Tambaza vs Azania (that Infamous Battle)!

nyie watoto wa shaban robert mlizoea kutoka na watoto wa kihindi..Ndiyo maana mlikaa kihindi hindi sana.....mlikuwa sleki sana shaban robert na mzizima....watoto wa uswahilini mlikuwa hamuwawezi....

Mimi nilikuwa mgumu wa Tambaza. Nilikuwa nawapora hela watoto wa SRSS
 
Kwa kumbukumbu zangu ni kwamba miaka ya 90/2000's kwa Tanzania ni Tambaza walitamba saana hadi yule dogo alipokuja kujiuwa. Nilisikia alikuwa just form 3. Hawa vijana kwa kweli akili zao zilikuwa hazijakaa sawa. Kuna dogo wangu alikuwa hapo mwaka 91 na akaja niambia kituko kimoja. Wanafunzi wakiwa wamesimama wakimsikiliza headmaster, mara wakamuona nyoka kaingia kwenye shimo. Basi wengine wakakimbia na kuchukua nyasi, wengine wakaleta moto na wakamuwashia nyoka. Moto ulivyozidi nyoka akatoka na wakamuuwa. Wakamchukua hadi kwenye fance ya shule iliko barabara na wakawa wanasubiri. Ghafla wakamuona MHINDI kwenye gari na wakamrushia. Mwisho wakarudi wote kwenye mstari kumsikiliza headmaster kama vile hakikuharibika kitu.

Hivi ugomvi wa Tambaza na Mgulani Secondary nani alikuja kushinda? Maana nasikia Mgulani walianza kutumia ma MP wa pale JKT kushusha kibano kwa Tambaza. Du, Tambaza kweli walitesa.

Miaka ya 70 mwishoni, kuna binamu yangu alikuwa akisoma Iyunga na alikuwa ni mmoja ya jamaa watesaji na wanyanyasaji na fujo nyingi sana kuanzia kwenye mpira, shuleni na safarini. Kuna jamaa yake mmoja akiitwa Joel Kad**e kama sikosei alikuwa akitusimulia jinsi alivyokuwa akiogopwa. Walifanya fujo Dodoma station hadi POLISI waliitwa. Kad**e alikuwa ni kama mdogo wake jamaa maana ukimgusa tu basi utakula "vichwa".
Fujo zao kubwa kabisa ilikuwa ni pale yule Waziri wa elimu wa wakati huo, marehemu Mgonja alitangaza kuwa "wanawake mashuleni wavae suruali na wanaume kaptura". Alipokuja Iyunga alilimwa swali kama hiyo ni mila ya Tanzania na akaanza kujibu upupu basi kabla hajamaliza alijikuta kabandikwa chapati usoni.
 
Kuna machizi walikuwa wakipandishiana na makonda wanateka vi Hiace vinavyokwenda Muhimbili hospitali, basi ki Hiace kinapigwa misele mpaka shuleni, halafu kikiingia getini tu Tambaza kabla hakijasimama machizi wote wanakuwa washaruka madirishani wamekimbia, just kuwaonyesha utemi makonda.

Kuna watu walikuwa hawana akili nzuri pale.
 
v3.jpg

It will always be in my memory,

Vurugu ya mwisho tuliingia Azania na chupa za mafuta yas petrol kama mabomu, nikiwa form two.

Tukarusha mabomu mawili laboratory ya Azania, wakawahi kuizima.Mara Azania wakatoka na makwanja , tumo ndani ya senyenge zao! Kilichotokea baada ya hapo inabaki historia.

Nilikimbia jangwani mabondeni huko nikakutana na tope linanuka vibaya sana, kuna wanafunzi wa azania walikuwa huko walikula kibano.It was war-like zone

Lakini nakiri afadhali walituhamishia mikoani, maana nisingemaliza salama, umri wa kubalehe ule na kufuata mob saikoloji ungetumaliza.

Ulikuwa ukituleta darasani moto wa kuotea mbali!! makonda walikuwa wanaheshimu Tambaza bwana

Label ya shule ilikuwa kali mpaka leo sijaona mfano wake, yangu ilikuwa kijani-group two!

SAMBUKILE-TAMBAZA!!!!!!!!!!!!!!!
 
