilishwa jeshi la polisi desemba mwaka jana. Lakini jeshi hilo halikumkamata yoyote wala kumhoji, hadi pale mwenyekiti wa jukwaa la wahariri, absalom kibanda, alipovamiwa na kuumizwa.

Aidha, nchemba amedai kumiliki video ile desemba mwaka jana, lakini rekodi hiyo iliwekwa kwenye mitandao ya kijamii (youtube na jamii forum) baada ya kutekwa kwa kibanda. Hapa mtu makini anaweza kujiuliza, hiki kimelenga nini?

Kwamba genge hili la kina nchemba na wenzake, walipanga kumteka kibanda, wakatimiza lengo lao hilo, baadaye wakaingia kwenye plani b ya kutaka kuihusisha chadema. Wakamtumia ludovick joseph rwezahula ambaye ni mshitakiwa wa pili katika kesi ya lwakatare, kufanikisha mkakati wao huu wa kishetani.

Ndugu waandishi wa habari;
huu ni mchezo mchafu na wahatari mno ambao kwa vyovyote vile, haupaswi kuvumiliwa. Kuanzia sasa nimeamua kwa dhati kabisa, kukomesha mchezo huu ambao unahatarisha uhai wa taifa letu.

Kwa kuanzia, kesho jumatatu, nitaongoza jopo la mawakili sita wa chadema kumtetea bw. Lwakatare. Wenzangu wengine katika kesi hii, ni profesa abdallah safari, tundu lissu, edson mbogoro, peter kibatara na nyaronyo kicheere. Huko mbele tutaongeza mawakili wengine, akiwamo mmoja anayewekwa na familia ya lwakatare.

Ndugu waandishi wa habari;
mnaweza kujiuliza, kwa nini chadema kimechukua uamuzi huu wa kuweka kundi kubwa la wanasheria katika kesi hii ya lwakatare? Jibu ni kwamba tumegundua kuwa kesi hii imefunguliwa kwa lengo maalum la kuidhoofisha chadema na kuinusuru ccm ambayo inakabiliwa na dhahama ya kushindwa katika uchaguzi mkuu ujao kutokana na kushamiri kwa makundi.

Hivyo wameamfungulia kesi lwakatare, kwa lengo la kutaka kuaminisha umma kuwa chadema ni chama cha magaidi, kinapanga ugaidi na hivyo kichukiwe. Hilo ndilo lengo lao. Basi!

Ndugu waandishi wa habari;
pili, nitakwenda mahakamani kuwasilisha ombi maalum la kuomba amri ya mahakama kuagiza makampuni ya simu za mkononi kuwasilisha mahakamani statement za simu za watu kumi (10) ili kusaidia mahakama kutenda haki na jamii kujua ukweli wa mambo haya.

Watu ambao nitaomba mahakama itoe amri ya kuletwa taarifa zao simu
na meseji (sms) ni naibu mkurugenzi wa usalama wa taifa nchini (tiss), jack zoka, anayetumia simu na. 255756xxxxx, naibu katibu mkuu wa chama cha mapinduzi (ccm), mwigulu lameck nchemba, anayetumia simu tano zikiwamo 0754 xxxxx, 0757 xxxxx, 0714 xxxxx na 0787 xxxxx na ludovick joseph rwezahula, ambaye simu zake ni, 0715 xxxxx na 0753 xxxxx.

Mwingine ambaye mawasiliano yake yanahitajika, ni waziri wa mambo ya ndani ya nchi, emmanuel nchimbi, anayetumia simu na. 0754 003388, mhariri mtendaji wa magazeti ya mwananchi, dennis msaky anayetumia simu mbili, 0655 xxxxx na 0764 xxxxx na bw. Sinbad mwagha, ambaye ni afisa wa idara ya usalama wa taifa, anayetumia simu 0754 xxxx.

