SoC03 TAKUKURU tumieni njia hizi kupambana na rushwa ya ngono katika Taasisi za Elimu ya Juu

Stories of Change - 2023 Competition

Lidafo

JF-Expert Member
Sep 26, 2019
551
747
Rushwa ya ngono imekuwa ni tatizo sugu hasa katika Taasisi za elimu ya juu, Usugu wa tatizo hili unachangiwa na pande zote mbili yaani mtoaji rushwa hapa namanisha wanafunzi lakini pia waombaji rushwa yaani wahadhiri na wakufunzi wa vyuo vikuu.

Madhara ya rushwa ya ngono yanaonekana waziwazi athari zake Kiuchumi kwani wale wasio na sifa wanapewa mamlaka wasiyoweza kuendesha lakini pia kijamii kwani rushwa ya ngono ni uvunjaji wa haki za binadamu.

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU), Imekuwa ikitoa miongozo mbalimbali katika kupambana na rushwa ya ngono hasa vyuoni. Jitihada hizo zimetoa athari katika kukabiliana na tatizo hili ila bado tunatakiwa kuongeza mbinu na njia mbalimbali kama taifa kuhakikisha tunapambana na tatizo hili kisawasawa.

Hivyo basi ikiwa ni wajibu wa kila Mtanzania kutoa maoni yake juu ya wapi na kipi kiboreshwe, Napendelea kushauri TAKUKURU kutumia njia hizi mbili nitakazo zielezea katika kupambana na Rushwa ya ngono taasisi za elimu ya juu.

1. KUONGEZA SEHEMU YA KUWEZESHA WANAFUNZI KUTOA TAARIFA DHIDI YA RUSHWA YA NGONO KATIKA MIFUMO YA ARIS VYUO VIKUU

Katiaka Taasisi za elimu ya juu kila mwanafunzi anakuwa na akaunti ya ARIS ambayo itamwezesha kuona matokeo yake pamoja na taarifa mbalimbali, Mfumo huu wa ARIS umerahisisha mambo mengi katika utendaji kazi vyuo vikuu.

Hivyo TAKUKURU katika kuhakikisha kuwa inapambana na rushwa ya ngono vyuoni ni vizuri wakaongea na taasisi zote za elimu ya juu na serikali ikaweka sheria kwamba kila taasisi ya elimu ya juu kuwa na sehemu itakayo mwezesha mwanafunzi kutoa taarifa kupitia akaunti yake ya ARIS na sehemu ya utoaji taarifa iunganishwe moja kwa moja na ofisi za TAKUKURU ili pale ambapo mwanafunzi ametoa taarifa, Mfano mhadhiri fulani kutoka chuo fulani ameomba rushwa ya ngono TAKUKURU waweze kuona na haraka kuanza kufanyia kazi.

FAIDA ZA NJIA HII
  • Kutoa nafasi ya wazi Kwa kila mwanafunzi aliyeombwa rushwa ya ngono au kufanyiwa vitendo vinavyoashiria rushwa ya ngono kuwa huru kutoa taarifa pasina mlolongo mrefu, Hivyo inatoa urahisi wa utoaji taarifa.
  • Kuwawezesha maafisa wa TAKUKURU kupata taarifa za moja kwa moja kutoka kwa Wanafunzi wa vyuo mbalimbali na hivyo kuwa na takwimu nzuri ya vyuo gani ni tatizo na vimekithiri kwa rushwa ya ngono na hivyo ni rahisi kwa TAKUKURU kuandaa mipango kazi itakayo saidia kupambana na rushwa ya ngono kwa chuo husika.
  • Njia hii inatoa usiri dhidi ya mtoaji taarifa na hivyo ni rahisi kwa maafisa wa TAKUKURU kuandaa mtego wa kumnasa mlalamikiwa yaani wafanyakazi wa vyuo mbalimbali kama wahadhiri na wataalamu mbalimbali upande wa uongozi.
  • Kuongeza uwoga na wasiwasi kwa wahadhiri kwani watahofia kufikishwa katika mamlaka husika na hivyo kuwa na mazingira ya heshima kati ya wahadhiri wa vyo vikuu na Wanafunzi.