Sikonge haya wabeja mayo!...naona Julius kakimbia...hivi swali langu ni hivi kwa nini shule nyingi za wanaume watupu tanzania or mchanganyiko zilikuwa na fujo sana na kujiona ni wababe kupita kiasi...shule kama Forest/kigurunyembe enzi hizo ilikuwa inaongoza kwa ufuska,tambaza kwa fujo,Ilboru handsome boys (some-to-do)...kuna shule moja moshi/arusha pia wavulana walikuwa na fujo sana nimeisahau jina....sijui kama zile tabia za zamani hadi leo bado zipo...
 
Wabs,

Aliyepiga picha hii atakuwa amesimama karibu na kisima fulani cha zamani kilikauka kikawa kama jaa la taka.

Hiyo picha inakumbusha mbali sana, hapo mlangoni kulikuwa na kijiwe cha kutesa njuka.
 
Mimi nilimaliza pale Tambaza 92.Watemi enzi zile walikuwa Okello( huyu jamaa kwa vichwa alikuwa kiboko), no Mbungi n shetani lakini shetani alimaliza mapema zaidi na alikuwa anajulikana sana.Kuna anayejua yupo wapi huyu.

Form one nilitishiwa maisha sana na mtemi mmoja wa form two aliyeitwa Onyango, eti alikuwa anataka aninyanganye shillingi kumi nauli yangu, nikakataa, form 2 nzima walinifukuza nikavuka barabara mpka kwenye kile kiosk cha mhindi, lakini jamaa waka give up.

Oh nakumbuka siku zile! Tulikuwa hatuna woga kabisa !
 
v3.jpg

It will always be in my memory,

Vurugu ya mwisho tuliingia Azania na chupa za mafuta yas petrol kama mabomu, nikiwa form two.

Tukarusha mabomu mawili laboratory ya Azania, wakawahi kuizima.Mara Azania wakatoka na makwanja , tumo ndani ya senyenge zao! Kilichotokea baada ya hapo inabaki historia.

Nilikimbia jangwani mabondeni huko nikakutana na tope linanuka vibaya sana, kuna wanafunzi wa azania walikuwa huko walikula kibano.It was war-like zone

Lakini nakiri afadhali walituhamishia mikoani, maana nisingemaliza salama, umri wa kubalehe ule na kufuata mob saikoloji ungetumaliza.

Ulikuwa ukituleta darasani moto wa kuotea mbali!! makonda walikuwa wanaheshimu Tambaza bwana

Label ya shule ilikuwa kali mpaka leo sijaona mfano wake, yangu ilikuwa kijani-group two!

SAMBUKILE-TAMBAZA!!!!!!!!!!!!!!!

Napenda tu kusema kuwa kati hao jamaa waliokwenda mkoa kuna jamaa niliwakuta pale Iyunga Tech sec. Mbeya(enzi hizo).
Jamaa kweli walikuwa distinguished character.
We ulienda wapi mazee?
 
Sikonge haya wabeja mayo!...naona Julius kakimbia...hivi swali langu ni hivi kwa nini shule nyingi za wanaume watupu tanzania or mchanganyiko zilikuwa na fujo sana na kujiona ni wababe kupita kiasi...shule kama Forest/kigurunyembe enzi hizo ilikuwa inaongoza kwa ufuska,tambaza kwa fujo,Ilboru handsome boys (some-to-do)...kuna shule moja moshi/arusha pia wavulana walikuwa na fujo sana nimeisahau jina....sijui kama zile tabia za zamani hadi leo bado zipo...

Bi Maringo,

Ngoja niweke maneno ya Waberoya:

Lakini nakiri afadhali walituhamishia mikoani, maana nisingemaliza salama, umri wa kubalehe ule na kufuata mob saikoloji ungetumaliza.

Nafikiri hii ilikuwa ikichangiwa na kukosa wanawake basi inakuwa ni bomu litakalolipuka muda wowote.