Wengine, ni bw. Shaali ali, afisa mwinge wa usalama wa taifa anayetumia simu na. 0716xxxxx, saumu k. Malungu, mwenye kutumia simu 0719 xxxxx na 0789 xxxxx, simu mbili zinazotumiwa na mtuhumiwa mkuu wa utekaji wa dk. Steven ulimboka, bw. Ramadhani abeid igondo ikiwamo 0713 xxxxx, simu za bw. Ridhiwani kikwete ambazo ni 0754 xxxxx, 0784 xxxxx, simu ya dr. Steven ulimboka, ambayo ni 0713 xxxxx, pamoja na simu zote tatu za willifred lwakatare, ambazo ni 0786 xxxxx, 0713 xxxxx na 0758 xxxxx.

Ndugu waandishi wa habari;
mtu mwingine muhimu nitakayeomba mahakama itoe amri ya kutolewa kwa taarifa zake, ni mwandishi wa habari na mpigapicha wa magazeti ya serikali, muhidini issa michuzi. Mwandani huyu wa ikulu, ndiye aliyeandika ujumbe kwa njia ya emeili kuipongeza ofisi binafsi ya rais (obr) na usalama wa taifa kwa kupata video ya lwakatare.

Pongezi za michuzi kwa tiss ndizo zinanisukuma kuiomba mahakama kuagiza kupatikana taarifa zake. Michuzi anaipongeza tiss kwa kuibua njama za wahalifu, lakini mimi ninajua tiss ikipata njama za aina hiyo haraka inapeleka ushahidi polisi, lakini huu wa lwakatare ulipelekwa youtube, badala ya kwenye vyombo vya sheria.

Maneno ya michuzi kwamba ni tiss imeibua hiyo video yanathibitisha ushiriki wa tiss kwenye mchezo huo mchafu, na kwamba chadema kinajua kuwa michuzi alishirikiana na watu wa usalama wa taifa katika kazi hiyo chafu. Software za video (editing) walizotumia zilitoka kwake. Fedha ya kuandaa hiyo video zilitoka usalama na ikulu. Tunajua kuwa wale vijana wa ada estate na yule jamaa anayempelekea kigogo wa jamii forum, walilalamika sana kwa mmoja wa wamiliki wa jf.

Ndugu waandishi wa habari;
chadema kinajua kuwa mmoja wa watuhumiwa hawa, mwigulu nchemba anafanya mipango na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya vodacom ili kumsaidia kufuta taarifa zake. Nachukua nafasi hii, kuionya kampuni hiyo kuacha kucheza mchezo huo kwa kuwa ni kinyume cha sheria za mamlaka ya mawasiliano (tcra).

Tunahitaji mawasiliano haya kwa kuwa mwigulu – zinaonyesha mtuhumiwa huyo akifanya mawasiliano mfululizo na ludovick, yakiwamo yale ya tarehe 4 machi 2013. Hii ilikuwa siku moja kabla ya kibanda kutekwa.

Ndugu waandishi wa habari;
hawa niliowataja ni watu muhimu sana katika upangaji wa mkakati wa utengenezaji wa video ya lwakatare na vitendo vya kihalifu vya utekwaji wa kibanda na tukio la kutekwa na kisha kutupwa msutuni kwa mwenyekiti wa jumuiya ya madaktari nchini, dr. Steven ulimboka.

Kwa mfano, simu ya mwigullu nchemba, namba 0714 xxxxx, 0756 xxxxx na 0757 xxxxx, zimefanya mawasiliano mara kadhaa na ludovick joseph, saumu k. Malungu, jack zoka, ali shaali na ramadhani ighondo. Mawasiliano hayo yalifanyika katika kipindi ambacho mgomo wa madaktari ulishamiri; baadaye yakarudi tena kati ya 26 desemba mwaka jana na 15 machi mwaka huu.

Miongoni mwa mawasiliano ambayo tunaona yanahusika na ujambazi huu, ni yale ya 28 desemba, siku ambayo mkanda wa lwakatare umerekodiwa; tarehe 4 hadi 6 machi 2013, siku moja kabla ya kibanda kutekwa na yale ya usiku wa manane (saa 8:17) wa 13 machi 2013, ambako mchana uliofuata lwakatare alikamatwa.

Huyu mwagha ndiye aliyekuwa anatumika kuwasiliana na saumu malungu, ambaye tulimtaja kuwa ndiye aliyekuwa amepewa kazi na mwigulu na usalama wa taifa, kurubuni vijana wetu kwa fedha ili kutoa ushahidi wa uongo juu ya video ya lwakatare.

