TAMISEMI kama mmeshindwa kuandaa mifumo mizuri ya watu kuomba ajira ni bora mkarudisha zama za posta. Mfumo umekuwa usumbufu

gimmy's

JF-Expert Member
Sep 22, 2011
3,283
3,274
Wanabodi salaam!
Serikali kupitia Tamisemi wametangaza ajira tar 20 mwezi huu kwa kada ya afya na elimu.Tunaishukuru serikali kwa hizi ajira kwani kimsingi hali ya ukosefu wa ajira imekuwa janga nchini.

Tatizo lililopo ni mfumo(system) kwenye uombaji hizi ajira unamatatizo yanayopelekea watu wengi kushindwa kuomba hizi ajira na hapa ndipo nimeona nimshuri Bashungwa kama wameshindwa kutengeneza mfumo mzuri wa watu kuomba ajira ni bora waturudishe posta ili kutoa fursa sawa kwenye uombaji hizi ajira.

Ukiingia kwenye a/c ya tamisemi instagram utaona watu wengi wenye malalamiko lakini wanakosa msaada,tamisemi wametoa namba ya simu kwa yeyote mwenye changamoto lakini namba haipatikani.

Kwenye huu mfumo wao,ukikosea kujaza na bahati mbaya ukasubmit hakuna namna yaku edit hata kama ni muda huohuo,ni mfumo wa hovyo sana.

Wapo watu wengi kozi zao hazipo kwenye mfumo na wanapo jaribu kuwataarifu tamisemi kwenye a/c yao instagram wanawajibu kwakuwapa namba ya simu ambayo haipatikani wakiwataka wawapigie ili wawakwamue.

Naomba sana serikali kwanza watatue hizi changamoto lakini pia waongeze muda watu wote wapate fursa yakuomba ajira kwani kwachangaoto za huu mfumo wiki mbili walizozitoa kwa watu kuomba hizi ajira hazitoshi.
 
Yap mfumo unazengua lakini katika hyo changamoto ya kuedit taarifa ipo unachotakiwa kufanya ni kama unatumia simu inatakiwa uiseti kwenye mfumo wa desktop kwa kubonyeza vitufe vitatu vya kulia kwenye browser unayotumia na utaweza kufanya editing
 
Wanabodi salaam!
Serikali kupitia Tamisemi wametangaza ajira tar 20 mwezi huu kwa kada ya afya na elimu.Tunaishukuru serikali kwa hizi ajira kwani kimsingi hali ya ukosefu wa ajira imekuwa janga nchini.

Tatizo lililopo ni mfumo(system) kwenye uombaji hizi ajira unamatatizo yanayopelekea watu wengi kushindwa kuomba hizi ajira na hapa ndipo nimeona nimshuri Bashungwa kama wameshindwa kutengeneza mfumo mzuri wa watu kuomba ajira ni bora waturudishe posta ili kutoa fursa sawa kwenye uombaji hizi ajira.

Ukiingia kwenye a/c ya tamisemi instagram utaona watu wengi wenye malalamiko lakini wanakosa msaada,tamisemi wametoa namba ya simu kwa yeyote mwenye changamoto lakini namba haipatikani.

Kwenye huu mfumo wao,ukikosea kujaza na bahati mbaya ukasubmit hakuna namna yaku edit hata kama ni muda huohuo,ni mfumo wa hovyo sana.

Wapo watu wengi kozi zao hazipo kwenye mfumo na wanapo jaribu kuwataarifu tamisemi kwenye a/c yao instagram wanawajibu kwakuwapa namba ya simu ambayo haipatikani wakiwataka wawapigie ili wawakwamue.

Naomba sana serikali kwanza watatue hizi changamoto lakini pia waongeze muda watu wote wapate fursa yakuomba ajira kwani kwachangaoto za huu mfumo wiki mbili walizozitoa kwa watu kuomba hizi ajira hazitoshi.
Kichaka eti ni waombaji ni wengi
 
Haya mambo ya internet watz tumeyakimbilia mapema lakin serikal bado haijapata wataalam wazuri
Siyo kweli kinachofanyika ni kwamba TAMISEMI wanadungu zao ambao wamepeleka majina manually hawa wakuomba online ni geresha tu sana sana kwenye watu laki 2 waliomba manually wanaweza kuchukuliwa 500 tu wengine wote ni offline
 
Tuwe wakweli mfumo hauna shida tatizo lipo kwa muombaji mfano mimi nimetumia dk 45 kukamilisha ila cafe niliofanyia kazi kuna waombaji hawana namba za nida,wengine wameshindwa kujibu maswali ya nida kama vile jina la mwisho au la kati la mama n.k. pia wengine yanatofautiana majina ya vyeti vya taaluma.nida na kuzaliwa na wengine hawana namba za nida kwa kifupi mfumo uko poa kwa sasa ila wazembe ndio wanalalamika ili kuukumbatia uzembe wao
 
Usijione wewe ni fundi kuliko wengine eti kwasababu tu umefanikiwa kukamilisha kwa haraka.Zipo kozi nyingine ni kweli hazikuepo kwenye mfumo na wameziweka baada ya watu kulalamika.