Wasichana kama wapo wanasaidia kutuliza ujinga wa wavulana. Wengine huwa wanabaki kuonyesha ubabe wao kwa Wasichana badala ya wenzao. Nakumbuka nikiwa Tech. College Arusha, vijana wa Ilboru walifunga timu zote kwa mpira na mwisho wakaja kwetu wakapata goli zao za kutosha na hawakurudi tena. Mwisho ukaja ugomvi wa Wasichana wa Machame Sec. Kuna graduation moja ya Ilboru wakaja Machame. Jamaa wachache wa TCA wakazamia na wakakipata kibano. Basi ilipofika next weekend jamaa wakaja kuangalia Video show pale TCA, wakatimuliwa. Ila kwa sababu kilikuwa ni chuo, wengine ni watu wazima na wengine na wasichana, hii kitu ilikufa wiki hiyohiyo. Wiki lililofuata jamaa hawakuwa na muda wa kukaa kuwawinda Ilboru wasizamie Video Show. Kwa hali ilivyokuwa pale ilikuwa inaonekana ni jambo la kitoto sana ingawa baadhi yetu kama tungelikuwa ni Secondary na wenzetu wamepigwa basi tungelitembeza kibano.

Nikiwa Mazengo tulishashika makwanja kwenda kuwatandika jamaa wa Mazengo Flats kwa sababu wenzetu wawili walipigwa na watu wa sehemu hiyo. Mungu bariki jamaa wakampelekea headmaster habari (Mzee Mkoba) na akaja mbio kututuliza na kuahidi atafuatilia hadi wjamaa wakamatwe na hilo lisirudie tena. Ila ilisaidia kwani baadhi ya mambo yalibadilika.
 
Wabs,

Aliyepiga picha hii atakuwa amesimama karibu na kisima fulani cha zamani kilikauka kikawa kama jaa la taka.

Hiyo picha inakumbusha mbali sana, hapo mlangoni kulikuwa na kijiwe cha kutesa njuka.

Haswaa mkuu, shule ukipita siku ya wikiend kimyaaa! si unajua mitaa ya upanga ile! subiri wakati wa kugawa chakula. wanafunzi tanzania tumetesa bwana acheni jamani, mtu uko day lakini bado unakula chakula cha mchana!!! na ole wako njuka uwe kimbelembele!!!

Napenda tu kusema kuwa kati hao jamaa waliokwenda mkoa kuna jamaa niliwakuta pale Iyunga Tech sec. Mbeya(enzi hizo).
Jamaa kweli walikuwa distinguished character.
We ulienda wapi mazee?

walinipeleka Umbwe-Moshi, siri kubwa ya ilikuwa umoja wa ajabu, watu wanaishi kama familia! tulifika umbwe tukastimulate hali ya mpira na vijana wacha waige mlegezo style ya kuvaa suruali, rap ndio zilikuwa zinaanza anza nchini, basi duh!

Namaliza Umbwe ile hali ya umoja wa wanafunzi ikawa imeenea kwa wote, uko nako tukalianzisha na shule ya jirani inaitwa Lyamungo, pigana sana baada ya kufungwa goli moja kwenye football!!!!, acha bwana; foolish age we iache tu!!

Iyunga Tech nayo ilikuwa familia ile ile ya shule za vurugu...

Bi Maringo,

Ngoja niweke maneno ya Waberoya:

Nafikiri hii ilikuwa ikichangiwa na kukosa wanawake basi inakuwa ni bomu litakalolipuka muda wowote.

Wasichana kama wapo wanasaidia kutuliza ujinga wa wavulana. Wengine huwa wanabaki kuonyesha ubabe wao kwa Wasichana badala ya wenzao. Nakumbuka nikiwa Tech. College Arusha, vijana wa Ilboru walifunga timu zote kwa mpira na mwisho wakaja kwetu wakapata goli zao za kutosha na hawakurudi tena. Mwisho ukaja ugomvi wa Wasichana wa Machame Sec. Kuna graduation moja ya Ilboru wakaja Machame. Jamaa wachache wa TCA wakazamia na wakakipata kibano. Basi ilipofika next weekend jamaa wakaja kuangalia Video show pale TCA, wakatimuliwa. Ila kwa sababu kilikuwa ni chuo, wengine ni watu wazima na wengine na wasichana, hii kitu ilikufa wiki hiyohiyo. Wiki lililofuata jamaa hawakuwa na muda wa kukaa kuwawinda Ilboru wasizamie Video Show. Kwa hali ilivyokuwa pale ilikuwa inaonekana ni jambo la kitoto sana ingawa baadhi yetu kama tungelikuwa ni Secondary na wenzetu wamepigwa basi tungelitembeza kibano.

