TRIBUTE: Pumzika Lowassa. Kazi umekamilisha, umeacha alama, mwendo umeumaliza. Watanzania wazalendo tutakukumbuka daima-1

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,499
113,608
Pumzika Lowassa Pumzika, Kazi Umekamilisha, Mwendo Umeumaliza, Pumzika!.
IMG-20240216-WA0113.jpg

20240218_084641.jpg

Toka kumetokea msiba wa Edward Lowassa hapa Jamiiforums tukimuita kwa jina maarufu la Mwamba wa Kaskazini, ile Jumamosi iliyopita, mpaka leo, akisubiri kupumzishwa kwenye makao yake ya milele, hapo kesho Jumamosi, mimi sikufanikiwa kuandika kitu chochote kumhusu Mwamba huyu, ila baada ya kupumzishwa sasa ndio angalau nitaweza kutulia na kuandika kitu muhimu kikubwa kumhusu Edward Lowassa, hii makala ya leo ni ya utangulizi tuu, makala yenyewe haswa ni wikieijayo.

Nilivyomfahamu Edward Lowassa

Kwa nature ya kazi yangu ya uandishi wa habari, nikihudumu kwenye vyumba vya Habari toka mwaka 1990 – 2020, na Lowassa alikuwa ni kiongozi, hakuna mwandishi yoyote wa Habari, hard news ambaye hakuwahi kukutana na Lowassa, hivyo nimekuwa nikim cover kwenye kazi mbalimbali za kihabari.

Siku zote na dunia nzima, Habari ni bure, hivyo sisi waandishi wa zamani, zaidi ya mishahara kwenye kazi zetu, tulikuwa tunaandika Habari bure, na japo mpaka sasa Habari bado ni bure lakini kuna Habari za bure, na kuna Habari lazima utumie gharama kuzipata ili uziandike.

Ziara za Lowasa ana Kuasisiwa kwa Mishiko kwenye Sekta ya Habari.

Lowassa akiwa Waziri wa Mifugo, nikapangiwa kuzungunguka nae kwenye ziara ya kutembelea ranchi za taifa, ofisi tulilipwa fedha za kujikimu na wizara ya mifugo ilitoa usafiri. Waandishi tukahesabiwa tuko wangapi, kwa kawaida waandishi huwa hatupangiwi gari maalum bali tunabananishwa katika magari yoyote ya kwenye pool na most times huwa ni magari mikweche na tunakuwa wa mwisho kufika kwenye tukio, lakini kwenye ziara za Lowassa, waandishi tumetengewa gari maalum na sio mikweche!, gari la waandishi lilikuwa magari ya mwanzo kwenye msafara na sio mwisho. Na kila tunapokwenda tunakuta tumeisha tafutiwa mahali pa kulala hotel nzuri wanazofikia viongozi, hivyo atakapo fikia yeye ndipo waandishi mtafikia hapo na zimelipiwa!, hizo ile per diem yote ya ofisini, unakunja unaisunda!. Kama hiyo haitoshi, kila jioni, unasainishwa bahasha nyingine nene yenye posho!. Mshiko, hivyo kwangu mimi ziara za Lowassa ndizo zilizonifungulia fursa ya mishiko ya waandishi au bahasha za waandishi.

Toka wakati huo Lowassa akaagiza kwenye mikutano, semina, warsha, makongamano na ziara za viongozi, kama mnalipana posho, waandishi wa Habari nao pia ni binadamu, hivyo nao wanastahi kulipwa posho, na hapa sasa ndio bahasha rasmi za waandishi zikaasisiwa na kurasimishwa!. Siku hizi kuna baadhi ya habari, bila kuwaangalia waandishi kwa hizi bahasha za posho, hawatoi kitu!, na imefikia hatua baadhi ya waandishi kuwa wawazi kama tukio halina posho, mimi siji na nikija sitoi!. NB. Mimi japo napinga rushwa ya aina yoyote kwa jina lolote, ila naunga mkono hizi bahasha halali za waandishi wa habari kwasababu hizi sio rushwa Waandishi wa Habari na Bahasha: Sio Kila Bahasha ni Rushwa

Wiki ya Maji.

Akiwa Waziri wa Maji, aliasisi Wiki ya Maji, enzi hizo nikiwa TBC Newsroom, ukaja ofisi mwaliko wa kuhudhuria wiki ya maji, barua ikasema wajigharimie usafiri, watarejeshewa fedha zao, mwaliko ule nikampanga Mhariri nipangiwe mimi, enzi hizo Mhariri Mkuu wa TBC ni Mshana, Siku zilipokaribia nikaulizia vipi hii trip, nikaelezwa kumetokea kazi nyingine nyingi muhimu zaidi, hivyo sisi TBC hatuna mtu wa Camera Kwenda ku cover, nikamwambia mhariri mimi nina camera yangu na nita cover mwenyewe, nikapewa ruhusa.

Hapa sio kuwa najidai, mimi ndio mwandishi wa Habari wa kwanza wa Tanzania kufanya kitu kinaitwa VJ (Video Journalist). Vyombo vyote vya Habari vinatumia watu wawili mmoja ni mwandishi wa Habari ni mwingine ni mpiga picha. Mimi licha ya kuwa ni mwandishi wa Habari, pia nilikuwa ni mpiga picha, hiivyo ikitokea upungufu wa wapiga picha, naaandika Habari mwenyewe, napiga picha mwenyewe, na nikifika newsroom naingia cut to cut mwenyewe kuihariri, na baadaye naingia studio kuisoma. Utaratibu huu wa VJ umenipatia trips nyingi sana za nje ya nchi.