Vilevile, mawasiliano ya mwiguluna mwagha, katika kipindi hicho nayo tunayahitaji. Kwa sababu, huyu mwagha anayetumia simu 0754xxxxx, mbali na kuwasiliana na mwigulu, ndiye aliyekuwa anawasiliana na mmoja wa waliomteka ulimboka; na ndiye aliyewasiliana na saumu kati ya 20januari na machi 6 mwaka huu.

Ndugu waandishi wa habari;
ludovick alifanya mawasiliano ya mwisho na joyece agustine, ambaye anatumia simu na. 0717 xxxxx, mawasiliano ambayo yalifanyika saa 5:13 usiku. Hiyo ndiyo ilikuwa simu yake ya mwisho usiku huo; katika siku hiyo ludovick aliwasilisna na joyce mara tisa kuanzia saa 12: 54 asubuhi.

Kwa mujibu wa taarifa za kwenye mtandao wa jamii forum, ambako video ya lwakatare ilitumwa, ludovick alikamatwa machi 15 mwaka huu. Hata hivyo, rekodi katika simu yake na. 0715 xxxxx inaoyesha 17 machi ludovick alifanya mawasiliano na joyce augustino. Mawasiliano hayo yalifanyika saa 8: 9 usiku, wakati inadaiwa na polisi alishakamatwa.

Naye mhariri wa mwananchi, bw. Msaky ambaye anatajwa kutaka kutekwa na ludovick na lwakatare, amekuwa na mawasiliano kadhaa na ludovick – mtu anayepanga kumteka. Ludovick na msaky walifanya mawasiliano mfululizo kati 27 desema 2012, siku moja kabla ya video ya lwakatare haijarekodiwa na 7 machi siku moja baada ya kibanda kutekwa.

Msacky alitumia simu zake hizo mbili (0764 xxxxx na 0655 xxxxx) kuwasiliana na ludovick, huku ludovick akitumia 0753xxxxx. Mawasiliano ya 31 desemba yalifanyika ludovick akiwa tegeta, jijini dar es salaam. Mawakala hawa wawili wa usalama wa taifa (ludovick na msaky), walikutana 31 desemba 2012, katika hoteli ya tamal, mwenge jijini dar es salaam.

Ndugu waandishi wa habari;
baada ya kupitia taarifa hizi za mawasiliano ya simu za mwigulu nchemba, ludovick joseph, ramadhani ighondo na saumu malungu tumegundua yafuatayo: Kwamba, ramadhani ighondo, amefanya mawasiliano mara nyingi na mwigulu, mwagha na zoka; naye mwagha amefanya mawasiliano na mwigulu na saumu; naye saumu amefanya mawasiliano na mwagha, mwiguluna shaali ali, ambaye ni afisa usalama wa taifa.

Tumegundua vilevile, kuwapo mawasiliano kadhaa kati ya ludovick na msaky; ludovick na mwigulu; msaky na nchimbi; msaki na mwagha, samu na mwagha na ramadhani ighondo abeid, anayetuhumiwa kumteka dk. Ulimboka na mwanga na mwigullu.

Tumegundua pia kuwapo mawasiliano kati ya ulimboka na ramadhani; zoka na ighondo na ridhiwani na ighondo. Mawasiliano haya yalifanywa mfululizo usiku wa juni 2012 siku ambayo dk. Ulimboka alitekwa.

Tumepata kufahamu pia kwamba baadhi ya watu waliotajwa na gazeti la mwanahalisi kuwa waliwasiliana na ighondo usiku wa juni 26, mwaka 2012, wamefanya mawasiliano pia na mwigulu, mwagha na shaali ali.

Ndugu waandishi wa habari;
mwagha ni afisa usalama wa taifa anayefanyakazi makao makuu ya idara hiyo. Ndiye yule anayetumika kuendesha michezo ya kuhonga wanasiasa wa ccm na upinzani. Ni mwagha anayepanga wabunge na kuwapanga waongee nini kwa maslahi ya ccm. Ushenzi wote anaoongea mwighulu bungeni, hupewa na mwagha kwa maelekezo ya jack zoka.