Nikiwa Mazengo tulishashika makwanja kwenda kuwatandika jamaa wa Mazengo Flats kwa sababu wenzetu wawili walipigwa na watu wa sehemu hiyo. Mungu bariki jamaa wakampelekea headmaster habari (Mzee Mkoba) na akaja mbio kututuliza na kuahidi atafuatilia hadi wjamaa wakamatwe na hilo lisirudie tena. Ila ilisaidia kwani baadhi ya mambo yalibadilika.

Kweli mkuu, ila tuache utani kipindi kile ukimaliza boarding au shule za jinsia moja unatoka umeiva , zilikuwa zinafundisha maisha, I mean people were bright at that time,

Shule za wavulana tupu au wasichana tupu regardless day au boarding walikuwa wanafanya vizuri sana

Nasikia serikali inataka kuua kabisa boarding, mama yangu!!
 
Kuna huyo marehemu Puza,huyo aliwatesa sana Azania,lakini nafikiri ali commit sucide na mazishi yake yalihudhuriwa na mamia kama siyo maelfu ya waombolezaji...Alikuwa akitokea maeneo ya hapo Sinza "Kwa Mugabe"
 
Namaliza Umbwe ile hali ya umoja wa wanafunzi ikawa imeenea kwa wote, uko nako tukalianzisha na shule ya jirani inaitwa Lyamungo, pigana sana baada ya kufungwa goli moja kwenye football!!!!, acha bwana; foolish age we iache tu!!

Iyunga Tech nayo ilikuwa familia ile ile ya shule za vurugu...

Kweli mkuu, ila tuache utani kipindi kile ukimaliza boarding au shule za jinsia moja unatoka umeiva , zilikuwa zinafundisha maisha, I mean people were bright at that time,

Shule za wavulana tupu au wasichana tupu regardless day au boarding walikuwa wanafanya vizuri sana

Nasikia serikali inataka kuua kabisa boarding, mama yangu!!

Unakumbuka yale mambo mnatoka zenu mkoa kwa kukodi mabasi?
Si tulikuwa tukichukua gogo la TAZARA(kama unakuja dar nakumbuka wanafunzi tulikuwa tunalipa nusu sijui siku hizi), enzi hizo ilikuwa ubabe kwenda mbele,kuna siku tulikutana na watoto wa mwakaleli sec. humo kwenye gogo ilikuwa noma.
watoto wa Sangu,Meta na mbeya day wanatukumbuka vizuri(iyunga).

Ilikuwa mkisikia mmetangazwa kwenye vyombo vya habari kuwa mmefanya vurugu basi kwenu ilikuwa raha kweli.
Dah! kweli noma.
 
Bi Maringo,

Ngoja niweke maneno ya Waberoya:

Nafikiri hii ilikuwa ikichangiwa na kukosa wanawake basi inakuwa ni bomu litakalolipuka muda wowote.

Wasichana kama wapo wanasaidia kutuliza ujinga wa wavulana. Wengine huwa wanabaki kuonyesha ubabe wao kwa Wasichana badala ya wenzao. Nakumbuka nikiwa Tech. College Arusha, vijana wa Ilboru walifunga timu zote kwa mpira na mwisho wakaja kwetu wakapata goli zao za kutosha na hawakurudi tena. Mwisho ukaja ugomvi wa Wasichana wa Machame Sec. Kuna graduation moja ya Ilboru wakaja Machame. Jamaa wachache wa TCA wakazamia na wakakipata kibano. Basi ilipofika next weekend jamaa wakaja kuangalia Video show pale TCA, wakatimuliwa. Ila kwa sababu kilikuwa ni chuo, wengine ni watu wazima na wengine na wasichana, hii kitu ilikufa wiki hiyohiyo. Wiki lililofuata jamaa hawakuwa na muda wa kukaa kuwawinda Ilboru wasizamie Video Show. Kwa hali ilivyokuwa pale ilikuwa inaonekana ni jambo la kitoto sana ingawa baadhi yetu kama tungelikuwa ni Secondary na wenzetu wamepigwa basi tungelitembeza kibano.

