NBS hawajazingatia vigezo vya human machine interaction katika mfumo wa uombaji wa kazi za muda mfupi za Sensa

MlekwaKik

Member
May 18, 2022
8
6
NBS wanawachezea akili Watanzania kwa kutumia uelewa wao mdogo katika mambo ya Technology na Haki za Watumiaji wa Mifumo mbali mbali ya huduma. NBS wamefanya uhuni kwa kutozingatia vigezo vya Human Machine Interaction (Usability and User Experience (UX)) katika mfumo wao wa kuomba ajira za muda za Sensa.

Kuna mapungufu yafuatayo katika Mfumo huo ambayo ni ya upande wa Developers na sio upande wa Internet Connectivity issues:
  • Mtumiaji akishajaza Mkoa, Wilaya, Halmashauri, Jimbo, kuna Taarifa za Tarafa, Kata na Mtaa zinachelewa sana kuonekana na inachukua muda kama sekunde 30 kwa baadhi ya Mikoa sio yote. Hiyo shida ipo kwenye Algorithms ambazo zimetumika hapo na sio Internet Connectivity. Maana ake Testing haikufanyika kisawa sawa inavyotakiwa.
  • Link ambayo mtumiaji anatakiwa kuclick ili aweze kuprint application form kwajili ya kuweka saini, ina shida ambayo ni upande wa Developers pia kutokuwa makini kuzingatia kanuni za Usability and UX.
  • Ukishamaliza kujaza form unatumiwa password kwa njia ya email, lakini kuna wakati hiyo password inakataa au username inakataa. Lakini katika Mfumo huo hakuna option ambayo mtumiaji amepewa kuweza kurecover password yake ikiwa ameisahau au anataka kuweka password ambayo ni rafiki kwake kuikumbuka, hilo ni jambo la ajabu sana na sijui Developer gani anaweza kufanya designing ya aina hiyo. (Na hili ndo tatizo kubwa Zaidi kwenye Mfumo huo)
Kwa kanuni za Human Machine Interaction hivi vitu sio sawa labda kama wametumia Junior Developers, lakini ni aibu kwa Taifa letu kuwa na Mfumo kama huo kutoka Taasisi kubwa ya Serikali kama NBS. Labda kama kuna hidden agenda nyuma ya pazia. Wameweka njia pekee ya msaada ni kupiga simu kwao, simu ambazo muda wote hazipatikani au zipo busy. Kama Google au Instagram au Facebook ambazo zinatumiwa na Watanzania karibia mil 20 zingetumia mfumo wa kwenu, sidhani kama zingepata Watumiaji wengi Duniani. Kuna Mifumo mingi sana Tanzania ambayo ni bora sana na zina mifumo mizuri ya self-help na learnability kwa Watumiaji bila kuwa na haja ya kupiga simu huduma kwa wateja.

Kuna njia nyingi sana ambazo ni user friendly za kumuelekeza Mtumiaji wa Mfumo kujisaidia mwenyewe bila kuwa na haja ya kupiga simu. Na kwa maendeleo haya ya teknolojia hapa Tanzania sidhani kama kuna mtu ambae alikaa darasani akasoma Computer Science au Computer Engineering kwa miaka 3 au 4 anaweza kuwa hajui namna ya kumpa uhuru Mtumiaji wa Mfumo wa TEHAMA katika kufikia lengo anapoingia katika Mfumo fulani wa TEHAMA.

Kwenye mfumo huo Watumiaji wanaweka taarifa kama namba zao za simu, namba za NIDA pamoja na emails zao, zingetosha kabisa kuwapa uhuru watumiaji kuweza kupata password mpya iwapo za mwanzo zinasumbua bila kuwa na haja ya kuwapigia simu huduma kwa Wateja wa NBS. Na bado usalama wa kimtandao ungekuwa haujaharibiwa kabisa. Lakini pia Watumiaji walitakiwa kupewa uhuru wa kubadirisha password na kuweka password ambazo ni rafiki zaidi kwao kuweza kukumbuka.

Sasa na ndiyo maana naita huu ni utapeli umefanywa na Taasisi ya Umma. Wanatakiwa kurekebisha hizo changamoto au kasoro na matangazo ya ajira yatolewe upya. Fikiria ni watu wangapi wanaenda kukosa hizi kazi kwa uzembe ambao sio wa kwao wala haupo ndani ya uwezo wao. Au ndo ile ile ki-Tanzania tunatangaza kazi huku tayari kuna watu wameandaliwa kwajili ya hizo kazi. Tuache kuwafanya watu kama mazombie wasio na akili timamu, hata hizi kazi za elfu 20 bado mnataka kuwanyima hawa vijana wasio na ajira mitaani. Sio sawa, NBS fanyeni jambo hapa kama kweli mnataka kutenda haki mbele za Mungu. Mfumo wenu ni wa hovyo na wala sio rafiki kwa watumiaji.
 
Nashauri waongeze muda huku wakifanya marekebisho pia ya mfumo.

 
Duh umeandika kwa uchungu sana..
Lakini kumbuka ni mfumo wa muda mfupi tu huu..
So huwezi kuwekeza nguvu nyingi kwenye temporary system
 
Duh umeandika kwa uchungu sana..
Lakini kumbuka ni mfumo wa muda mfupi tu huu..
So huwezi kuwekeza nguvu nyingi kwenye temporary system
Bado sio sawa kuwa na mapungufu ya kitaalamu, haipo sawa. Manesi wakiweka hospitali za muda mfupi katika viwanja vya maonesho huwa hawatumiii vifaa feki kupima wagonjwa. Wanaenda wakiwa full na kila kitu.
 
Back
Top Bottom