Hii nchi ngumu sana wewe endelea na utetezi.Kwenye haya mambo ya ajira ni kawaida sana ukakuta wakati wewe umefunga kwa kutokula na kunywa ukimuomba Mungu wenzako kupitia ndugu huko TAMISEMI wanashinda baa wakisubiri kupangiwa kazi.

Nimalizie kwakukusisitiza kwamba kama umebahatika kujaza mapema isiwe kigezo chakuona wanao fail sababu hawajui nini chakufanya.
 
mimi huwa siapply mapema huu mwaka wa saba natuma application maana ni mhanga wa ajira toka 2015.pia baadhi ya changamoto kawaida kujitokeza kama hizo za kozi ndio maana wametolea ufafanuzi kozi zinazoonekana ndizo walizopata kibali.vipi ulisoma bachelor of education administration from UDOM
 
Mode nisaidie rekebisha heading "imekua"

Wala usijisumbue sana, hizo nafasi zimetangazwa kwenye mtandao ili kukidhi matakwa ya kisheria tu, lakini tayari hizo nafasi zimeshapata watu muda mrefu.
 
mimi huwa siapply mapema huu mwaka wa saba natuma application maana ni mhanga wa ajira toka 2015.pia baadhi ya changamoto kawaida kujitokeza kama hizo za kozi ndio maana wametolea ufafanuzi kozi zinazoonekana ndizo walizopata kibali.vipi ulisoma bachelor of education administration from UDOM
Bachelor degree in adult and continuing education imewekwa baada ya malalamiko haikuwepo mwanzoni,sasa iweje wapate kibali baada ya malalamiko?
 
Tuwaambie vijana ukweli sio kuwadanganaya danganya daily:
1.Hakuna serikali inayoajiri zaidi ya graduate 10% hivyo 90+ wanatakiwa wengi wakaajiriwe na sekta binafsi na waliojaaliwa wakajiajiri
2.Nchi yenu imeua ukuaji wa sekta binafsi kwa mikodi ,urasimu ,wivu na rushwa.
3.Hata achaguliwe malaika hakuna namna ya kurudisha ajira hata kwa asilimia 10 ya wote walio mtaani
4.Degree si kitu vijana wenzenu dunian walishajua ,Kenya hapo ma baamed wengi ni graduates wanalipwa 150k ya tanzania,nigeria wamachinga na tax drivers wana masters
5.katika walioandika maombi ile taasisi ya herufi tatu ya kusanya hela maombi 50000 wameajiliwa 200 ,inamaana katika vijana 100 anaeajiliwa ni mmoja tu serikalini .
USHAURI
Umri unaenda na uchumi wetu hauna dalili kuwa utafufuka kiivyo,wanasiasa wanasema mkafuge kuku mara fungueni kampuni huko ni kuendelea kuwaaminisha degree ni archievement kubwa na unastahili makubwa ,Mimi nawaambia jishushe mtaji wa maskin ni nguvu na akili zako ,kama mdada tafuta hata laki 2 uza chakula stend chapat maandaz wali wa cheap onesha usomi wako kwa kuwa msafi kuzidi wenzio customer care etc mwanaume nunua baskeli weka group la wasap sambaza mkaa uliouweka kwenu chumba kisichotumika waundie group uchukue oda
Mafuta hujitenga watu ambao wana mitaji ila hawaoni mtu makini wa kusimamia ninwengi ila mtu anataka aanzishe mantilie ya mill 40 ya kupika kuwapa wamama wakauze masherehe akuajili ww na tai yako ???
Vijana wanaoishia la saba au form 4 wakafeli wanautumia huu ushauri,wakishamaliza form 4 akapiga 4 ya mwisho anazama mtaani kuwa boda boda anajenga network ya kujuana na watu wengi anajichanga miaka 3 ananunua boda yake anajiingiza udalali na uchawa mara kapata mcholo wa kuchukua vitunguu iringa kuleta dar miaka mitano wakati ww unalia ajita zina rushwa mara mifumo mibovu mwenzio anamke na watoto 2 ,kajenga kanyumba kibulugwa na ameshanunua uwanja wa kujenga lodge yake
Ww unaendelea kuchambua vita ya ukraine kwa kina na iphone yako ya mtumba huku ukinunuliwa bia na hawa waliofeli form 4 maana unataka kujenga ghorofa kwa kuanzia ghorofa ya 3
 
Back
Top Bottom