Hivyo wiki yabmaji nikabeba camera yangu nikasafiri kwa gharama zangu, ilikuwa Arusha, japo nilitumia usafiri wa basi, kule Arusha nikajiongeza kwa kujisajili tuko wawili na tumetumia usafiri wa ndege, ili kurudishiwa nauli nene. Kwenye malipo walihitaji boarding pass!, ilikuwa shughuli kupata boarding pass mbili!.

Kazi ya kwanza ni kumtafuta mtu wa kujifanya ndie cameraman wangu, nikampata nikampiga picha na kumsajili ni mpiga picha wa TBC!, Wakati wa kusaini posho, si wale jamaa wa malipo, wakaomba kila mtu aonyeshe kitambulisho cha ofisi!. Duh…nikajiuliza sasa itakuwaje?, akili ikaninijia mimi na yule mtu wangu tukaingia steshenari, tukadurufu kitambulisho changu, tukatoa kitambulisho kingine chenye jina la mpiga picha halisi wa TBC lakini picha ya mtu mwingine. Mpango huu ukafanikiwa, nikavuta mpunga wa nguvu, na pesa shetani, baada ya kuzishika, yule jamaa ambaye tulikuwa tugawane, baada ya kulipwa, aliingia mitini!, kitu kibaya zaidi sio kunitapeli pesa, bali alitokomea na kile kitambulisho fake chenye jina halisi la mpiga picha wa TBC.

Nilirudi ofisi, nikaandika story yangu na kuwatengenezea kipindi, huku nyuma yule kanjanja wangu akiendelea kufanya ukanjanja kwenye matukio mbalimbali mbali ya kihabari kwa kujifanya ni mtu wa TBC, siku ya siku, akadakwa, akanitaja!, moto ukaniniwakia!.

Jee nini kilitokea baada huyu jamaa kujitaja mimi ndio nilemtegengeneza kitambulisho fake cha TBC?. The essence ya story hii ni kuonyesha how far people can go and can do to make money!, kisa ni ili tuu kuvuta mishiko ya Edward Lowassa. Hili la Lowassa kupigania posho kwa waandishi wa habari, limetuheshimisha sana wana tasnia wa habari nchini.

Tukutane wiki ijayo kwa sehemu ya pili ya Buriani ya Lowassa ambapo pia utakisikia kisa jinsi Edward Lowassa alivyookoa maisha ya Mtanzania mmoja ambaye almanusura afie huko Rome nchi Italy!.

Pumzika Lowassa Pumzika!, Kazi Umekamilisha, Umeacha Alama, Mwendo Umeumaliza, Watanzania Wazalendo, Tutakukumbuka Daima, Pumzika!.

Paskali
Update
Makala mwendelezo Lowassa alikipenda kiti moto kipindi!. Aliokoa maisha yangu Rome Italy!. He was "Of the People, By The People, & For The People!" ADIOS... AMIGOS...!.
P
 
Na hapo ndipo kwenye shida kubwa tanzagiza, unasifia lowasa kuwalipa posho na kugharamia watu wasio waajiriwa wa serikali unaita ni ubinadamu, swali je hiyo bajeti imetokea wapi? hiyo fedha mliolipwa aliitoa mfukoni au serikalini? vp kuhusu auditing? kwa maana kila senti ni lazima iwe kwenye bajeti na maelezo ya ilivyotumika, hamna tofauti na raisi samia anayenunua magoli, hali ya kawaida akipaswa kutolea maelezo kwa kugawa fedha za walipa kodi kama mali yake binafsi.

Ukitaka kujua kwa nini sisi ni masikini soma hilo gazeti hapo juu …
 
na hapo ndipo kwenye shida kubwa tanzagiza, unasifia lowasa kuwalipa posho na kugharamia watu wasio waajiriwa wa serikali unaita ni ubinadamu, swali je hiyo bajeti imetokea wapi? hiyo fedha mliolipwa aliitoa mfukoni au serikalini? vp kuhusu auditing? kwa maana kila senti ni lazima iwe kwenye bajeti na maelezo ya ilivyotumika, hamna tofauti na raisi samia anayenunua magoli, hali ya kawaida akipaswa kushitakiwa kwa kutumia na kugawa fedha za wakipa kodi hovyo kama mali yake binafsi.

ukitaka kujua kwa nini sisi ni masikini soma hilo gazeti hapo juu …
maadam ni watanzania hamna shida

Serikali sio lazima iwalipe watumishi wake tu, hata na raia wake wanyonge pale inapowezekana wanalipwa, Mfano ni TASSAF

Waandishi walifanywa wanyonge na waajiri wao yeye akawaheshimisha, sioni shida
 
maadam ni watanzania hamna shida

Serikali sio lazima iwalipe watumishi wake tu, hata na raia wake wanyonge pale inapowezekana wanalipwa, Mfano ni TASSAF

Waandishi walifanywa wanyonge na waajiri wao yeye akawaheshimisha, sioni shida

siyo tatizo, swali ni kwamba hiyo fedha inatokea wapi? kuna bajeti iliyotengwa na serikali kwa ajili ya kuwalipa wasio waajiriwa? point iko hapo, umeongelea tasaf, fedha ya tasaf inajulikana ilikotoka, kwa nini hata kuna bunge la bajeti basi kama kila mtawala anaweza kuchukuwa fedha na kugawa anavyojisikia?

ili nchi iweze kuendelea ni lazima kila senti iwe accounted for, book keeping ifanyike na fedha ilipwe kwa kufwata sheria na siyo matakwa ya mtu binafsi halafu mnaiita “ubinadamu” …
 
Jinsi Chadema walivyokubali kununuliwa awe mgombea na jinsi wanavyolilia attention kwenye huu msiba ni very very sad .... Lowassa legacy ni kuwavua nguo wapinzani waliomtukana na kumuita fisadi halafu wanamlilia alivyokufa na wanamuita mzalendo
 
Back
Top Bottom