Msolid1990
Senior Member
- Apr 2, 2012
- 144
- 50
Wakuu Habari,
Leo nimeona nielezee kidogo kwa namna gani unaweza kujua uhalali wa kilometer zinazosoma kwenye gari unalotaka kununua either mkononi kwa mtu ama yard.
Hii njia haitaweza kuapply kwa magari yote kwa sababu mbali mbali ikiwemo kwamba kipindi fulani hapa nyuma magari yalikuwa yanakaguliwa hapa Tanzania na sio nchi yanakotokea kama Japan.
TBS wametoa mamlaka ya ukaguzi wa magari yote yanayokuja Tanzania kutokea Japan kampuni inayojulikana kama EAA COMPANY LIMITED(EAA Company Ltd – EAA Company Ltd), ukishanunua gari Japan kabla ya kuwa shipped litapelekwa kwenye hii kampuni na watalikagua na likikidhi vigezo vya kuingiza gari Tanzania basi gari litapatiwa Document inaitwa Certificate of Roadworthness. Hii kampuni inafanya ukaguzi pia wa Magari yanayoenda nchi nyingine kama Bahamas, Mauritius, Uganda, Zambia, Zimbabwe n.k. Kwa wenzetu wa Kenya wao shirika lao la viwango (Kenya Bureau of Standards) wanatumia kampuni inayoitwa QISJ(Quality Inspection Services Japan) kukagua magari yanayoenda Kenya.
Kwa kampuni ya EAA tunayotumia Tanzania wakishafanya ukaguzi na gari likafanikiwa kupass inspection, basi linapatiwa certificate of roadworthness. Lakini pia wana huduma ya E-certificate which means wanakuwa na hii certificate mtandaoni ambapo kunakuwa na category mbili moja ni Exporter E-Certificate na nyingine ni General Public/Client E-certificate access.
Kwa upande wa Exporter E-certificate hapa inahitaji access kuweza kuingia na kupata hiyo certificate, kwa upande wa General Public/Client E-certificate unachohitaji hapa ni Chasis number/ VIN number ya gari tu ili uweze kuona baadhi ya taarifa muhimu za hiyo gari wakati wa ukaguzi.
Sasa mojawapo ya kipengele kinachoonekana kwenye details za gari baada ya kufanyiwa ukaguzi ni kitu wanaita INSPECTED MILEAGE ambacho kinaonyesha siku gari limekaguliwa odomoter yake ilikuwa inasoma kilometer ngapi, na hii ni baada ya kampuni ya ukaguzi ya EAA kujiridhisha kwamba odomoter haijachezewa.
UKITAKA KUVERIFY GARI UNALOTAKA KUNUNUA UFANYEJE?
Niliona gari inauzwa Instagram na kulingana na taarifa za inspection inaonekana imeingiza Tanzania miezi michache iliyopita kwa kuwa kwenye mwezi wa 8 ndo ilifanyiwa inspection plus shipping days itakuwa imeingia tu juzi kati hapa, kwa hiyo lilikuwa linauzwa kama gari Jipya na kwenye plate number wameweka chasis number na wanaonyesha Milleage ni Km 48139, Lakini nilivyochukua chasis number ya hili na kuweka kwenye website ya EAA inaoenakana inspected mileage kule Japan ilikuwa ni Kilometer 165,731 kwa maana kwamba kilometer zimeshushwa kwa takribani 100,000+ lilivyoingia Tanzania.
Nitaweka picha mbili(Tangazo la instagram na pia details za ukaguzi) nikiwa nimeficha details nyingine kwa sababu ni biashara za watu.
Ni vizuri kujua uhalali wa mileage ya gari unalonunua kuepusha kuuziwa gari lenye milleage kubwa kwa bei ya gari lenye mileage kidogo.

- Tafuta Chasis number ya gari unalotaka kununua
- Ingia kwenye website ya kampuni ya EAA hapa (E-certificates)
- Kisha ingiza chasis numbe yako mara nyingi zinakuwa kwenye mfumo wa (XXXX-XXXXX)
- Kisha bonyeza kitufe cha Verify certificate, utaona details za gari ikiwemo inspected mileage