Nikiwa Mazengo tulishashika makwanja kwenda kuwatandika jamaa wa Mazengo Flats kwa sababu wenzetu wawili walipigwa na watu wa sehemu hiyo. Mungu bariki jamaa wakampelekea headmaster habari (Mzee Mkoba) na akaja mbio kututuliza na kuahidi atafuatilia hadi wjamaa wakamatwe na hilo lisirudie tena. Ila ilisaidia kwani baadhi ya mambo yalibadilika.

Hizo issue za sec. na vyuo kuwa na maugomvi zilikuwa nyingi sana.
Jamaa wa Mbeya Tec. College wanakumbuka tulivyo kuwa tunagombea wasichana wa Loleza,siku chache baadaye tulikuwa tukienda kula wali huko huko.(MTC)

teh teh teh..... tulikuwa tunaita nyalini(kwenye wali)
 
Unakumbuka yale mambo mnatoka zenu mkoa kwa kukodi mabasi?
Si tulikuwa tukichukua gogo la TAZARA(kama unakuja dar nakumbuka wanafunzi tulikuwa tunalipa nusu sijui siku hizi), enzi hizo ilikuwa ubabe kwenda mbele,kuna siku tulikutana na watoto wa mwakaleli sec. humo kwenye gogo ilikuwa noma.
watoto wa Sangu,Meta na mbeya day wanatukumbuka vizuri(Iyunga).

Ilikuwa mkisikia mmetangazwa kwenye vyombo vya habari kuwa mmefanya vurugu basi kwenu ilikuwa raha kweli.
Dah! kweli noma.

Mkuu,
Sijui kama mlifanya fujo kama huyu binamu yangu. Huwezi amini kuna kaka yangu alipofika UDSM alianza kupata habari zaidi. Kuna vijana walikuja siku moja na kumuuliza "wewe SIKONGE, hivi yule Sizya SIKONGE ni ndugu yako?" Waliendelea kumpa story za UBABE wa jamaa miaka hizo.

Alikuwa akicheza mpira basi hata mpira uwe chini kama mita moja, yeye anapiga kichwa. Akipigana yeye kichwa tu. Ikianza fujo yeye anapita anagawa dozi ya vichwa tu. Shuleni Iyunga na shule za jirani walikuwa hawana hamu naye kabisa. Ila kama kawaida, form 4 alikula sijui Div.4??

Shule za boarding zilikuwa kali sana miaka hizo. Jioni mnakusanyika wengi na chaki zenu darasani. Mnawatafuta wakali wanakushushieni vitu ubaoni na mkitoka hapo, karibu wote mna Div. 1. Nakumbuka nikiwa Mazengo, vijana wa walikuwa wakiwa mwaka wa mwisho, wanasoma kimakabila. Mie na vijana wa Sikonge/Tabora tulifanya hivyohivyo. Katika kundi zima aliyefeli ni mie na nilipata Div2 huku nikipungukiwa 1 point kuingia 1. Ilikuwa masikitiko makubwa kuharibu rekodi yetu. Ila niliondika na A ya somo moja liitwalo Plumbing and Brick work na kama sikosei nilikuwa PEKEE Tanzania.

WABEROYA: Mshikamano wa Secondary zamani ulisaidia watu wengi sana. Mie ningelisoma shule kama za sasa ningelipata Div 4. Ila enzi hizo wenzio wanakubeba hadi vitu vinaanza kueleweka. Ukija mtihani na wewe unaonekana ni MKALI kumbe KIBONDEEEEE....
 
Siku ya kwanza ya kuripoti shule 'Njuka' wa Tambaza alimpiga 'fiksi'/'magirini' Njuka wa Azania kuwa yeye ni Kidato cha 2 ikabidi dogo wa Aza Boyz akubali 'mkwala' atoe hela ya kula mihogo na zile juisi zilizokuwa zinahifadhiwa kwa barafu za mortuary ya MMC!

Kwenye medani ya malavidavi mnaikumbuka hii: Tambazana vs Azajangwa?
 
Yaani mlikuwa mnamwibia Prof. Shaba barafu zake?

Ndiyo maana mie vya barabarani niliacha kula kabisaaaa hasa baada ya siku kuona JINGA moja likipa chafya kwenye maembe linayouza na tayari yameshamenywa....

Sasa Tambazana na Azajangwa ndiyo nini?

NB: Jamani ngoja nilale......
 
Back
Top Bottom