CCM ihalalishe rushwa kwa kuwa imeshindwa kuidhibiti

Sir robby

JF-Expert Member
Jun 22, 2022
2,400
4,073
Wadau habari,

Moja ya ahadi za Mwana- CCM ni hii
Rushwa ni Adui wa Haki Sitapokea wala kutoa Rushwa.

Ahadi hiyo imethibitika kushindikana ndani ya CCM kama Chama Tawala na SERIKALINI kwa sababu viongozi wote wa Serikali, Bunge na Mahakama pamoja na majeshi yetu ni wanachama wa CCM japo kwa uficho na kulijua hilo mpaka uwe na akili kubwa.

CCM imekuwa kwenye chaguzi zake toka ngazi ya Chini mpaka taifa, Chaguzi ambazo zimegubikwa na malalamiko makubwa ya utoaji na upokeaji wa rushwa pamoja na Serikali kuwa na Chombo cha kupambana na RUSHWA TAKUKURU lakini chombo hicho kimeshundwa Kabisa kuzuia rushwa ndani ya CCM na kupelekea CCM kuchukua Hatua za kufuta Baadhi ya chaguzi kitu ambacho Kilishangaza WATU kwani tulio Wengi Tulitarajia CCM ingewafikisha TAKUKURU ili watoaji na wapokeaji wafikishwe mahakamani.

Kutokana na CCM kushindwa KUIDHIBITI RUSHWA tunaishauri CCM na SERIKALI yake IHALALISHE RUSHWA ili ITOLEWE na KUPOKELEWA HADHARANI

Kidumu CHAMA CHA MAPINDUZI
 
Soma gazeti hili

mwananchi_official_1669443731679119.jpg
 
Sasa CCM na rushwa tangu lini vikaachana?

Ni sawa na kusema unataka utenganishe udugu baina ya ndugu wawili wazaliwa wa tumbo moja.
 
Kamwe ccm haiwezi kupiga vita rushwa hata mara moja kwani wao ndio waasisi, waleaji, wapokeaji, waboreshaji!
Yaani ni chanda na pete
 
Back
Top Bottom