TAMISEMI kuweni na utu japo kidogo

APA CHICAGO

JF-Expert Member
Oct 20, 2019
259
293
Leo nikiwa zangu Maeneo ya Mtaa wa Isevya mjini Tabora nimekutana na mlinzi mmoja wa shule ya sekondari ya serikali akaniambia ya kwake ya moyoni kuwa ana miezi miwili sasa hajalipwa yaani wa Saba na wa nane.

Akasema mhasibu wa shule Kila akimpigia anajibiwa mfumo haujafunguliwa wa kuwawezesha kulipa.

Maswali niliyojiuliza ni haya hivi hao TAMISEMI wanafikilia shule zikifungwa na walinzi wanakuwa likizo hivyo hawalipwi?

Je, wao hapo TAMISEMI wanaweza kufanya kazi bila kulipwa mishahara miezi miwili 2 na kuendelea?

Maofisa wa TAMISEMI mnaoshugulika na mifumo ya malipo mashuleni acheni urasmu usio na maana na ubinafisi kumbukeni Kuna watu wengi tu wanategemea vijisenti ili wagange Maisha Yao na familia zao kama huyu baba niliyekutana naye Tabora.

Bashungwa ongilia kati hili kama ni kweli mfumo haujafunguliwa.
 
Mkuu test man, we acha tu baba wa watu alikuwa anaongea na maumivu kweli nikawza sana hivi wangekuwa wao ingekuwaje.Yaani unafanya vitu bila kujali Kuna watu Wana athirika na maamuzi yako.
 
Ombi kwenu viongozi wa Jamii forum huu Uzi uwekeni uonekane siuoni ili wahusika wauone wapate ujumbe.Maana hofu yangu kubwa watu wakishajifungia Kwenye vyumba vyenye viyoyozi wanasahau kuwa Kuna watu wanashida Nje.
 
ni kweli hata mimi bosi wangu huwa anachukua tenda za serikali.jamaa toka mwezi wa sita mwishoni aliniambia mifumo inafugwa mwezi wa saba yaani hadi leo anasema ado haijafunguka na yeye hajalipwa
 
Back
Top Bottom