2. KUWA NA OFISI YA TAKUKURU KWENYE KILA TAASISI YA ELIMU YA JUU.

Hapa TAKUKURU inatakiwa kumuweka afisa TAKUKURU kila chuo, Afisa huyo atakuwa anapokea taarifa za walalamikaji lakini pia afisa huyo atakuwa anasaidia kutoa elimu kwa wanafunzi na wahadhiri juu ya athari za rushwa ya ngono, Kwa nchi kama Tanzania ni rahisi kufanya njia hii kwani hatuna ukwasi wa taasisi nyingi za elimu ya juu idadi ya afisa TAKUKURU mmoja katika kila taasisi ya elimu ya juu ni idadi ambayo kama taifa tunaweza kuimudu.

FAIDA ZA NJIA HII

  • Njia hii inatoa fursa kwa wanafunzi kueleza changamoto zao kwa maafisa wa TAKUKURU lakini pia inatoa fursa kwa maafisa wa TAKUKURU kutoa ushauri kwa wanafunzi juu ya mienendo yao na mavazi kwa ujumla, Jambo ambalo pia kwa kiasi kikubwa limechangia kukua kwa rushwa ya ngono vyuoni.
  • Kuongeza uwoga kwa wakufunzi kwa kujua kuwa afisa TAKUKURU yupo eneo la chuo na anafanyakazi kwa karibu zaidi.
  • Njia hii inatoa nafasi Kwa maafisa TAKUKURU kuandaa semina na kuunda vikundi mbalimbali vya upingaji rushwa ya ngono vyuoni, Yaani njia hii inatoa fursa Kwa wanafunzi kupata elimu ya maswala ya rushwa sio tuu rushwa ngono bali pia rushwa Kwa ujumla wake.
  • Kuwafanya maafisa TAKUKURU kushiriki katika shughuli mbalimbali za utoaji elimu vyuoni na hivyo kuwa sehemu ya kuwaandaa wahitimu bora na kupata wafanyakazi wenye kujali utu na wenye elimu ya kutosha kuhusu rushwa ya ngono na madhara yake Kwa taifa.
HITIMISHO
Rushwa ya ngono inachangiwa na pande mbili, Upande wa wakufunzi wa vyuo na upande wa Wanafunzi hivyo basi ni vizuri kwa wanafunzi wa vyuo vikuu kuzingatia maadili ya uongeaji na uvaaji wanapo amiliana na wakufunzi wao vyuoni huku wakiwa na msimamo katika kukemea na kupaza sauti kwa mtu yeyote anayetumia mamlaka kurubuni na kuahidi kutoa nafasi ya upendeleo kwa kigezo cha kupewa rushwa ya ngono.

Wadau mbalimbali na asasi za kijamii pia zisichoke kutoa elimu na misaada mbalimbali ya kisheria kwa wahanga wote walioathirika na uvunjwaji huu wa haki kwani rushwa ya ngono inatoa nafasi ya upendeleo kwa asiye stahili na hivyo kama taifa tunaingia katika tatizo la kuwa na wahitimu wasomi wasio na sifa na hivyo kuletea taifa hasara kubwa.

Kwa pamoja tunaweza, Ewe Mtanzania amka na kemea rushwa, Anza wewe na mhamasishe mwingine ewe afisa TAKUKURU timiza wajibu wako ili kuijenga Tanzania imara.
 
Mawazo mazuri, lakini hiyo ya kumuweka afisa takukuru katika kila chuo nayo ni shida, walimu wakikuona unaingia ofisi ya takukuru, wanakumark kuwa unawachoma, mwisho wanakukamata makusudi ili urudie mwaka au udisco kabisa.
 
Changamoto hiyo inaweza kuwepo lakini tukumbuke pia sheria zipo zinazomlinda mwanafunzi, Na hii itakuwa ni rahisi kubaini kama kuna mhadhiri anafanya hujuma hizo kwani itakuwa ni jinsia ke dhidi ya jinsia me.
Lakini pia ikitokea mwanafunzi amefanyiwa hujuma na hajaridhika na matokeo sheria ina mruhusu kukata rufaa na mitihani yake itapitiwa upya kama kuna hujuma zitaonekana tu na hapo ndipo sheria kali zaidi zitachukuliwa kwa mhusika.
Lakini pia, Uwepo wa afisa TAKUKURU chuoni utasaidia sio tu kupambana na Rushwa ya ngono lakini pia Rushwa yeyote itakayofanyika chuoni kwani kuna wanaume wanawapa pesa wahadhiri ili wavujishiwe mitihani, Kwahiyo uwepo wa maafisa TAKUKURU vyuoni bado una umuhimu mkubwa na faida nyingi kulinganisha na changamoto zitakazo jitokeza.

Ok sawa.
 
Back
Top Bottom