Naye shaali ndiye aliyekutana na afisa wetu wa usalama, ahmed sabula na mwenzake, machi 29 mwaka huu katika hoteli ya see cliff jijini dar es salaam. Katika mkutano huo kati ya sabula, kijana wetu wa usalama na afisa usalama wa serikali bw. Shaali alitaka sabula akubali kutumika kwa kutoa taarifa za vikao vya chama, kuwasilisha kwake nyaraka za kamati kuu na kueleza mipango ya chama katika kesi ya lwakatare.

Kwenye mpango huu, afisa huyo wa usalama wa taifa ambaye ninamfahamu vizuri, alimuahidi sabula kiasi cha sh. Milioni 30 na kwamba fedha hizo angelipwa wiki iliyopita. Aliahidiwa pia kwamba kila nyaraka atakayopeleka atalipwa ujira.

Aidha, sabula aliahidiwa kulipwa shilingi 500,000 (laki tano) kila mwezi; afisa wetu huyu ameripoti tukio hilo kwa viongozi wake wa chama. Yule mwenzake aliandaliwa kuwa shahidi wa kesi ya lwakatare; aliambiwa akikubali dili hiyo atalipwa kila mwezi sh. 500, lakini akaombwa kuwa mvumilivu kwa kuwa atalazimika kupotea kwa miezi kama mitano hadi sita.

Ndugu waandishi wa habari;
kitendo cha mwigulu kuwasiliana ramadhani ighondo, mwigulu kuwasiliana na ludovick, saumu kuwasiliana na mwigulu, ighondo kuwasiliana na ulimboka, zoka kuwasiliana na ighondo, tena katika muda uleule ambao ighondo amewasiliana na ulimboka na saumu kuwasiliana na mwagha, ni uthibitisho tosha kwamba usalama wa taifa wako nyuma ya mipango hii ya michafu ya kupanga utekaji na kisha kutaka kukichafua chadema.

Aidha, kitendo cha ludovick kuwasiliana msaky; ighondo kuwasiliana na mwagha, ridhiwani kikwete kuwasiliana na ighondo, tena kila baada ya ighondo kuwasiliana na ulimboka na jack zoka, ni uthibitisho mwingine kuwa genge hili la wahalifu linashirkiana na baadhi ya watu kutaka kuangamiza taifa.

Ni uthibitisho tosha kwamba hawa ndiyo wanaowahonga wanachama wa chadema na watu wengine ili watoe ushahidi feki dhidi ya lwakatare, na kwamba ni usalama wa taifa walioandaa ile video uchwara inayopigiwa chapuo na mwigulu.

Ndugu waandishi wa habari;
chama cha mapinduzi kinajua kwa hali ya sasa hakiwezi kushinda uchaguzi wa mwaka 2015 huku chadema ikiwa katika hali nzuri ya kisiasa tunayoiona sasa. Wanajua kabisa ccm imegawanyika, kundi lolote litakalopita ndani ya ccm, litahujumu kundi jingine. Ni kama ilivyotokea uchaguzi mdogo wa arumeru mashariki.

Ndiyo maana wanapanga kila mbinu kutaka kuiangamiza chadema. Nasi tunasema katu hatutakubali kuona chadema kinakufa. Tutapambana usiku na mchana. Juna na mvua. Hadi tushinde hila hizi.tunawaambia wanachama wetu na wale wanaotuunga mkono, chadema ni chama kikubwa. Kina mtandao kila mahali, kuanzia ikulu hadi polisi; na hivyo hakitakufa au kuzorota kwa mambo ya kupikwa.

Ni imani yangu kwamba amri ya mahakama itawafichua wote hawa ni kuirudisha tanzania katika amani yake. Ni lazima tufikike mahala watu hawa wafahamike mbele ya umma, tunataka wafahamu kuwa maisha ya mwanadamu yana thamani kuliko siasa chafu na ufisadi wanaouendeleza.

Nawashukuru kwa kunisikiliza.

Mabere marando,
dar es salaam

kazi ipo hii kama kweli bac tunakoenda ni kubaya. Dat why baadhi ya watu walikuwa wanatabiri kifo cha cdm, kumbe sio utabari ni hujuma, kweli mungu na waungwana shetani na wahuni
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom