maiyanga1
JF-Expert Member
- Mar 1, 2017
- 1,317
- 1,790
Jana tumesikia bodaboda wa Korogwe walivyojichukulia sheria mkononi na kulichoma moto bas la Saibaba, baada ya mwenzao kugongwa na kufariki. Mashuhuda wanasema bodaboda aliingia barabarani bila tahadhari.
Maeneo kadhaa nchini bodaboda hawazingatii sheria, chakushangaza zaidi wanaweza kufanya hivyo mbele ya askari wa usalama barabarani. Lakini inapotokea ajali hata kama imesababishwa na bodaboda bado dereva atashambuliwa na gari itaharibiwa.
Mara kadhaa tunashuhudia wanavyo pitia kushoto wakati wa kulipita gari lililoko mbele, wanavyopita bila kusimama kwenye vivuko vya wenda kwa miguu, wasivyotii taa za kuongozea magari, achilia mbali pikipiki kubeba abiria zaidi ya mmoja na kutokuvaa helmet.
Kwanini bodaboda huwa hawachukuliwi hatua wanapovunja sheria za barabarani?